Nitakuwa wa mwisho kuamini kama matatizo ya Simba yanatokana na akina Try again.
Tatizo la Simba lipo kwa Mo mwenyewe, huyu boss swala la maarifa na busara za kiuongozi hana kabisa.
Kiuongozi anashindwa ku deal na changamoto za timu mpaka asikilize mashabiki wanataka nini. Mashabiki tunamtaka Chama kiongozi unafuata,
Mashabiki tunamtaka Luis kiongozi unafuata.
Mashabiki tunamtaka Barbra kiongozi huyo unafuata.
Jana alipotoa kauli kuwa atakuwa live Instagram kusikiliza maoni ya mashabiki kuhusu timu ya Simba ni mchezaji gani aachwe na mchezaji gani asajiliwe, ndipo nilipogundua mwenendo wa Simba unachangiwa na huyu mtu.
Kitu pekee cha kuweza kuinua Simba ni katiba mpya, kwa jinsi ilivyo hata huyo Barbra anayeletwa atafanya kazi kwa maslahi ya Mo. Hivyo inategemea na akili ya Mo je inawaza kupata faida kubwa kupitia timu au kuifanya timu ya Simba iwe kubwa Africa. Yule mkuu wa scouting si aliteuliwa na huyo huyo Mo lakini tunaona aina ya wachezaji wanaosajiliwa wakifanya vibaya lawama ni kwa Mangungu na try again utafikiri wao ndio wanaosajili. Hata kama tukisema kuna upigaji, hakuna mtu mwenye uchungu na pesa yake kama muhindi. Muhindi huwa ana mentality ya kupigwa hivyo kwenye swala la pesa ni lazima atafuatilia na ajue pesa yake imetumikaje. Muhindi anaweza kupa ela ukanunue kitu na lazima atataka uthibitisho wa bei uliyonunulia ikibaki hata mia tano tu haisamehewi. Muhindi yupo makini sana kwenye pesa haibiwi kizembe na huwa haamini mtu.
Simba itarudi kwenye ubora mpaka Mo mwenyewe aamue kuwa serious na Simba katika upande wa kuijenga na sio upande wa kuinyonya