KERO Responded Zahanati ya Kimara iongezewe dawa muhimu, kuwaambia wagonjwa wakanunue dawa nje ya kituo sio sawa

KERO Responded Zahanati ya Kimara iongezewe dawa muhimu, kuwaambia wagonjwa wakanunue dawa nje ya kituo sio sawa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wiki iliyopita nilienda Zahanati ya Kimara Mwisho kwa ajili ya matibabu ya kijana wangu ambaye hakuwa sawa kiafya, baada ya kufika tulipokelewa na kufanyiwa vipimo vinavyohitajika.

Hata hivyo, baada ya majibu kutoka, tuliandikiwa dawa muhimu kwa ajili ya matibabu yake lakini nikaambiwa hazipatikani ndani ya zahanati, niliambiwa nikanunue dawa hizo katika duka la dawa lililopo nje ya kituo hicho.

Hali hii imenishangaza na kunisikitisha, kwani zahanati inapaswa kuwa na dawa za msingi ili kuwahudumia wananchi kikamilifu. Kulazimika kununua dawa nje kunaongeza gharama zisizotarajiwa kwa wazazi na walezi, hasa kwa wenye kipato cha chini.

Aidha, inaleta usumbufu na kuchelewesha upatikanaji wa matibabu kwa wakati, ni muhimu mamlaka husika zifuatilie suala hili kwa karibu na kuhakikisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya unaboreka.
1773297654724.png
Pia soma ~ Mwigulu: Fedha zinakuja lakini kila mgonjwa akienda hospitali anaambiwa akanunue dawa, pale hamna, TAKUKURU chunguzeni
 
Back
Top Bottom