Zaidi ya miti milioni 226 imepandwa Tanzania nzima

Zaidi ya miti milioni 226 imepandwa Tanzania nzima

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
ZAIDI YA MITI MILIONI 226 IMEPANDWA TANZANIA NZIMA

Kupitia kampeni ya kitaifa ya upandaji miti millioni 1.5 kwa kila Halmashauri nchini, jumla ya miti milioni 226.97 ilipandwa kwa mwaka 2023/2024 ambapo miti milioni 211.81 ndiyo ilistawi ikiwa ni sawa na asilimia 76%.

Tathmini ya miti iliyopandwa kupitia kampeni hii kwa mwaka 2024/2025 inaendelea.

Pia Serikali imeendelea kutoa elimu kuhusu mazingira na kuhamasisha wananchi kupanda miti kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo kwa mwaka 2024/2025 jumla ya miti milioni 150 ilipandwa.

Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar na miaka 60 ya Muungano kwa mwaka 2024 jumla ya miti 53,000 ilipandwa.

Tathmini ya miti iliyopandwa kupitia utaratibu huu kwa mwaka 2024/2025 inaendelea
 

Attachments

  • VID-20250413-WA0035.mp4
    18.9 MB
Back
Top Bottom