Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

SIJAONA BARABARA ZA KANDA YA ZIWA, YAANI HATA MOJA TU, BASI KAMA SIO MOJA HATA KILOMETA MOJA YA LAMI, DUH HATARI SANA.... HII NCHI NGUMU SANA HII.
 
Hoja yako hiyo (maandishi mekundu) ina mashiko, ila ni ndoto kudhani kuwa vyombo vyetu vya usalama vinaweza kufuatilia!! Tanzanite inapatikana tu Tz lakini wauzaji kwenye soko la dunia siyo Tz. Ukuta umejengwa lakini utoroshaji umerudi kwa mwendokasi.

Najiuliza Tanzania imeweka dhamana gani kwa Mkondarasi akubali kukopa pesa Benki kutujengea barabara? Je, kwa nini Serikali haikukopa fedha Benki za kumwezesha huyo Mkondarasi (kwa kuwa inaamini ana uwezo wa kujenga hizo barabara [emoji848]) kwa masharti yetu?

Ni Kiongozi mwenye agenda binafsi anaweza kukubali aina hiyo ya mkataba. AIBU

ANAUPIGA MWINGI - kazi iendelee
 
SIJAONA BARABARA ZA KANDA YA ZIWA, YAANI HATA MOJA TU, BASI KAMA SIO MOJA HATA KILOMETA MOJA YA LAMI, DUH HATARI SANA.... HII NCHI NGUMU SANA HII.
Huu sio mwisho wa Ujenzi,zinakuja zingine kibao tuu pengine na huko zitakuwwpo..

Pili hiyo inayoishia Simiyu ni Kanda gani?
Mwisho sio Kila Barabara lazima ijengwe Kwa satili hii ya EPC+F,hii ni maalumu Kwa Barabara za kufungua Uchumi tuu/Productive areas.
 
Barabara za kulipia Huwa ndio Zina element ya BOP na kiukweli ni chache sana Africa Kwa sababu inaleta ukakasi wa Kisiasa Kwa hapa Africa na Tanzania in particular
 
Nchi haiweki dhamana badala yake Contractor ndio anatakiwa kuweka dhamana ya pesa ndefu in form of bank guarantee Ili sisi tumbane Financier wake..

Kumbuka hii model mkandarasi ndio anabear takribani risks zote ambazo yeye ameziweka kwenye bei(offer price).

Mwisho uzuri contractors wengi ni Wachina na Taifa lao Lina uwezo Sasa Til.4 ni pesa ndogo sana kwao ndio maana umeona contractor wa 4 tuu kwenye miradi 7.
 
Hizo barabara zilikuwa hazina lami au wanaondoa ya mkoloni wanaweka ya mchina? Kama zilikuwa hazina tangia mkoloni basi tuna safari ndefu sana.
 
Hizo barabara zilikuwa hazina lami au wanaondoa ya mkoloni wanaweka ya mchina? Kama zilikuwa hazina tangia mkoloni basi tuna safari ndefu sana.
Ukiacha ya Igawa Tunduma zingine zote hazikuwa na lami,hata hiyo ya Igawa Tunduma ilikuwa single lane Sasa itakuwa Dual Carriage road ndio kusema inajengwa Barabara Mpya.
 

Kwenye mikataba ya ujenzi, ambapo mwenye mradi anamlipa "Contractor" fedha ya kutekeleza, anapaswa kuweka dhamana. Lakini aina hii ya mkataba ambapo "Contractor" anatumia fedha yake aweke dhamana ya nini?
 
Kwenye mikataba ya ujenzi, ambapo mwenye mradi anamlipa "Contractor" fedha ya kutekeleza, anapaswa kuweka dhamana. Lakini aina hii ya mkataba ambapo "Contractor" anatumia fedha yake aweke dhamana ya nini?
Akikiuka makubaliano unadhani itakuaje? Ni pesa yake lakini Serikali inamlipa hatua Kwa hatua so dhamana lazima
 
Nimependa plan ya hizo barabara , itafanya vaadi ya sehemu ziwe na njia fupi .
Byw kidatu ifakara tayari kunamalizika lami kwa nini mkataba wa barabara hii mpya uanzie tena kidatu?
 
Yule aliyewafanya wahandisi wote wa Tanroads kuhamia kwenye siasa za chama cha kijani
Nakupa mfano Mwingine unaoonesha kwamba gharama Huwa sio uniform kama unavyotaka kulazimisha..
Eg Mpanda-Tabora unit cost per km ni 1.4bln Kwa bei ya 2018 na hii kama.unaifahamu Ina mto 1 tuu na Barabara ni imenyooka Haina cuttings..

