Zaka au sadaka ni hiari, kuwapigia simu waumini kuwakumbusha ni kuwalazimisha

Zaka au sadaka ni hiari, kuwapigia simu waumini kuwakumbusha ni kuwalazimisha

Namna ya utoaji zaka ndo tatizo linapoanzia. Binafsi naona namna sahihi ni kupeleka kwa watoto yatima na watu wasiojiweza maana ndo lengo kuu la zaka. Angalau kanisa katoliki linamiliki vituo kadhaa vya kulea yatima, hao naweza kuwaelewa wakisisitiza utoaji zaka.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Ile kwa watoto yatima,wajane,wafungwa,nk haitwi zaka inaitwa sadaka.
Pana zaka, sadaka, michango, mavuno, shukrani.
KILA moja ina maelezo yake
 
Huendi mbinguni kwakua unatoa sadaka, na wala hutozuiwa kuingia mbinguni kwakua hutoi sadaka. Katika zile amri kumi toa ama usitoe sadaka haipo katika hizo..

makanisa hasa ya kilokole 70% ya muda wa ibada ni kuhubiri baraka utakazopata ukitoa sadaka. Na makanisa haya huwa wana sadaka sijui zaka zaidi ya ngapi kwny ibada moja.

Na siyo hayo makanisa tu, hata katoliki nao wanaelekea hukohuko. Kwny jumuia mnaletewa sijui padre hana godoro sijui hana kile, mumchangie.

Toa sadaka acha kulalamika,mkono unaotoa unayo heri kuliko unaopokea.
 
Utoaji ni kwa ajili ya watu wajuao utajiri ni nini na siri zake nini za kuupata sio kwa ajili.ya malofa wasiotarajia kuwa matajiri kwenye maisha yao

Utajiri una siri nyingi ndio maana watu wengi maskini
Ukiona mtu anatoa iwe sadaka,zaka au kuwapa maskini ,Au kusaidia jamii awe kaokoka au la bila mbwembwe wala kelele jua huyo mtu ana roho ya utajiri.

Mleta mada ni mfano mzuri wa watu wenye roho ya umaskini na pepo la umaskini ukija kutajirika wewe niite mbwa sio rahisi kwa hiyo roho uko.nayo

Mwenye roho ya utajiri hana shida hata ya kusubiri kitabu cha dini kiseme atajenga kanisa au msikiti nk na hata kutoa mamilioni yanayozidi hata hizo zaka na mafungu ya kumi ya vitamins.Yuko juu ya sheria kama Paulo alivyosema siko chini ya sheria tena nimevuka huko

Mtu kuhamasishwa kuwa atoe fungu la kumi kanisani ni ushahidi mmojawapo kuwa kwenye hilo kanisa kuna wengi wenye pepo na roho ya umaskini

Watu wanatoa asilimia tisini ya mapato yao na hawafiliski ni matajiri wakubwa duniani lofa a a struggle kutoa kafungu tu ka kumi na bado hiyo hata asipotoa umadkini unamfuata hadi kwenye nyayo

Tanzania wako watu kibao hutoa nusu za mapato yao na zaidi kusaidia dini na jamii walokole na wasio walokole na hawafiliski

Mleta mada wala hahitajiki malaika ayueleze hali ya maisha yako ikoje ila ukweli ni kuwa una changamoto kubwa za kifedha na pepo la umaskini limeweka makao makuu kwenye maisha yako
Wewe ndo masikini wa kwanza, kwa mtazamo wako huo hutokuja kufanikiwa (kiuchumi)
Siri ya utajiri ni kuheshimu kila senti unayoshika. Ukiona mtu anatoa sadaka au msaada mkubwa basi ujue katoa sehemu kidogo ya mali ambayo haiwezi kuathiri uchumi wake na huwa anajua ataifidia vipi. Chunguza makanisa mengi ya kilokole wamejaa masikini na fukara wa kutupwa!
 
Kwa Kifupi naona wewe ndiye una shida...

