Zaidi ya Wakulima wa miwa 11,000 Kilombero Morogoro wameungana na Mpina kumpeleka Bashe mahakamani

Zaidi ya Wakulima wa miwa 11,000 Kilombero Morogoro wameungana na Mpina kumpeleka Bashe mahakamani

Acha kumjibu kwa kejeli. Ni kweli hao wanaotetewa na Mpina wamepandisha bei ya sukari kwa kutengeneza uhaba bandia. Sukari imechezea kati ya Tas 6000 hadi 10000 hapo majuzi. Bashe kanyagia hapo hapo.
umeisoma lakini sheria yenyewe wanayoipinga wakulima?
 
Zaidi ya wakulima wa miwa 11,000 wa Bonde la Mto Kilombero mkoani Morogoro wameungana na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kumpeleka mahakamani Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kuruhusu uingizaji holela wa sukari kinyume cha sheria uliosababisha viwanda vya sukari kushindwa kununua miwa yao kutokana na kukosa soko la sukari na kutaka kuua kilimo cha miwa nchini.

Wakulima hao wamesema sukari imejaa kwenye viwanda kwani sukari ya kutoka nje ambayo imeingia bila kodi imewaathiri zaidi wao wakulima.


Pia soma=> Mpina kuwapeleka Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria
Hawa wakulima wana syndicate yao ndio maana Bei ya sukari iko juu
 
Kwani huko Kilombero na Morogoro hakuna wabunge wa kuwatetea hao wakulima? mmefanya vizuri sana kuungana kwenda mahakamani kupinga hiyo sheria mpya ya bashe kuhusu sukari
CCM na Spika wao kuna wabunge wa kumsifia Samia siyo kuwatetea wananchi. Isipokuwa Luhaga nimemtoa kwenye kundi hilo.
 
Wapeleke miwa viwandani waache ujinga wa kesi hautawasaisia ,watapoteza pesa na na hakuna watakachopata.
Unamsaidia Bashe au vp? Kwahiyo wakulima umewafanya wajinga hawana akili na hawastahili kutetea haki zao! waTanganyika wa leo siyo wa mwaka 47
 
Halafu utakuta pamoja na madhila haya, wakulima hawataonesha hasira yao kwa kuikataa CCM 2024 / 2025 kwa kura nyingi, wataamini propaganda za CCM kuwa inawajali.
 
Wanapoteza muda tu. Mimi ni mwenyeji wa Mbeya. Miaka yote Mbeya sukari tunatumia ya Ilovo kutoka Malawi na inapatikana sana kwa bei nafuu. Na wanaoleta hiyo sukari hawaombi vibari kwa Hussein Bashe.

Jiulize tu kwa nini viwanda vyetu vuinashindwa kuuza sukari kwa bei competitive.

Kesi haina mashiko, hili ni soko huria, wapunguze gharama za uzalishaji na wazalishe sukari nyingi tutanunua
Cartel
 
Back
Top Bottom