Zaburi 113:7: Humwinua fukara kutoka mavumbini, humnyanyua maskini kutoka unyonge wake

Zaburi 113:7: Humwinua fukara kutoka mavumbini, humnyanyua maskini kutoka unyonge wake

Be specific unataka nini, mwambie

Isaya 43:26.
26. Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Lakini pia yeye ni Baba usisahau hili

Waebrania 11:6.
6. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Hayo yote nimeyafanya zaidi ya miaka 20 bado bilabila
 
Acha uvivu, Fanya kazi, Tumia pesa kwa nidhamu, Jifunze kuwekeza mkuu!!

Mafanikio ni kuunganisha Codes tu, hayahitaji power from Source fulani.

Acha kujifunika na kujitetea kwa poroja za dini, Huyo Mungu angekua ana nia ya kuwainua wote muwe Matajiri asingeuumba Umasikini.

Kwanini kaumba umasikini wakati anataka wote muwe matajiri?
 
Sijui moderator wanatumia Biblia gani? Yangu katika Zaburi 113:7 inasema "Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani." Sasa wao wameedit kutoka wapi?
 
Acha uvivu, Fanya kazi, Tumia pesa kwa nidhamu, Jifunze kuwekeza mkuu!!

Mafanikio ni kuunganisha Codes tu, hayahitaji power from Source fulani.

Acha kujifunika na kujitetea kwa poroja za dini, Huyo Mungu angekua ana nia ya kuwainua wote muwe Matajiri asingeuumba Umasikini.

Kwanini kaumba umasikini wakati anataka wote muwe matajiri?
Kwamba Mungu ameumba umasikini?
 
Ndiyo.

Infact kulingana na maelezo ya hicho kifungu, Mungu anayetajwa hapo ndiye kaumba umasikini.
Huu ni mtazamo wako na uelewa wako ni vizuri uheshimiwe..

lakini haimanishi upo sahihi

Mungu kila alichokifanya alilifanya katika ubora.. Tupo hapa tulipo kwasababu yetu wenyewe.

Bado akafanya njia ili tusiendelee kuwa katika hizo hali.

Kwa mara nyingine ni uamuzi wetu ndio utakao amua uwe mtu wa namna gani

Ukitaka uzima hauna budi kumkubali Yesu Kristo katika maisha yako, au kama ukiona ni porojo utapata ulichochagua
 
Back
Top Bottom