Kama mimi ni mimeamua kutoa Sehemu ya Kumi ya mali zangu na kupeleka kanisani na hiyo hela ikatumika kunua vyakula na kulipa mishahara watumishi na kujenga miundo mbinu mizuri ya kiibada wewe kinachokuuma ni nini?

Hata kama ni agano la kale wewe unasumbuka na nini?

Mbona kuna watu wengi wanakesha bar kila siku na kununua pombe za gharama na Nyama na kununua Makahaba na ulafi uliopindukia wanatumia fedha nyingi tena mara nyingine hata mshahara wote?? Hao hauwaoni kuwa wa na shida? Ila unaumia roho kwa Mimi kutoa 10% ya mapato yangu kupeleka kanisani? Unasisitiza kwamba ni Agano la kale..

Kuna vitu vingi sana vya aibu na kutapanya fedha vinafanywa na hao hao wasio walokole lakini hamuoni, ila mnasumbuka na Sadaka...

Pilipili usiyoila yakuwashia nini??
Mimi huwa naelewa wapinga zaka na sadaka,huwa ni wajumbe wa shetani.Ili kuwapumbaza Wakristo wajinga Ili waweze kuwaangusha, sadaka na zaka ni hirizi tosha mchawi akugusi wala kuchezea mali yako.
Wao kwa shetani wanatoa hadi asilimia 80 Ili wapate nguvu. Uleta mafundisho ya kuwakatikisha tamaa Wakristo Ili wasiwe na ulinzi waweze kuwaloga kirahisi.
 
Wewe ndo masikini wa kwanza, kwa mtazamo wako huo hutokuja kufanikiwa (kiuchumi)
Siri ya utajiri ni kuheshimu kila senti unayoshika. Ukiona mtu anatoa sadaka au msaada mkubwa basi ujue katoa sehemu kidogo ya mali ambayo haiwezi kuathiri uchumi wake na huwa anajua ataifudia vipi. Chunguza makanisa mengi ya kilokole wamejaa masikini na fukara wa kutupwa!

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Matajiri wakubwa wanaoongoza duniani ni wayahudi

Wao hata hiyo sheria ya fungu la kumi walishatoka huko

Mtoto toka mdogo hupewa hela ambayo hutakiwa kugawanywa mara tatu

Mfano anapewa elfu sita anaigawa mara tatu

Elfu mbili ya Mungu inapelekwa healing, elfu mbili ya kwake ya kutumia na elfu mbili ya kuweka kwenye vitega uchumi viwe vya familia au vyake ni pesa ya biashara hiyo
Myahhudi siipata milioni tisa mgao huo huo

Na hata wakishinda vita wakateka mali mgao hivyo hivyo

Sababu kubwa wao huamini Mungu anastahili mgao wake kwa kuwa ndie atoae uzima,akili na nguvu za kupata utajiri na asilimia yake kwenye kilichopatikana

Ndio maana nasema utoaji sio kwa ajili ya malofa wasio na mpango wa kutajirika wabaki na vihelq vyao huko after all mtu hata asipotoa hapelekwi jela a aki na vihela vyake
 
Nina mambo kadha wa kadha nataka niongee leo. Kwanza samahani mno kwa ndugu zangu walokole wenzangu kwa maneno na maswali makali ninayokwenda kuuliza humu...
Lazima kwanza uelewe maisha yetu yote yanatakiwa kuwa ushuhuda, pili suala la kumshukuru Mungu halichagui umetendewa makubwa au madogo kwa muono wako, mabaya au mazuri bibilia inasema mshukuruni Mungu Kwa Kila jambo, kama mtoto amefaulu ufaulu wa juu peke yake kuliko wengine, ama alifanya mtihani akiwa anaumwa hajiwezi pengine ulikata tamaa kwamba atarudia tena lakini mtoto akakomaa na akatoboa na ilihali wapo waliokuwa wazima hawajafauru kama yeye na ndani yako unatamani kushuhudia why not?

