Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme wa Stiegler's gorge

Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme wa Stiegler's gorge

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Serikali ya Tanzania inajiandaa kukata miti eneo la ukubwa wa asilimia tatu ya hifadhi ya taifa Selous.

Mapema asubuhi ya Jumatano, serikali ilipokea maombi ya zabuni ya kukata miti hiyo kutoka kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi yaliyoonyesha nia ya kutekeleza mradi huo wa kukata miti.

Serikali inasema ukataji huu wa miti zaidi ya milioni 2 ni maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la kuzalisha umeme wa megawati 2,100 utakaojengwa ndani ya hifadhi hiyo.

Hatua hii inaongeza ukosoaji dhidi ya serikali kutoka kwa wanaharakati wa mazingira ambao tangu serikali kutangaza nia ya kujenga mradi huo wa umeme, wamekuwa wakipinga mradi huo kuwa ni hatari kwa wanyama pori na viumbe wengine waishio katika hifadhi hiyo ya Selous, ambayo inatambuliwa pia kama urithi wa dunia.

Wanamazingira wakosoa

Ni wazi kwamba serikali ya Tanzania imedhamiria kuendelea na mradi huu wa kufua umeme, huku kukiwa na ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa mazingira, ambao wanaelezea wasiwasi wao kuhusiana na athari za hali ya mfumo wa kiikolojia ndani ya hifadhi ya Selous.

Hata hivyo hivi karibuni kuhusu mradi huo Rais John Magufuli aliweka wazi kwamba, serikali yake haitakwamishwa na ukosoaji wa aina yoyote ya kimazingira katika kutekeleza mradi huu mkubwa wa umeme.

Rais alisistiza kuwa wakati serikali yake inatekeleza sera ya viwanda,mradi huu wa umeme ni muhimu zaidi kufikia malengo hayo.

Mtendaji mkuu wa wakala wa misitu Tanzania Profesa Dosantos Silayo ameiambia BBC sababu za kuuzwa kwa miti itakayokatwa kwenye hifadhi hiyo kupisha mradi huo.

''Sasa serikali imeona si vizuri kuiondoa miti katika hali ya kuiharibu inaweza kuwa na thamani, serikali imeamua kuitoa kwa utaratibu ambao utaiwezesha iuzwe kwenye makampuni mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya kutengeneza samani ndani na nje ya nchi, hii si biashara, na kwa kweli haijawa nia ya serikali kufanya uharibifu kwenye hifadhi zake''.

Hata hivyo Mwanasheria wa mazingira Dokta Rugemeleza Nshala amezungumzia ni hatua gani za muhimu kuzingatiwa katika utekelezwaji wa mradi huo.

''Ni kitu ambacho kinapaswa kitekelezwe kwa umakini mkubwa kwa sababu eneo la hifadhi na bado lile eneo wanalotaka kukata miti bado halijatolewa kutoka eneo la hifadhi na ni eneo ambalo ni la urithi la dunia.Umeme unahitajika na mazingira yanahitajika.mazingira yakiharibika hasara ni kubwa zaidi''.

Kwa sasa Tanzania inayokadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 50,inazalisha kiasi cha megawati 1,400 tu za umeme kiwango ambacho hakikidhi mahitaji ya nishati ya umeme ya nchi.

Mradi huu mkubwa wa umeme unatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati zaidi ya 2000 za umeme ili kuimarisha mahitaji halisi ya umeme.

=====

Tathimini ya mradi huu ambao hata wabunge waliomba iliwahi kutolewa kwa umma?

Bahati mbaya sana Tanzania ya leo kuona mbali ni negativity na kuona karibu ni positivity.

Wacha tusubiri ya huko mbeleni.
 
Tathimini ya mradi huu ambao hata wabunge waliomba iliwahi kutolewa kwa umma?

Bahati mbaya sana Tanzania ya leo kuona mbali ni negativity na kuona karibu ni positivity.

Wachs tusubiri ya huko mbeleni.

huu ujinga wa magharibi ndio kwanza unausikia?

EIA ya mradi huo ipo na ndio inaongoza mradi mzima huo.

Kila kitu kinachofanywa nchini chenye lengo la kuboresha maisha ya Watanzania wewe upo kinyume chake. Aibu itakupata a good always over evil
 
Huu ujinga wa magharibi ndio kwanza unausikia?
EIA ya mradi huo ipo na ndio inaongoza mradi mzima huo.
Wewe na hao mabwana wako mtaendelea kupiga kelele. Ulivyo mshenzi Kila Kila kitu kinachofanywa nchini chenye lengo la kuboresha maisha ya Watanzania wewe upo kinyume chake. Aibu itakupata a good always over evil

Tathimini ya huo mradi umeiona?
 
