Zaidi ya Magaidi 600 wa Hezbollah waangamizwa na Israel huko Lebanon-Kusini!!!

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
9,662
Reaction score
8,023
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Jumatatu kuwa Israel itaongeza nguvu ya mashambulizi yake nchini Lebanon ili “kuisambaratisha” Hezbollah.

Katika ujumbe wa video uliorekodiwa, Netanyahu amesema kuwa Israel ipo vitani dhidi ya Hezbollah na kwamba katika wiki za hivi karibuni jeshi la Israel limewaua zaidi ya wapiganaji 600 wa kundi hilo nchini Lebanon.

Netanyahu ameongeza kuwa tayari ameagiza “kukanyaga mafuta zaidi,” akimaanisha kuongeza kasi ya mashambulizi, huku akisisitiza kuwa Israel “itaisambaratisha” Hezbollah.

Pia amesema kuwa kuna timu maalum inayoshughulikia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) zinazotumia mfumo wa fiber optic zinazotumiwa na Hezbollah.

Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema katika taarifa kwamba limeanza kushambulia miundombinu ya Hezbollah katika Bonde la Beqaa mashariki mwa Lebanon pamoja na maeneo mengine mbalimbali nchini humo.

Soma Pia: Magaidi 6 wa Hezbollah waangamizwa huko Al-Bureij Lebanon!!

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Lebanon yalianza kutekelezwa mwezi Aprili. Hata hivyo, licha ya makubaliano hayo, Israel imeendelea kufanya mashambulizi karibu kila siku nchini Lebanon, huku Hezbollah nayo ikiendelea kushambulia nafasi za kijeshi za Israel.

View: https://www.instagram.com/reel/DZLBV67ASTQ/?igsh=MW9uZDBsYWR2YnZscg==
 
Back
Top Bottom