Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Huwezi jua shida unashinda kwenye umbea mda mwingi..

EPC+F maana yake Engineering (detailed design),Procurement, Construction and Financing..

Kiufupi Serikali inaalika mkandarasi anaeweza kufanya hizo kazi na aoneshe financing model kabisa harafu wnakubaliana gharama Kwa mda mrefu yaani concessional agreement,risks zote atabeba contractors hivyo itamlazimu kuwa makini na kujenga Kwa Ubora na atakuwa analiowa mdogo mdogo ndani ya mda wa consessional agreements inaweza fika miaka 30 na mda wote huo ni wajibu wa contractor ku maintain Barabara kabl ya kuja kukabidhi.
Hapa ndio nimekuelewa na hio model Watanzania hatuiwezi
 
Hapa ndio nimekuelewa na hio model Watanzania hatuiwezi
Kwa nini msiiweze? Kwa mama ya kukosa mtaji na Utaalamu sawa.

Hii model ni relatively expensive kulinganisha na traditional model ila ni efficient sana Kwa maana mkandarasi atajenga Kwa haraka na Kwa Ubora Kwa sababu Barabara ikizingua kabla ya mda ni zigo lake so binafsi naopenda hii..

Kwa sababu Barabara zikiwahi Kukamilika mapema inaanza kuzalisha immediately na Serikali inapata uwezo zaidi wa kulipa obligation zake..

Ule utaratibu wa zamani Barabara ya km 100 unaweza maliza miaka 10 unaijenga tuu huku hasara za riba ya kuchelewa ikiwa kubwa..
 
Ahadi hewa watu wamesaini mikataba [emoji38][emoji38] we Jamaa Bure kabisa..

Kwanza tangu lini Samia amewahi kukupa ahadi hewa? Kwanza sio Barabara tuu Bali Hadi kwenye Afya amefanya mapinduzi, kwenye Elimu ndio kabisa Watoto wooote wanapata mkopo na Sasa kawaongeza wa diploma,Ajira ndio usiseme..

Samia ni kichwa kingine,anataka awasaidie huko kwenye bandari Wajamaa mbakaza Kwa kung'ang'ania umaskini na ujinga [emoji16][emoji16][emoji16]
Hizo trilioni 3 zipo kwenye bajeti ipi? Hyo barabara ya Igawa, mbeya, vwawa mpaka tunduma ilihaidiwa na serikali toka 2012. Leo hii ni miaka 10 zinazungumzwa siasa....
 
Hizo trilioni 3 zipo kwenye bajeti ipi? Hyo barabara ya Igawa, mbeya, vwawa mpaka tunduma ilihaidiwa na serikali toka 2012. Leo hii ni miaka 10 zinazungumzwa siasa....
Aliyekwambia zinalipwa mara Moja nani? Umewahi ona Barabara imekamilika Kwa mwaka mmja?
 
Hii modal hata marehemu asingeiweza tungekula kula mawe miaka 50 . Huyu mama ana akili sana kwa sababu anasikia ushauri wa wataalamu wake.
Yule alikuwa mjamaa anaogopa gharama harafu anasahau kwamba kuchelewa ni more costful kuliko kulipa gharama kubwa kidogo ila ukaleta Mageuzi makubwa na ya haraka kwenye uchumi..

Barabara ambazo zingekamilika Kwa miaka 20 zinaenda Kukamilika ndani ya miaka 4 zinaanza uzalishaji huku Serikali ikitumika pesa ilizozalosha kulipia Madeni mdogo mdogo bila ku stress Uchumi.
 
Kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru Tanzania imepata Rais Samia apewe maua yake.

Serikali ya Rais Samia imeandika Historia nyingine ya ubunifu kwa kusaini kuanza ujenzi wa barabara za kuu za lami kwenye mikoa 13 kwa pamoja zenye jumla ya urefu wa KM 2035 kwa mtindo wa EPC+ F (Engineering, Procurement, Construction and Finance) kwa gharama ya Tsh.Tilioni 3.8 ambapo miradi inatarajiwa Kukamilika ndani ya miaka 4 (2023-2027).


Akizungumza wakati wa kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa amesema kwamba, barabara hizo hazitokuwa za kulipia tozo kama wapotoshaji wanavyosema. Ikumbukwe hii haijawahi tokea toka Uhuru, walinda legacy mnafundishwa kazi.

My Take
Samia anawaonesha kwamba Private Sector inalipa kuliko Ujamaa mbuzi ambao baadhi ya watu wasiojielewa wanakumbatia.

Ndio maana hata kwenye Bandari anataka awafundishe namna ya kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu badala ya kuhubiri propaganda za Uzalendo mbuzi na umaskini over years.

Hongera sana Mh. Rais, na Waziri wa Mbarawa Kwa Ubunifu,Historia itaandika jina lako kwa wino Mwekundu.

=====

MIRADI YA BARABARA ILIYOSAINIWA KWA UTARATIBU WA EPC + F

i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;

ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa;

iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki;

iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma;

v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale;

vi) Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa; na

vii) Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa na inapita katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga.

UPIGAJI NDIO HUU SASA:

Gharama ya miradi yote 3.8 Trilion kwa ujenzi wa kms 2035.

Swali: Kilometa moja inajengwa kwa Tsh ngapi?

Chukua 3,800,000,000,000/ 2035 upate bei ya kujenga km moja.

Kwanini bei ya km moja ni kubwa kiasi hicho?
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.

Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.

Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.

Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.

Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.

Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.

Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.

Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.

Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?

Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?

Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.

Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.
 
UPIGAJI NDIO HUU SASA:

Gharama ya miradi yote 3.8 Trilion kwa ujenzi wa kms 2035.

Swali: Kilometa moja inajengwa kwa Tsh ngapi?

Chukua 3,800,000,000,000/ 2035 upate bei ya kujenga km moja.

Kwanini bei ya km moja ni kubwa kiasi hicho?
Kwa nini usifanye hesabu unanipa assignment Mimi? Mimi tayari najua gharama,wewe ndio eleza upigaji ni kiasi gani.
 
Kwa nini usifanye hesabu unanipa assignment Mimi? Mimi tayari najua gharama,wewe ndio eleza upigaji ni kiasi gani.
Waziri ni msomi na ni Professor, nilitarajia akupatie jibu ulilouliza ila nimeandika kukuamsha kuwa kuna upigaji mkuu
 
Waziri ni msomi na ni Professor, nilitarajia akupatie jibu ulilouliza ila nimeandika kukuamsha kuwa kuna upigaji mkuu
Mimi ninajua nataka wewe hapo unieleze Ufisadi uko wapi Ili tufanye wote analysis,si umejenga hoja wewe au?
 
Back
Top Bottom