Nyingine hii ya Mpemba Hadi Isongole/Mpakani mwa Malawi yenyewe ni km 50 tuu unit cost ni zaidi ya bil.2.1 per km Kwa sababu ilikuwa na Madaraja mengi na milima ya kukata na kujaza vifusi vya kutosha..

Mwisho hoja ni kwamba still hiyo gharama ni nafuu sana maana unit cost yake per km ni 1.9bln.

Ukienda Barabara ya Makete Njombe ni zaidi ya Bil.2 per km nk nk.
 
Akikiuka makubaliano unadhani itakuaje? Ni pesa yake lakini Serikali inamlipa hatua Kwa hatua so dhamana lazima
Mkataba wa "Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC+F)" ni tofauti na mikataba migeni ya ushirikiano kati ya mwenye mradi na mwekezaji km "Public Private Partnership (PPP)" au "Build Operate and Transfer (BOT)" ambayo yote hiyo "Mwekezaji" anabeba "risks" zote na mwenye mradi anachohitajika ni kuwa na uhakika "Contractor" anao uwezo kifedha, utaalamu na anaaminika. Pia mwenye mradi anapaswa kuingia na mwekezaji mkataba utakaolinda uwekezaji.

Je, kwenye hii mikataba ya EPC+F, ya ujenzi wa barabara, mwekezaji/"Contractor" analindwa vipi? Itapendeza kuona moja ya mikataba hiyo.
 
Nimependa plan ya hizo barabara , itafanya vaadi ya sehemu ziwe na njia fupi .
Byw kidatu ifakara tayari kunamalizika lami kwa nini mkataba wa barabara hii mpya uanzie tena kidatu?
Pengine ni naming ya jina tuu au kutakuwa na Changamoto Kwa Barabara ya Sasa kiasi kwamba inatakiwa kufanyiwa rehabilitation (sijapita hii so hapa am just guessing) maana hata Igawa-Tunduama Kuna Barabara ya lami pia..

Mwisho itafupisha umbali na kufungua uchumi Mpya mathalani kutoka Songea Hadi Dar Magari Yote Sasa yatapitia Ifakara na Moro umbali utakuwa sawa na Dar -Mbeya km 800 plus kutoka zaidi ya km 1000 za Sasa..

Aidha umbali wa Tanga Hadi Mwanza au Mikoa yote ya Lake Zone au Nchi za Magharibi itakuwa mfupi chini ya km 800,hakuna route ya Bus ,Tanga-Mwanza Sasa itakuwepo.

Ila Kizuri zaidi Sasa Bandari ya Tanga itaanza kuwa Busy maana kutoka Tanga kwenda huko Kanda ya Ziwa ni pafupi kuliko kutoka Dar,just imagine Km 1300 vs km 800
 
Sawa ila sidhani kama Serikali inaweza kiuka makubaliano ya kimkataba maana hata Kwa mikataba ya Sasa kwani contractor Huwa analindwaje? Mbona sijawahi ona sehemu ambayo contractor analindwa per say? Sana sana ni kwamba Kuna riba ya kuchelewesha mkataba na Serikali ndio inalindwa dhidi ya Mkandarasi kuingia mitini.

Mwisho sio lazima kuona mkataba ingia tovuti ya idara ya Manunuzi au ingia shule mwenyewe Kwa ku google Kila kitu utaona kinavyofanyika..
 
Bandari ya Tanga inakwamishwa na kina . Meli za Roro hazitii nanga pale.
 
Hili ni jukwaa la kuelimishana na kwa kuwa wewe ndiye uliyeleta uzi na unatetea aina hiyo ya mkataba wa ujenzi, tujuze zaidi. Ukifanya hivyo utakuwa unaondoa maswali kuhusu uhalali wake, kama ilivyo kwa mkataba wa Bandari
 
Bandari ya Tanga inakwamishwa na kina . Meli za Roro hazitii nanga pale.
Hata zingekuwa zinatia Nanga ,Barabara gani ingetumika kufika Mwanza? Ya kupitia Arusha Hadi Singida? Nani afanye huo mzunguko?

Hope Serikali itapanua zaidi hiyo Bandari na hivyo kuiwezesha kupata Huduma ya Meli kubwa .
 
Achana nae mkuu, amezoea zile kiki za kijima
 
Ukiacha ya Igawa Tunduma zingine zote hazikuwa na lami,hata hiyo ya Igawa Tunduma ilikuwa single lane Sasa itakuwa Dual Carriage road ndio kusema inajengwa Barabara Mpya.

Kama ni hivyo Mama apewe Maua yake maana tuliaminishwa NZIRANKENDE JIKONO JANDAMA alijenga mtandao mkubwa sana wa Lami mpaka akawa anazindua tena barabara zilizojengwa na JAHCARHIRE KEYQWERTY.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…