Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ile ya Morogoro Songea nayo ipo?
Chinese again
Hapa ndio nimekuelewa na hio model Watanzania hatuiweziHuwezi jua shida unashinda kwenye umbea mda mwingi..
EPC+F maana yake Engineering (detailed design),Procurement, Construction and Financing..
Kiufupi Serikali inaalika mkandarasi anaeweza kufanya hizo kazi na aoneshe financing model kabisa harafu wnakubaliana gharama Kwa mda mrefu yaani concessional agreement,risks zote atabeba contractors hivyo itamlazimu kuwa makini na kujenga Kwa Ubora na atakuwa analiowa mdogo mdogo ndani ya mda wa consessional agreements inaweza fika miaka 30 na mda wote huo ni wajibu wa contractor ku maintain Barabara kabl ya kuja kukabidhi.
Kwa nini msiiweze? Kwa mama ya kukosa mtaji na Utaalamu sawa.Hapa ndio nimekuelewa na hio model Watanzania hatuiwezi
Mpaka hapa ninapotype nipo Green wala sihami ng'o maana ndiko kuliko tamalaq demokrasia ya kweli!Kipindi Cha Jiwe ,wewe si ulikuwa huko Kijani?
Soma kwanza mradi unatumia modal gani ya utekelezajiMakampuni yote ni ya China.
Ina maana hakuna local engineering company ya kuweza kujenga barabara?
Huu ni uhuni na uhaini kabisa.
Ukonga mnazalisha nini?Hizo barabara na jimbo la Ukonga imo?
Hii modal hata marehemu asingeiweza tungekula kula mawe miaka 50 . Huyu mama ana akili sana kwa sababu anasikia ushauri wa wataalamu wake.Hapa ndio nimekuelewa na hio model Watanzania hatuiwezi
Hizo trilioni 3 zipo kwenye bajeti ipi? Hyo barabara ya Igawa, mbeya, vwawa mpaka tunduma ilihaidiwa na serikali toka 2012. Leo hii ni miaka 10 zinazungumzwa siasa....Ahadi hewa watu wamesaini mikataba [emoji38][emoji38] we Jamaa Bure kabisa..
Kwanza tangu lini Samia amewahi kukupa ahadi hewa? Kwanza sio Barabara tuu Bali Hadi kwenye Afya amefanya mapinduzi, kwenye Elimu ndio kabisa Watoto wooote wanapata mkopo na Sasa kawaongeza wa diploma,Ajira ndio usiseme..
Samia ni kichwa kingine,anataka awasaidie huko kwenye bandari Wajamaa mbakaza Kwa kung'ang'ania umaskini na ujinga [emoji16][emoji16][emoji16]
Aliyekwambia zinalipwa mara Moja nani? Umewahi ona Barabara imekamilika Kwa mwaka mmja?Hizo trilioni 3 zipo kwenye bajeti ipi? Hyo barabara ya Igawa, mbeya, vwawa mpaka tunduma ilihaidiwa na serikali toka 2012. Leo hii ni miaka 10 zinazungumzwa siasa....
Yule alikuwa mjamaa anaogopa gharama harafu anasahau kwamba kuchelewa ni more costful kuliko kulipa gharama kubwa kidogo ila ukaleta Mageuzi makubwa na ya haraka kwenye uchumi..Hii modal hata marehemu asingeiweza tungekula kula mawe miaka 50 . Huyu mama ana akili sana kwa sababu anasikia ushauri wa wataalamu wake.
Umemjibu vizuri,sio Kila Barabara inaweza jengwa Kwa staili hii,only productive areas Ili kufungua uchumiUkonga mnazalisha nini?
Kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru Tanzania imepata Rais Samia apewe maua yake.
Serikali ya Rais Samia imeandika Historia nyingine ya ubunifu kwa kusaini kuanza ujenzi wa barabara za kuu za lami kwenye mikoa 13 kwa pamoja zenye jumla ya urefu wa KM 2035 kwa mtindo wa EPC+ F (Engineering, Procurement, Construction and Finance) kwa gharama ya Tsh.Tilioni 3.8 ambapo miradi inatarajiwa Kukamilika ndani ya miaka 4 (2023-2027).
Akizungumza wakati wa kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa amesema kwamba, barabara hizo hazitokuwa za kulipia tozo kama wapotoshaji wanavyosema. Ikumbukwe hii haijawahi tokea toka Uhuru, walinda legacy mnafundishwa kazi.
My Take
Samia anawaonesha kwamba Private Sector inalipa kuliko Ujamaa mbuzi ambao baadhi ya watu wasiojielewa wanakumbatia.
Ndio maana hata kwenye Bandari anataka awafundishe namna ya kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu badala ya kuhubiri propaganda za Uzalendo mbuzi na umaskini over years.
Hongera sana Mh. Rais, na Waziri wa Mbarawa Kwa Ubunifu,Historia itaandika jina lako kwa wino Mwekundu.
=====
MIRADI YA BARABARA ILIYOSAINIWA KWA UTARATIBU WA EPC + F
i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;
ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa;
iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki;
iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma;
v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale;
vi) Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa; na
vii) Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa na inapita katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga.
UjingaTunafidia bandari
Kwa nini usifanye hesabu unanipa assignment Mimi? Mimi tayari najua gharama,wewe ndio eleza upigaji ni kiasi gani.UPIGAJI NDIO HUU SASA:
Gharama ya miradi yote 3.8 Trilion kwa ujenzi wa kms 2035.
Swali: Kilometa moja inajengwa kwa Tsh ngapi?
Chukua 3,800,000,000,000/ 2035 upate bei ya kujenga km moja.
Kwanini bei ya km moja ni kubwa kiasi hicho?
Waziri ni msomi na ni Professor, nilitarajia akupatie jibu ulilouliza ila nimeandika kukuamsha kuwa kuna upigaji mkuuKwa nini usifanye hesabu unanipa assignment Mimi? Mimi tayari najua gharama,wewe ndio eleza upigaji ni kiasi gani.
Mimi ninajua nataka wewe hapo unieleze Ufisadi uko wapi Ili tufanye wote analysis,si umejenga hoja wewe au?Waziri ni msomi na ni Professor, nilitarajia akupatie jibu ulilouliza ila nimeandika kukuamsha kuwa kuna upigaji mkuu