Yusuph Mwenda: Kati ya watanzania Milioni 62, wanaolipa kodi ni Milioni 2 tu

kwamba watu mill 2 tu ndio wanalipa kodi wengine wote wakinunua bidhaa hua hazijaongezewa kodi ya VAT ? Au kodi ni ya PAYE(pay as you earn) peke yake ?
Direct tax. Kodi ya moja kwa moja. Indirect tax zinalipwa na watanzania wote. Tax base ya direct tax inatakiwa kuongezeka, hii nchi direct tax inalipwa na watu wachache sana.
 
Kila mtanzania analipa kodi
 
Direct tax. Kodi ya moja kwa moja. Indirect tax zinalipwa na watanzania wote. Tax base ya direct tax inatakiwa kuongezeka, hii nchi direct tax inalipwa na watu wachache sana.
ok, sasa hao wanaotakiwa kulipa direct tax ni kina nani? Na wapo wangap?
 
Kila bidhaa inayoliwa nchi hii imepigwa kodi zaidi ya moja .
Huyu mpumbavu naye anapewa cheo cha TRA na hajui kwamba kila bidhaa inayotumika au kuliwa na hao watu milioni 60 ambao asilimia zaidi ya 70 ni hohehahe wa kutupwa nchini humu imepigwa Lundo la kodi .
 
Au ndio akili za kuwaza kodi ni mpaka paye na importation taxes au service levy Tu ?
 
Wenye uwezo hawapewi hicho cheo
Hamna kamishina wa kodi hapo
 
Anajua kuliko wewe,hajaokotwa huyo amekulia humo TRA
 
Sio kweli Watz wengi wanalipa kodi (VAT) kupitia manunuzi ya bidhaa mbalimbali wanazotumia majumbani mwao. Pia wanalipa kupitia mitandao ya simu wanazotumia, Luku (Property tax). Huyu anajaribu kutupanga sasa akishindwa kukusanya VAT kutoka kwa wafanyabiasha wakubwa ambao hawapeleki makusanyo ya VAT iliyolipwa na watz. Hivyo kusema eti watz 2 million ndio wanaolipa kodi tu ni uongo wa wazi kabisa. Huduma nyingi zitolewazo kwa watz zinalipiwa kodi kwa njia moja ama nyingine.
 
Hayo mambo ya kushangaa walipa kodi ni wachache bila kufanya utafiti wa kwanini na kufanya general soln ndiyo mwisho mnakuja na njia za ulipaji kodi za lazima ambazo mwisho zinafail na kuleta mkanganyiko kwenye jamii

Ukitaka kuongeza tax base create mazingira ya kuongeza fursa za watu kufanya kazi, shusha ushuru bandarini watu waweze kuagiza bidhaa kwa unafuu wafanye biashara, ondoa ushuru au upunguze kusaidia bidhaa zisafirishwe kwa urahisi toka mashambani kwenda masokoni watu wafanye biashara na njia nyingine ukistimulate biashara watu wengi watafanya biashara, kazi na utakuwa na watu wenye kipato hata ukiwataka walipe kodi hakuna atakayekataa

Sasa kwa hali hii hata uje na mbinu gani huwezi kuongeza zaidi ya kusababisha migogoro uongeze kodi kwenye jamii iliyotoka kulia kwa ongezeko tu la 500 kwenye luku!? Ambayo nami nililia inatosha kuonyesha hali ya watu mifukoni ni mbaya sana
 

View:
 
Sio lazima ajue idadi lakini kila mmoja analipa kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…