Wanachama wa Simba na Yanga wote wana Tatizo moja la msingi. Tatizo Hilo ni "MAARIFA NA WELEDI" juu ya soko la soka.
Suala la kununua au kukodi klabu sio Tatizo. Tatizo ni kwa kiasi gani unaweza kufanya "mapatano" ya kuuza au kukodi kitu ambacho hujui thamani yake. Chifu Mangungo wa Msovero alifanya hivyo, serikali imefanya hivyo, ni ajabu na aibu kwa wanachama wa Simba na Yanga kurudia makosa yale yale.
Mbali ya majengo na rasilimali zenye kuonekana Simba na Yanga wana rasilimali kubwa isiyoonekana ambayo kitaalamu inaitwa "GOODWILL". Je, ni nani kati yetu ajuae thamani ya vilabu hivi viwili. Tunahitaji kwa hakika na bila shaka kujua thamani halisi ya vilabu hivi ili mchakato ima wa kukodisha au kuuza hisa ufanyike.
Yanga na Simba ni migodi inayotembea, tuitendee haki. Wapo watu waliozifanya klabu hizi kuwa hapo zilizopo, ni aibu na fedheha kubwa kwetu kudharau michango ya wazee wetu hao na kuzitoa klabu hizi bure. Kama sio kutetemeka basi watatikisika huko "MAKABURINI".