KANDA MBILI
Member
- Jul 9, 2012
- 60
- 57
Historia ya Cde Bakari inaendelea kumtafuna kwa alikotoka na ambako yupo. Alipokuwa kwenye sekretarieti kama katibu wa vijana Simanjiro alikuwa kikwazo sasa kwa wilaya ya Missenyi ndio kawa kikwazo kabisa kama bosi wa chama. Ndugu Katibu Mkuu najua utakuja Missenyi ila naomba kabla hujafika nikuelezee mambo machache kuhusu katibu wetu wa Missenyi.
Ndugu Bakari akiwa katibu wa UVCCM Simanjiro aliwahi kushiriki kula hela za vikundi za vijana nikimaanisha Saccos na kupelekea vijana kutoelewana. Mbali na hilo huyu ndugu Bakari akiwa ni mmojawapo wa usimamizi wa uchaguzi kata ya Endiamtu alisababisha kuleta mvurugano kutokana na kushiriki kupitisha majina ya watu wasiyokubalika kwenye kata hiyo na kuja na majina ya watu mfukoni. Hii inaonyesha moja kwa moja kwamba ni mtu mwenye ghiriba na mbadhilifu wa mali za umma na mpokea rushwa.
Tuachane na ya Simanjiro tuje kwenye wilaya yetu ya Missenyi. Kitendo cha kuletwa huku na kuwa katibu wa Chama kuna mambo ambayo ameyafanya yanatia doa chama cha mapinduzi lakini mbali na hayo yanatia doa serikali yetu chini ya Amiri jeshi Mkuu Mh Samia Suluhu Hassan. Kabla ya yote ameleta mparanganyiko ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Anajua kila kitu na ana dharau, kebehi kwa wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi. Tunajua hiki chama tangu enzi na enzi ni chama cha kijamaa ambacho kinatusisitiza tupendane na kuheshimiana.
Ubadhirifu wa pesa kwenye ofisi, Ndugu Bakari amekuwa mlafi kupitiliza, Kuna asilimia ambazo huwa zinarudi kwa ajili ya kuwapa motisha ambazo ni posho za mabalozi , makatibu tawi na makatibu kata. Kwa Bakari hicho kitu hakifanyi hadi sasa ameweza kula hela zaidi ya 12,000,000/=tshs (milioni 12). Anafanya ujanja wa zamani wakati dunia iko wazi. Yeye anachokifanya anamaliza miezi hata minne bila kuwapatia posho zao halafu baada ya hapo ndio anawapa ya mwezi mmoja. Hii imesababisha mabalozi kukata tamaa na kingine kufanya makatibu tawi na kata kukatishwa tamaa ya kukitumikia Chama chao kutokana na ubadhilifu na ubabe wa ndugu Bakari.
Kula michango ya wadau, kuna ujenzi unaendelea wa nyumba za watumishi na majengo ya chama ,Bakari amekuwa akitumia mwanya huo hela hizo kuzitafuna ambapo amepelekea ujenzi kuweza kukwama. Hii inawakatisha tamaa wadau wanaokipenda chama kusitisha michango yao kwakuwa hawaoni hatua yeyote inayoendelea ya ujenzi. Kuna kundi litajitokeza kumtetea lakini haya mambo yapo naamini mtafanya upembuzi yakinifu kujua ukweli.
Kuleta mfarakano kwenye ofisi, Ndugu Bakari ameonyesha madhaifu makubwa ndani ya ofisi ya CCM ya Missenyi. Leo hii ofisi ya CCM ya Missenyi hakuna mawasiliano mazuri baina ya watumishi. wenyewe hawaelewani. Kiukweli ndugu Bakari ndio kikwazo na inasababisha watu wasitimize wajibu wao kutokana na aina ya uongozi wake. Hii inapelekea kasi ya uchapakazi kuwa ndogo.
Penzi kitovu cha uzembe, Ndugu Bakari amelevywa na mapenzi. Tunajua katibu wa UWT ni mke wa mtu. Ila kitendo cha Bakari kuwa na mahusiano na katibu wa UWT imekuwa shida sana kwa Missenyi. Leo hii mgeni akija atashindwa kuelewa katibu wa UWT ni nani na Katibu wa Chama ni yupi. Baada ya penzi kukolea huyu katibu wa UWT amekua akifanya maamuzi mengi kwa watumishi wengine. Hii imepelekea watumishi wengine kukatishwa tamaa na kuingiliwa kwenye majukumu yao ya kazi.
Ndugu viongozi wa ngazi ya juu ya chama, tunaomba mtusaidie huyu mtu kumrekebisha na kumpa onyo maana naona hata mkoani huu umekuwa mfupa mgumu. Tunampenda lakini hofu yetu kubwa tunaenda kwenye kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji na baada ya hapo tunaelekea 2025 kwenye uchaguzi mkuu. Kwa uongozi wake na taratibu zake inaweza kupelekea chama chetu kisifanye vizuri maana hakuna maelewano mazuri baina ya watumishi kwa watumishi na watumishi kwa wanachama. Tunaimani nguvu ni umoja na hili jambo mtalifanyia ufumbuzi.
Kuhusu huo ubadhilifu ushahidi upo na mengine nimeamua kukomea hapo.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Ni mimi Kanda Mbili mfia chama wa CCM