Nikija kwenye suala la Zaka kwanza kama umeamua kutoa sio hiari ni lazima ila utatoa kadiri Mungu alivyokubarikia, huyo mchungaji anayekupigia simu ni tapeli kwasababu yupo roho mtakatifu was kukumbusha juu ya hilo. Tumsifu Yesu Kristo. Mapendo. Bwana Yesu Asifiweee........
 
Matajiri wakubwa wanaoongoza duniani ni wayahudi

Wao hata hiyo sheria ya fungu la kumi walishatoka huko

Mtoto toka mdogo hupewa hela ambayo hutakiwa kugawanywa mara tatu

Mfano anapewa elfu sita anaigawa mara tatu

Elfu mbili ya Mungu inapelekwa healing, elfu mbili ya kwake ya kutumia na elfu mbili ya kuweka kwenye vitega uchumi viwe vya familia au vyake ni pesa ya biashara hiyo
Myahhudi siipata milioni tisa mgao huo huo

Na hata wakishinda vita wakateka mali mgao hivyo hivyo

Sababu kubwa wao huamini Mungu anastahili mgao wake kwa kuwa ndie atoae uzima,akili na nguvu za kupata utajiri na asilimia yake kwenye kilichopatikana

Ndio maana nasema utoaji sio kwa ajili ya malofa wasio na mpango wa kutajirika wabaki na vihelq vyao huko after all mtu hata asipotoa hapelekwi jela a aki na vihela vyake
Hao hata wasingetoa zaka bado wangefanikiwa maana mafanikio huanzia kichwani kwa mtu.
Vipi kuhusu matajiri wa Kimarekani wasio wayahudi nao wanatoa zaka kwa nani!!!??? Nipe mifano ya matajiri wa hapa Tanzania pia then turudi kwa walokole wako wa hapahapa nchini.
 
KWA shetani watu wanatoa Sana ndio maana wanabarikiwa, mtu akiambiwa alete ng'ombe aulizi mara mbili mbili. Lakini Mkristo anatoa chenji mabaki ndio utegemee atabarikiwa thubutu.

Thus mchawi anamgalagaza Mkristo KWA sababu mchawi anatoa zaka na sadaka kwa shetani, ambayo ni 60% ya mapato yake anatumia 40.

Mkristo kaambiwa atumie 90% kumi tu ndio atoe lakini hawezi.
 
Agano jipya linaanzia kwenye kuzaliwa kwa Yesu mpaka kifo na baada ya kifo chake. Niambie ni wapi Yesu hakusisitiza UPENDO na utii kwa Mungu na kuzifata sheria zake.
 
Hao hata wasingetoa zaka bado wangefanikiwa maana mafanikio huanzia kichwani kwa mtu.
Vipi kuhusu matajiri wa Kimarekani wasio wayahudi nao wanatoa zaka kwa nani!!!??? Nipe mifano ya matajiri wa hapa Tanzania pia then turudi kwa walokole wako wa hapahapa nchini.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Inategemea nani ni Mungu wake.
 
Wewe ndo masikini wa kwanza, kwa mtazamo wako huo hutokuja kufanikiwa (kiuchumi)..
Nchi zikizoendelea zina connection na Mungu kama hujui

Nakupa mfano Marekani ndio nchi pekee duniani ambayo haiamini kuwa pesa pekee ndio msingi wamafanikio

Na wameandika kabisa kwenye pesa yao ya noti ya dola kuwa In God we trust sio in our brain and our plans we trust!!

Narudia .utajiri una siri nyingi mojawapo ni kutoa ndio mabilionea wote wenye na wasio dini kwenye kutoa wanapenda mno.