Nikikumbuka jinsi alivyozindua kwa mbwembwe mradi wa barabara za juu pale Ubungo (Ubungo Inter-change); Sidhani kama mtasikia tena mtu akizungumzia huo mradi - WHITE ELEPHANT PROJECTS
 
Natumikia nchi yangu si wewe kibaraka cha walanguzi wa miradi ya Umeme nchini. Viwanda vinahitajika na Umeme wa kutosha unahitajika pia
Mnafiki tu wewe!Hio EIA wabunge walipewa?Uzalendo si kuwa na mahaba na watawala au kujipendekeza.

Wazalendo ni wale waliohoji wapewe EIA kwa nia njema then ndio waunge mkono.

Watu walipokuwa wanahoji ya Gesi ya Mtwara waliionekane sio wazalendo.Leo hii hiyo gesi inatumika kwa kiwango gani?

Uchumi wa gesi mliokuwa mnaimba uko wapi?

Nini ilikuwa logic ya kupitisha ile sheria kwa hati ya dharura?

Mkopo tulioingia kwa ajili ya hiyo gesi ya Mtwara nani analipa kama sio sisi?
 
Sidhani kama tuna uwezo wa kutekeleza huu mradi in ten yrs to come! We dont have smart leaders to implement it. Sorry!
Mradi utaanza julai 2018 baada ya miezi 32 utakuwa umekamilika. Pesa zipo. Wafanyakazi hawakuongezwa mishahara ili Pesa itumike kujenga miradi hii. Omba Mungu atupe uhai kushuhudia hatua hii ya maendeleo.
 
Ningependa kuiona hiyo tathimini ya EIA
 
Mnafiki tu wewe!Hio EIA wabunge walipewa?Uzalendo si kuwa na mahaba na watawala au kujipendekeza.

Wazalendo ni wale waliohoji wapewe EIA kwa nia njema then ndio waunge mkono.

Watu walipokuwa wanahoji ya Gesi ya Mtwara waliionekane sio wazalendo.Leo hii hiyo gesi inatumika kwa kiwango gani?

Uchumi wa gesi mliokuwa mnaimba uko wapi?

Nini ilikuwa logic ya kupitisha ile sheria kwa hati ya dharura?

Mkopo tulioingia kwa ajili ya hiyo gesi ya Mtwara nani analipa kama sio sisi?
Hakuna mbunge ambaye hana uwezo wa kuiona hiyo EIA akijitokeza huyo ni mbunge mpumbavu wa kiwango cha kimataifa.
Kwa sasa hakuna mgao ni kwa sababu ya gesi najua unaijua hilo
 
Ingawa mimi ni mbumbumbu ila ninachojua kidogo ni kuwa hata MAKAZI ya muanzisha bandiko yalikuwa MSITU miaka fulani nyuma.....

Wale mnaowaiga pia wamejenga mpaka kwenye kingo za mito isipokuwa tu wamejengea kingo imara mito yao.
 
Hata mradi wa mabasi yaendayo kasi kujengwa Jangwani kwa style ile ulikuwa ni umakini na uzalendo wa viongozi wa CCM.

Mradi uko salama kwasababu ushauri wa kitaalamu ndio ulizungatiwa na sio wa wanasiasa.

Hongereni sana mnajenga nchi!
 
Huu ujinga wa magharibi ndio kwanza unausikia?
EIA ya mradi huo ipo na ndio inaongoza mradi mzima huo.
Wewe na hao mabwana wako mtaendelea kupiga kelele. Ulivyo mshenzi Kila Kila kitu kinachofanywa nchini chenye lengo la kuboresha maisha ya Watanzania wewe upo kinyume chake. Aibu itakupata a good always over evil

1/ Tafadhali weka hapa EIA ya huo mradi.

2/ Huhitaji "ujinga wa magharibi" kufikiri and nobody does. Kama mradi una athari kwa mazingira, itabaki kuwa hivyo hata kama watu wote watakaa kimya. Na kusema kwamba mradi unaharibu mazingira na maisha ya watu (think about what will happen downstream), si kukataa "kinachofanywa nchini chenye lengo la kuboresha maisha ya Watanzania". Actually, unaboreshaje maisha ya Watanzania kwa kupuuza athari hasi za mradi? Unafikiri kati ya anaye-pretend kuwa mradi hauna athari hasi wakati una athari hasi na anayesema mradi una athari hasi wakati una athari hasi, ni nani anayeboresha maisha ya Watanzania?

