Tetesi: Zaidi ya wanawake 1500 wapo Dar es salaam kumpongeza Rais Samia Machi 19, 2023. Hawana nauli za kurudi nyumbani na hawajui wale/walale wapi

Tetesi: Zaidi ya wanawake 1500 wapo Dar es salaam kumpongeza Rais Samia Machi 19, 2023. Hawana nauli za kurudi nyumbani na hawajui wale/walale wapi

Muhimu wamefanikiwa kutekeleza adhma yao ya kumpongeza mama kuupiga mwingi, wasijali sana kuhusu kula au kulala maana hiki ni kipindi cha mfungo wa kwaresma, warudi wakajipange tena kwa ajili ya mwakani........mama hoyeeee....
 
Kuna ujinga mwingine kumuhusisha rais nikumkosea heshima.
 
Khaaa watu wamekodishiwa mabas waende kwa pamoja sema labda kula na kulala tu ambapo walio wengi walilala kwenye gari wenye ndugu walienda kwa ndugu we nae usikuze mambo khaaa! Kama imekosana na mbunge wako deal naye taratibu siyo kutuchafulia chama
 
Not related, ila jina lako limenikumbusha mpenzi wangu wa zamani ningali kijana akiitwa Hasegawa san. Alikuwa mrembo sana na alikuwa anapenda sana kujamiiana ila nilimucha Tokyo mwaka 1994 wala sijui aliendeleaje na maisha yake. Siku moja tulilala kwenye hoteli fulani kule Yokohama (karibu na Minato Mirai), ikawa hatukulala kabisa mpaka asubuhi!
Siku moja mlilala ikawa hamkulala mpaka asubuhi.Mofimu au nahau.Habari mkuu
 
Nilichogundua ukiwa ccm hutakiwi kusema ukweli.

Ccm mnamdangaya mama samia 100% kwa sababu unaweza je kuhamasisha wanawake nchi nzima kwenda Uwanja wa Taifa Dar bila kujali kuhakikisha wanawake wote wamepewa nauli ya kwenda na kurudi, chakula na malazi?
Kama Sio uhaini.

Wamama wengine wamebeba Watoto, wengine ni wajawazito, wengine ni wagonjwa.

Nina Mshauri Mama Samia Usome bandiko Hili na uwaulize wamama wote wakiwa uwanja wa Taifa kama wamewezeshwa chochote utapata majibu. Sahihi na utabarikiwa.

Hali ni mbaya kuliko na manunguniko ni makubwa mnoooo.

Na kuna dalili viongozi wa ccm mikoa na wilaya walipewa fedha ila wameziweka mifukoni na wanawake wote wanalia na kilio hiki kimfikia mama Samia kwa sababu wanarudi mikoani na image mbaya kuhusu Mama Samia.
Hivi kwani ilikuwa lazima muende?

Ni matumizi mabaya ya pesa na muda?

Hivi kupongeza kunaongeza tija gani kwa wananchi?

Mbona miaka ya nyuma hatukuyaona haya?
 
Hivi wajapani si inasemekana sio watu wa mambo hayo sana au wewe ulibahatika tu.
Hapana; watu wote wa maeneo hayo (yaani wachina wakorea na wajapani) wanapenda sana kuchepuka. Wake kwa waume wote ni tabia moja tu, ila wanawake wazuri walikuwa wanapenda sana watu wa nje ili waonekane kwa wenzao kuwa wanajua kiingereza pia. Kwa hiyo wavulana wa kijapani walikuwa wanajipendekeza kwetu kujenga urafiki kusudi wapitie migongo yetu nao wapate wanawake wazuri
 
Njoo kwenye hoja.
Leo kumetokea kituko Dar. Kuna wanawake zaidi ya 1,500 wamewasili Dar kutokea mikoa yote ya Tanzania. Nia ya wao kuja Dar ni Ili waweze kukutana Kesho asubuhi hadi saa nane Mchana Ili kumpongeza mama Samia.

Kwa masikitiko makubwa na huzuni kubwa wamama hao wamelipa nauli kwa fedha za mifukoni mwao wakitarajia kuwa watakuja kurejesha fedha walizotumia kusafiria.

1. Kituko kimeanza baada ya wao kukosa pa kulala wakitarajia kuwa wangekuwa wameandaliwa Maeneo au hotel za kulala. Kilichotokea hawajarejeshewa fedha za nauli za kuja Dar.

2. Hawajui watapata wapi nauli za kurudi makao mikoani.
3. Hawana mahali pa kulala.
4. Hawana uwezo wa kununua vyakula mahotelini.
5. Wengi wameamua kuondoka Kesho Jioni kurudi mikoani baada ya kutoka uwanja wa Taifa saa nane Mchana kwa Wale wachache wenye uwezo.
6. Kesho jumapili Mchana haijulikani watakuwa wapi.
7. Kuhudhuria kongamano hilo masharti ni lazima ununue kitenge 20,000 na kukishona kwa Gharama zako mwenyewe na wote wana sare ya kitenge cha Rais.

8. Wanawake wengine wamekuja na Watoto wadogo ambao wananyonyesha.
9. Wabunge wa ccm wanakotokea Viongozi wa UWT wamegoma Hata kuwachangiachakula, makazi na Usafiri Kwa mantiki kwamba maza anajipongeza mwenyewe na amealika na Bawacha.
10. Zaidi ya Wanawake 110 waliotokea Tarime mkoa wa Mara nauli ni 70,000 kila mmoja kwenda Dar tu, Bado kulala 50,000 na chakula Bado kurudi na walidanganywa na CCM kuwa watalipiwa Kila kitu imekuwa kinyume chake.

11. Wanawake wamekuwa frastrated kwa sababu kuna walioondoka tar 18.3.2023 kuelekea Dodoma Kwa nauli zao, kuna walioelekea Dar uwanja wa Taifa kwa nauli zao the same day, Pia Leo tar 19.3.2023 kuna kundi lililokuja Dar uwanja wa Taifa kwa nauli zao na Kesho wanakwenda Dodoma kwa nauli zao kuonana na tulio tangulia Dodoma.

Wenyeviti wa UWT mikoa yote mungu anawaona. Mama Samia wamama wenzako wako Dar kukufuata kukupongeza ila wamelala uwanja wa Taifa na hawajala na hawajui Kesho watakuwa wapi na watasafi vipi kurudi makwao.

HABARI HIZI UNAZO?KAMA UNAZO OKA WAKINAMAMA HAWA KUEPUSHA LAANA YA WATU WASIO NA HATIA

Wa kutokea kilimanjaro wamefungua uzi wao wanalalamika mateso ya safari hii!
 
Back
Top Bottom