Zahera: Hakuna mchezaji wa Yanga anaweza kucheza Pyramid FC. Tulisajili kwa ajili ya Ligi Kuu sio Klabu Bingwa Afrika

Zahera: Hakuna mchezaji wa Yanga anaweza kucheza Pyramid FC. Tulisajili kwa ajili ya Ligi Kuu sio Klabu Bingwa Afrika

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hawezi kuwasikiliza mashabiki wanachokisema kwa sasa baada ya kufungwa na Pyramids FC bali anawasiliana na uongozi ambao ulimpa mkataba.

Hayo yamekuja kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kutoa malalamiko yao wakimtaka Zahera kuondoka kutokana na matatizo wanayosema yamekithiri kwenye kikosi ikiwemo kushindwa kupanga vizuri kikosi cha kwanza pamoja na mbinu.

"Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga bali nilisaini mkataba na viongozi, kwahiyo siku viongozi wakinitaka kiwaachie timu nitafanya hivyo, sitokwenda mazoezini", amesema Zahera.

"Nina uzoefu mkubwa ila hapa Afrika, mashabiki wanakasirika. Hakuna mchezaji yoyote wa Yanga anayeweza kucheza Pyramids FC na lingine ni kwamba wakati tunasajili wachezaji, hatukusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika ila tulisajili kwa ajili ya ligi", ameongeza.

Aidha Zahera amesema kuwa mashabiki hawapaswi kumlaumu yeye kwa matokeo ya Klabu Bingwa kwani kikosi chake kiliandaliwa kwa ajili ya ligi kuu, ambako hawapo katika nafasi mbaya mpaka sasa, wakiwa wamecheza mechi chache.

Yanga inatarajia kusafiri hadi nchini Misri kuvaana na Pyramids katika mchezo wa marudio utakaopigwa wikiendi hii, ikiwa nyuma kwa kufungwa mabao 2-1.
 
Sasa yanga wasiende Misri maana hakuna wanachofuata zaidi ya kipige. Ila kasema ukweli ingawa ni mchungu
 
Kocha mkweli sana huyu. Msimu uliopita tuliona Timu inashindwa hata kulipa mishahara ya wachezaji, hadi kina Dante hadi leo wapo mtaani. Usajili ulifanyika kabla ya CAF haijatupatia nafasi 4 za ushiriki wa timu zetu. Yanga mkimtimua kocha Zahera laana yake itawaandama.
 
Mimi ni mmoja WA watu waliokuwa wakimuamini Sana zahera,lakini sasa nimeamini huyu kocha ni porojo mingi hii ni timu kubwa na hakikuandaliwa kwa ajili ya ushindi WA ligi ya ndani tu tunaitaji ushindi,asituone tunambabaikia ........
 
Mjinga tu,nilikuwa namuona wa maana kumbe anamambo ya kishamba sana,kuna chambo cha habari nimemsikia anaongea shit sana,siwezi muheshimu tena asepe tu
 
Kocha mkweli sana huyu. Msimu uliopita tuliona Timu inashindwa hata kulipa mishahara ya wachezaji, hadi kina Dante hadi leo wapo mtaani. Usajili ulifanyika kabla ya CAF haijatupatia nafasi 4 za ushiriki wa timu zetu. Yanga mkimtimua kocha Zahera laana yake itawaandama.
Tatizo sio kufuzu shida uwanjani yanga haileweki inacheza nini
Yanga hata kupiga pasi 4 hawawezi sasa utazema hii timu ina mwalimu
 
Kocha apewe mda!!!
Yaani tokea mechi za ndani,za kirafiki pia Yanga hawaonyeshi makali kabisa. Tatizo ni nini ? Pia huwa nina hasira jinsi alivyosababisha hadi Kakolanya akaondoka. Pia yule Matola mpaka leo huwa najiuliza kwa nini aliondoka.
 
Back
Top Bottom