3/ Huu si mradi wa kwanza (dam) kutekelezwa duniani. Mengi yameandikwa kuhusu damming. Miongoni mwa mambo yaliyopata kuleta fedheha kubwa kwa taasisi kama World Bank ni damming na huwezi kuwakuta wakitoa mkopo tena kwa miradi ya namna hiyo, japo wanaimezea mate kwa kuwa biashara yao ni kuuza mikopo. Soma. Read a bit ili uboreshe hoja zako. Si lazima kwamba ukisoma kidogo what is known about damming, basi utapinga mradi wa Stiegler's Gorge. La hasha, utaboresha hoja zako na kuondoa hisia kwamba uko "programmed". Kwa kuanzia, tafuta andiko la Angazi and Ndulu from the 1970s kuhusu athari za huu mradi downstream (these are agricutural economists). Pia tafuta kitabu cha Kjell Havnevik on the same case. Then, continue debating.
 
Mradi utaanza julai 2018 baada ya miezi 32 utakuwa umekamilika. Pesa zipo. Wafanyakazi hawakuongezwa mishahara ili Pesa itumike kujenga miradi hii. Omba Mungu atupe uhai kushuhudia hatua hii ya maendeleo.

Nani anajenga huu mradi? I mean contractor ni nani? Kama watz je, wana capacity (technical know how); Mimi sina imani kama utafanikiwa. Je, unafahamu yanayoendelea kwenye mradi wa barabara za ju Ubungo??
 
Kwa akili yako huu ujinga wa magharibi ndio kwanza unausikia?
EIA ya mradi huo ipo na ndio inaongoza mradi mzima huo.
Wewe na hao mabwana wako mtaendelea kupiga kelele. Ulivyo mshenzi Kila Kila kitu kinachofanywa nchini chenye lengo la kuboresha maisha ya Watanzania wewe upo kinyume chake. Aibu itakupata a good always over evil

watu kama wewe sometimes mnasikitisha......kwa sababu mnaangalia mambo kwa negativity tuu.... wakati wa kujenga mwendo kasi wapo waliohoji kuhusu kuweka ule mradi pale jangwani kwa sababu ni sehemu inayofahamika kwa miaka mingi kwamba ina experience mafuriko kwa sababu ya mto msimbazi. Lakini baadhi ya waliohoji waliimbiwa wanapinga maendeleo na wengi kuitwa CHADEMA! Hata tukaonyeshwa certificates za EIA. Haya leo tuko wapi? mvua ikinyesha usafiri wa DART unakuwa takataka! mabasi hayaendi Lakini yote haya ni maamuzi yasiyoangalia mipango na maslahi ya wengi baadaye.... ile ni hasara ya kitaifa. Si ya CCM wala CHADEMA wala CUF! Wote inatuumiza kama waTanzania. Sasa wapo leo wanaohoji huo mradi wa umeme kwenye hilo bonde la Stigler's Gorge. Hakuna anayefanya hivyo kwa sababu ana chuki au hapendi umeme! No, wengi wanauliza kwa sababu tunatamani maendeleo yetu leo yaende sambamba na utunzaji wa raslimali zetu kwa ajili ya Tanzania ya miaka ya baadaye. Unfortunately wapo kama wewe mleta mada unadhani unaipenda Tanzania kuliko wengine. Tanzania is our home. Jua liwake, mvua inyeshe....wote tuko hapa. Kwenye mambo ya kitaifa tuwe na mijadala mipana kwa sababu after all tunajenga nchi moja na hakuna mwenye monopoly ya akili au uelewa kama CCM mnavyotuaminisha.
 
Hii BBC ni ya kupigwa marufuku hapa nchini kwani wanadharau sana inamaana watanzania hawana akili za kutofautisha faida na hasara kwa miradi ya maendeleo hapa nchini? wao ndio wana akili sana eeeh. Watukome kabisa watuachie maisha yetu .
 
Natumikia nchi yangu si wewe kibaraka cha walanguzi wa miradi ya Umeme nchini. Viwanda vinahitajika na Umeme wa kutosha unahitajika pia

Tuliambiwa umeme wa gas utakuwa muarubaini wa nishati hapa nchini, tena tutauza mpaka nje. Sasa leo kuambiwa tunaenda kwenye wa maji watu wasihoji? Mnakuwa waongo kwa ajili ya maslahi yenu kisha mkibanwa mnaanza kuleta maelezo ya kizembe
 
Back
Top Bottom