Zaidi ya Shilingi Bilioni 600 kujenga upya Hospitali ya Muhimbili, Mkopo utalipwa baada ya miaka 25

Zaidi ya Shilingi Bilioni 600 kujenga upya Hospitali ya Muhimbili, Mkopo utalipwa baada ya miaka 25

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Muhimbili Mpya Inaenda Kuzaliwa,Zaidi ya Bilioni 600 Kutumika,hii ni Bonge la Mradi yaani Sawa na Kujenga Majengo Nusu ya Majengo Yote ya Wizara Pale Dodoma.

---
Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam umesema hospitali hiyo itabomolewa na kujengwa upya.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa Muhimbili ni moja kati ya miradi saba mikubwa ya Serikali iliyoidhinishwa, hivyo itabomolewa na kuanza ujenzi upya.

“Lakini itakwenda kwa awamu si kwamba itajengwa kwa wakati mmoja. Awamu ya kwanza tutaanza upande wa makuti kisha katikati na tutaenda na mbele. Tutaona hospitali nyingine mpya ambayo itakuwa na ukubwa kama huu wa sasa lakini majengo yatakuwa ya kisasazaidi,” amesema Prof. Janabi.

Prof. Janabi amesema kuwa gharama ya kujenga upya hospitali hiyo itakuwa ni zaidi ya Sh bilioni 600 ambazo wamepatiwa kama mkopo nafuu kutoka benki ya Exim na utaanza kulipwa baada ya miaka 25

Chanzo: Habari Leo

My Take
Udom na Ukubwa wake na Majengo Yote Yale ilijengwa Kwa Bilioni 600,Sasa Hiyo Muhimbili itakuwa na jipya gani Hadi igharimu pesa zote hizo? Kuna harufu ya upigaji

Screenshot_20230811-164212.jpg
Screenshot_20230811-164548.jpg

Pia, Soma=> Ufaransa yaipa Tanzania mkopo wa Tsh. Bilioni 361.7 kuzalisha umeme wa jua
 
Wasibomoe. Hizo hela wakajenge hospitali nyingine yenye hadhi zaidi maeneo mengine ya nchi mfano Dodoma Katavi na kwingineko!!

Utekelezaji huu ukifanyika itakuwa ni aibu kwa waliotoa wazo, walosikiliza wazo na kulikubali, kisha kulisimamia kulifanyia kazi!

Hii itakuwa ni kidonda juu ya suala la Bandari!
 
Hawahitaji ushauri wako, wao washafanya uamuzi hadi mkopo ushatolewa, hapo mkandarasi mshauri ni NHC
 
Back
Top Bottom