Yusuph Mwenda: Kati ya watanzania Milioni 62, wanaolipa kodi ni Milioni 2 tu

Ko hizi zinazokatwa kwa kununua umeme na vocha zinaenda wapi???

Mwamba anashindwa kung'amua hata kwa akili ya kawaida tu, basi tufanye aliyosema ni kweli, lakini watawala ndio wametaka hao watu milioni 2 ndio walipe kodi kwa sababu hawana fikra za kutengeneza walipa kodi wengi, wameshindwa kutengeneza miundombinu rafiki kwa wananchi kufanya kazi, hamna ajira, hamna matumizi sahihi ya rasilimali zetu, ni kula na kuzurura ndio kazi pekee wanayoijua.

Ila wakae wakijua kuwa Tanzania ni ya wote, ipo siku hali hii itabadilika na vizazi vyao vitapitia magumu kama haya wanayotupitishia sisi.
 
Kodi hutozwa matajiri aka mabilionea. Masikini huwa hawatozwi kodi. Hii ndiyo kanuni kuu ya government taxation.

Hata huko Marekani ni kodi za mabilionea ndizo huendesha matumizi ya serikali aka government budget. Hata kwenye ngazi ya familia ni kipato cha head of family ndicho huendesha matumizi ya familia aka family budget.

Serikali inachotakiwa kufanya ni kuwezesha kuzalisha mabilionea wengi ili iweze kupata pesa zaidi kutokana na kodi zao. Sisi tumekazana kukimbizana na masikini (wanyonge) kuwakamua kodi. Hadi watoto walio bado tumboni mwa mama zao tunawatoza VAT hususani kwa vyakula vyao ambavyo huvipata kupitia kile wanachokula mama zao through their placenta. Nguo za watoto na mahitaji mengine ya watoto tunazipiga VAT ya 18%. Watanzania wote million 62 wanalipa kodi ya VAT irrespective of their status including those who are in ICUs. Sasa huyu kamishina mpya wa TRA bado anasema hii haitoshi.

TRA ndiyo kikwazo kikuu cha kuzalisha mabilionea. Utakuta mtu anayejaribu kujiinua kibiashara anaanza kutozwa kodi lukuki kabla hata biashara yake haijainuka au haijaanza kabisa. Wanapaswa kusubiri hadi pale anapokuwa bilionea.
 
Kule halmashauri kuna tenda za ujenzi zinatolewa kwa kampuni mbali mbali za ujenzi sasa ili kuweza kukusanya kodi katika eneo ilo kila kampuni inayopewa tenda iwe inaleta paylist yawafanyakazi wake katika mradi usika ili Kila inapo produce certificate ili kulipwa wafanyakazi wa hyo kampuni nao wakatwe kodi. Sio kampuni inaenda kuokoteleza vijana mtaani nakuwalipa buku tatu kila siku. Wafanyakazi wanatakiwa wawe na mikataba bila kufanya hvyo kampuni zisipewe tender.
 
Hakuna ukweli wowote hapo.

Kila mTz asiye na ajira rasmi analipa kodi indirect kupitia Vat.

Wafanya kazi na wafanya biashara wakubwa utaratibu unaeleweka.
Pamoja na kufulukuta kote serikali haijafikisha watumishi laki saba.
 
Nikinywa la Pepsi tiyari nishalipa Kodi wanazungumzia Kodi Gani au hizi wanazochezea kina bashite na kina mwigulu?
 
Siwezi kulipa kodi directly ili hawa wajinga wazitumie hivyo namna hii.
Kuna mapato naingiza kila mwezi zaidi ya 6m ningetakiwa niyadeclare tra ili niwe nayalipia kodi ila sifanyi hivyo ng'o na fedha zenyewe nalipwa mkononi .
Haiwezekani niangaike nitengeneze base ya mapato halafu wajinga wazitumie hovyo namna hii
 

Attachments

  • 5772829-61bcb6aead70ef320cbcacf28f10751.mp4
    1.4 MB
Sioni sababu ya yeye kushangaa ila kama kiongozi wa taasisi nyeti inabidi aje na mkakati mzuri wa kuongeza mapato kwa wingi.
Lakini kwa mtazamo wangu tatizo kubwa njia nyingi za uchumi kwa taifa letu tumewapa wageni ni ngumu sana kukusanya mapato kwa watanzania ilihali wengi wao ni machinga na vibarua.
 
Kodi tunalipa aache uongo wake nimekula ugali huu unga umenunuliwa dukani duka ambalo wakala wao wa mapato muuza duka kaniuzia ambae nae aliponunua ule unga ulikatwa kodi chai sukari kodi imepita majani ya chai kodi yangu imepita shwaa hawa wanataka kodi gani tena au kodi ya moyo?
 
Huo ndiyo ukweli🤔, labda atasaidia kuongeza taxes payee bas kwa kuwa amelijuwa hilo.
Siyo wale wengine wanakomaa na hao 2 m badara ya kutanua wigi wa walipa kodi mika yote hawaongezeki.
 
Hata kama vijana ni %50 haondoi ukweli kuwa wanabebwa na %2 tu ya walipa kodi.
 
Huo ndiyo ukweli🤔, labda atasaidia kuongeza taxes payee bas kwa kuwa amelijuwa hilo.
Siyo wale wengine wanakomaa na hao 2 m badara ya kutanua wigi wa walipa kodi mika yote hawaongezeki.
TRA ni wavivu kama walivyo TAKUKURU mpaka kiongozi aseme flani achunguzwe ndipo wanatoka ofisini kufanya kazi.Wapo wafanyabiashara kibao hawana TIN na hata LESENI hawana, wanachojua ni kulipa kodi ya mwenye nyumba basi.
 
Kila bidhaa inayonunuliwa na mlaji wa MWISHO inalipiwa kodi hadi sanda ya maiti.
Mnataka kodi gani zaidi iliyosahaulika?
Mumetengeneza ajira ngapi mpya ili kuongeza walipa Kodi?
 
Hao wengi ni wangapi? Wako wapi? Maana unasema tu wengi bila kusema ni ngapi na wako wapi
Huelewi maana ya wengi na wakati gani neno wengi linatumika!!? Rudi darasani.
 
Reactions: Ame
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…