Zaidi ya Shilingi Bilioni 600 kujenga upya Hospitali ya Muhimbili, Mkopo utalipwa baada ya miaka 25

Serikali ya kipuuzi sana hii. Mipango yote ya hovyohovyo imejaa upigajin
wa fedha za umma
 
Kwan
AJabu kwanini wasitafute eneo jingine kubwa kando ya mji wakajenga hiyo hospitali nyingine ya kisasa badala ya kuongeza msongamano katikati ya mji
 

Hizo ni habari njema lakini nafikiri wangetafuta eneo Jingine hapo Dar wajenge hospitali nyingine mpya kabisa ya Muhimbili kama ilivyo Mloganzila ikisha kamilika wao wakahamia na hayo majengo ya muhimbili kwa sasa yakakodishwa au kuwekwa specialization mbalimbalia; mfano; macho, urinology, moyo nk au wakaifanya iwe National diagnostic unit (Maabara ya Vipimo vya Binadamu) ambapo kutakuwa na vifaa vya kisasa kabisa na kila kipimo kitapatikana hapo kwa haraka na kwa usahihi wa 95%+ bila ya longo longo za MRI imeharibika, umeme umekatika nk
Hii ni huduma muhimu sana kwa wanachi lakini pia kwa Hospitali zetu za juu kwani hakutakuwa na visingizio vya kukosa vipimo (watapeleka sample huko)


KWA HUU UMASIKINI WETU SIONI KAMA NI SAWA KUVUNJA MAJENGO YOTE YALE
 
Exactly
 
Kote sawa tu.Ila kwe pesa hizo bora wangejenga mpya ya rufaa.
Kujenga mpya kuna gharama zaidi.

Ukijenga hospital mpya, unahitaji ununue Vifaa vipya( ambavyo ni Gharama Sanaa).

Unahitaji uwe na madaktari bobezi na Bingwa. Kwa sasa tanzania tulionao ni wachache sana. Na kuwasomesha hawa ni gharama.

Unahitaji uwe na wataalamu wapya( wauguzi, madktari, watu wa madawa n.k.

Kujenga hospital mpya yenye ukubwa sawa na Muhimbili, si project ya kitoto.

Na unaweza fanya yote hayo, hospital ikashindwa kujiendesha.
 
Wewe nawe kama tunaseza nunua ma vx new models kila mwaka, tutashindwa kujenga Sibitali"in my bibis voice". Ni priorities tu.
 
Hili ni wazo zuri sana.

Majengo yale yamechakaa kupita kiasi.
 
Muhimu kuwepo Na angalizo ;

Wazingatie uadilifu mkubwa ktk mradi mzima huo kuanzia mwanzoni hadi mwishoni.

La sivyo majengo yatajengwa sub standard kisha wananchi Ndiyo watakaopata shida.

Yale majengo ya watoto yamejengwa miaka ya hivi karibuni lakini hayafai ukienda bafuni maji yanatuama,


Ujenzi gharama zake huwa ziko quantified ukilazimisha rushwa lazima wajenzi wa-compromise na quality ya kazi nzima.

Muogopeni Mungu .
 
Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam umesema hospitali hiyo itabomolewa na kujengwa upya.

Huu ni upotevu wa fedha...

Hiyo fedha ni bora ingetumika kujenga hospitali nyingine mpya kabisa kama walivyofanya Mloganzila...

Na Muhimbili ya sasa ingeendelea kuwepo kwa kuwa ndani yake kuna taasisi za tiba ambazo bado ni mpya na zina vifaa vizuri tu...
 
Watabomoa Baadhi ya majengo sio yote
 
Kuna muda kama wanaotuongoza kama hawana akili vilee,dah uvunje alafu ujenge
 
 
Hatutaki mawazo yenu. Sisi tumeishaamua lazima muhimbili tuipige chini. Hutaki tutaipiga chini, unataka tutaipiga chini.
 
Kabisa, za sasa (pamoja na Mlonganzila)wangezizatiti kwa vifaa vya kisasa na wataalamu, halafu eneo jingine, kubwa na nje ya msongamano wa Dar(mikoani) ndio wangejenga mpya ambayo ingetoa fursa kwa WaTz wengine wafikiwe kwa ukatibu kuliko wote kuja Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…