Nazani kwasasa jamaa upande wa kuhakikisha kila mtanzania anamiliki smartphones kwa Bei rahisi unaupiga mwingi..
Baada ya kuona machawa wengi wa mjini wanamsifia ikabidi na mimi nizame china plaza kwenda kuchukua simu 2.
Movie inaanza kuna oppo A83 alikua anauza Bei cheap sana na Gb 128 (online ads) kufika dukani wazee Bei ni tofaut na ile ya online kwa vile nilikua nmeyavulia maji nguo ni lzm nioge nikachukua simu 2 A83 na Samsung note 10+
Kufika kwangu ikabidi nikae nikague bidhaa za Used Dubai kwanza ile oppo A83 nimekuta ni Gb 32 baada ya kuu connect na computer yangu Alf simu inapata moto kichizi na inaisha chaji haraka.
Kioo kuna muda kinagoma kutachi weeee ikabidi niende kweny note 10+ quality ya camera sio kma note 10+ ya wife simu inapata moto unaweza kupigia pasi nguo
Ikabidi nirud dukani kwao maana online wanasema warranty mwaka Ila dukani unapewa miezi 6 tuu nayo ishu za hardware hawahusiki
Kufika dukani ishu ya oppo nikawaambia wakasema betri lzm ninunue wanifungie Ila baada ya ya hapo warranty inakua imeisha na ishu ya capacity majibu yao mabovu balaa
Nikawapa shida ya note 10 camera quality waksema ningenunua mpya
Kwa kwl mpk kuandika unyama wote nimeshindwa na walivyowajanja wana maduka mawili duka moja kwa ajili ya kununua tuu ila duka jingine Ndio uko unakuta foleni ya kesi za simu