Yutong/zongtong/Higer and scania buses

Yutong/zongtong/Higer and scania buses

Na hizo Scania model za sasa hivi ajali zake nyingi ni kugonga punda na wanyama wengine bara barani na litatoka tuu nje ya bara bara si kama ajali za bongo Basi unaona matairi yapo yote juu mabasi hayana balance kama vigari vidogo tuu..
 

Huko hamna kitu hamfikii scania hata kwa dawa
Wasafirishaji wa mizigo wengi wanatamani kupata Actross na wanayoyajua ma Truck kama wasomali waliopo msumbiji wao ni Actross tuu wanatushangaa sisi na Scania msomali akija mnadani asipokuta Actross na zipo scania, volvo na man zipo yeye anasema hakuna gari leo na bei ipo juu zaidi ya hayo yote..,
 
usifanye mchezo na Leyland CD. Pia Volvo wako vizuri sana. Unazikumbuka basis za Zainabs?

Nazikumbuka Zainabs, zilikua zinapiga kama sio Mbeya, Songea. Kuna siku ilitupita tupo kwenye Tawaqal, sis wenyewe tulikua tupo moto bati lakini alituachia vumbi tena sio ile kidogo kidogo, ni ile jamaa anapotea kama mmesimama.

Nafikiri alikuja kumuuzia Shabiby hizo basi.
 
Isanga family kitu unachoshindwa kutofautisha ni kimoja, kwa upande wangu nimesifia mabasi ya wachina kwa sababu wanaelewa mahitaji ya soko. Ukiongelea uimara na ubora, Scania, Volvo, Benz, Leyland and the likes ndio magwiji, tatizo linakuja pale ambapo bei yao iko juu sana kulinganisha na mchina.

Sasa hata kama Scania inadumu, lakini itakua imechakaa, hauwezi kulinganisha na Mchina mpya hata kama hatadumu sana lakini abiria ndio wanachokihitaji, anasa. Mchina kwa anasa hajambo mkuu. Hizo picha za mabasi ulizoziweka umeshawahi kuziona hapa bongo? Unafikiri ni kwanini? Biashara inahitaji kusoma upepo wa mwenendo wa soko unavyoenda. Unaweza kuwa na bidhaa bora kuliko washindani wako wowote, lakini kama hakuna soko na watu wanakimbilia mbadala lazima ubadili formation ya mchezo kutokana na mchezo unavyoenda.
 
Hapa tunaongelea vitu viwili tofauti, nakubali kwamba kwa uimara na umathubuti, Scania hana mpinzani lakini hicho kinazifanya ziwe na bei ya juu sana kwa wafanya biashara. Mchina amekuja na gari zake zenye kila aina ya anachohitaji abiria nikimaanisha comfortability na anasa zote. Juzi nimepanda moja wameweka hadi USB port unacharge simu yako, haukosekani hewani kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari.

Unaposema Mchina hawakamati akina Scania, weka bayana kwa upande upi, uimara wa gari au soko? Fanya uchunguzi kidogo tu, nenda ubungo stand ya mabasi, angalia kati ya mchina na Benz, Scania mabasi gani mengi?
bora umenena sie abiria tunataka gari quality na mwendo mzuri siyo wakukimbizana kama mtoa mada anavyosuggest
 
yutong,zutong NEW FORCE HANA MPINZANI KWASASA HAPA EAST AFRICA NA ATATEKA HADI AFRICA YOTE
 
Samaritani hayo mabasi hapa hakuna kwa sababu vitu vizuri vinaonekana anasa hapa kwetu ndio maana hao watanzania wenye mabasi hayo wamewekeza Zambia, South Africa na Zimbabwe sio kwamba wanashindwa kuleta huku ni vitu vingi vinafanya biashara ya mabasi quality kutokuja hapa na si kweli yakija mabasi bora kama hayo watashindwa kufanya kazi hapa ni vile wameona kule kwa sasa ni faida mara dufu zaidi ya hapa...
 
Ok mkuu nimekuelewa kumbe unazungumzia Ubungo nilidhani unazungumzia kwa Nchi zinazobeba mizigo mingi Africa kama South Africa,Zimbabwe, mozambique na Zambia ndio maana mnaipitisha Scania..

Weka utafiti wako hapa uone market trend ya soko la Scania na Mabasi ya asia uone, unafikiri tunaongea tu mkuu, au kosa imekua kutaja ubungo imekua nongwa?
 
mchina ni nomaaaa.. kwa huduma ndani ya basi..

na.hata kwa mfanyabiashara hela inarudi na faida anaipata fasta tu..

scania milion 100 huku mchina milion 50.. sasa tajiri gani mwehu anunue scania wakati mchina anarudisha hela yake fasta fasta tu
 
Weka utafiti wako hapa uone market trend ya soko la Scania na Mabasi ya asia uone, unafikiri tunaongea tu mkuu, au kosa imekua kutaja ubungo imekua nongwa?
Mkuu sio swala la utafiti hapo nikuelekeze kitu kimoja Nchi za kusini mfanyabiara ananunua basi mpya harafu yeye anakodisha kwa wasafirishaji maeneo ya Limpompo unakuta kaburu ana mabasi Scania kama ya ubungo hayo yote tena anakua na yard tatu mpaka tano na wapo wengi...sasa hivi wanachukua za kichina kwa ajili ya Zimbabwe na Zambia, SA hawajazi thibitisha ubora wake kwa matumizi yao kwa sasa ila nadhani wataingia mkuu mimi sipo kubishana hapa na utafiti ufanyike wa dunia au wa Ubungo...?
 
Mkuu sio swala la utafiti hapo nikuelekeze kitu kimoja Nchi za kusini mfanyabiara ananunua basi mpya harafu yeye anakodisha kwa wasafirishaji maeneo ya Limpompo unakuta kaburu ana mabasi Scania kama ya ubungo hayo yote tena anakua na yard tatu mpaka tano na wapo wengi...sasa hivi wanachukua za kichina kwa ajili ya Zimbabwe na Zambia, SA hawajazi thibitisha ubora wake kwa matumizi yao kwa sasa ila nadhani wataingia mkuu mimi sipo kubishana hapa na utafiti ufanyike wa dunia au wa Ubungo...?

Nimekusoma mkuu, uliposema kumbe naongelea Ubungo ndio nikataka nikutahadharishe kwamba wachina wanakuja juu sana, na ni threat kwenye kila idara. Tatizo lao vitu havidumu na vingine uimara unakua mzozo. Unaona hata makampuni makubwa wameenda kufungua ofisi zao huko kupunguza gharama za uzalishaji?

Ndio maana magari ya mizigo hana ushawishi sana, hali kadhalika makatapila huko dado wakongwe kama CATs na Volvo wataendelea kutawala.
Nimekupata vizuri sana mkuu.
 
Back
Top Bottom