Ndio maana huhamasisha hadi watu wao kutoa hata wawe dini hawana wanaambiwa basi toeni hata mitumba ziwe nguo.,magari nk vipelekwe kwa maskini Afrika huko

Ndio maana hata wewe waweza kuea mfaidika wa utoaji wao kwa kuvaa mitumba ya bei nafuu au kuendesha kagari mtumba toka ulaya au japani kalikotolewa na mtoaji wa kule kwa kabei kadogo ili kaletwe Africa na wewe maskini wa Afrika walau na wewe uwe na kagari kwa kuwa uwezo wa kununua kapya ulaya au japani huna

Sasa ukishakata kagari kako mtumba jeuri ndio inaanza sadaka au zaka kitu gani ujinga mtupu kisa una kagari used sasa wewe ndie bilionea tajiri kati ya maskini!!!
 
KWA shetani watu wanatoa Sana ndio maana wanabarikiwa, mtu akiambiwa alete ng'ombe aulizi mara mbili mbili. Lakini Mkristo anatoa chenji mabaki ndio utegemee atabarikiwa thubutu.
Thus mchawi anamgalagaza Mkristo KWA sababu mchawi anatoa zaka na sadaka kwa shetani, ambayo ni 60% ya mapato yake anatumia 40.
Mkristo kaambiwa atumie 90% kumi tu ndio atoe lakini hawezi.
Kwa shetani ukitoa unapata zaidi ila huko kanisani (siyo kwa Mungu) ukitoa ndo basi tena dhahama imekukuta! Tuna mifano mingi sana ya watu waliofirisika kwa kujifanya watoaji wakubwa makanisani.
Shetani mdiye mmiliki wa fedha, yeye anajua ni vipi atakupa hizo fedha maana ni miliki yake. Mungu ni mmiliki wa vyote duniani (uhai, afya, na uzima wa milele) isipokuwa pesa.
 
Inategemea nani ni Mungu wake.
Kwani kuna miungu wangapi huko makanisani!? Nnavyojua mimi Mungu ni mmoja so tutayapima mafanikio ya kila mlokole kwa kuamini yanatoka kwa Mungu yuleyule anyewabariki wengine.
 
Agano jipya linaanzia kwenye kuzaliwa kwa Yesu mpaka kifo na baada ya kifo chake. Niambie ni wapi Yesu hakusisitiza UPENDO na utii kwa Mungu na kuzifata sheria zake.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Wapi kabadilisha agano la kale.
Yeye alifuta sheria ngumu za Wayahudi mfano
1.Jino kwa jino akaleta upendo
( positivity)
2.kupondwa mawe KWA mzinzi
3.Wayahudi walifanya sabato kuwa ngumu. Wao walirusha jiwe umbali wa jiwe degree 360 awakutakiwa kufika hadi sabato iishe.
 
Kwann mnamwibia Mungu huku mkijifariji??
Screenshot_20230127_101544_Biblia.jpg
 
Nchi zikizoendelea zina connection na Mungu kama hujui

Nakupa mfano Marekani ndio nchi pekee duniani ambayo haiamini kuwa pesa pekee ndio msingi wamafanikio

Na wameandika kabisa kwenye pesa yao ya noti ya dola kuwa In God we trust sio in our brain and our plans we trust!!

Narudia .utajiri una siri nyingi mojawapo ni kutoa ndio mabilionea wote wenye na wasio dini kwenye kutoa wanapenda mno.
Ndio maana huhamasisha hadi watu wao kutoa hata wawe dini hawana wanaambiwa basi toeni hata mitumba ziwe nguo.,magari nk vipelekwe kwa maskini Afrika huko

Ndio maana hata wewe waweza kuea mfaidika wa utoaji wao kwa kuvaa mitumba ya bei nafuu au kuendesha kagari mtumba toka ulaya au japani kalikotolewa na mtoaji wa kule kwa kabei kadogo ili kaletwe Africa na wewe maskini wa Afrika walau na wewe uwe na kagari kwa kuwa uwezo wa kununua kapya ulaya au japani huna

Sasa ukishakata kagari kako mtumba jeuri ndio inaanza sadaka au zaka kitu gani ujinga mtupu kisa una kagari used sasa wewe ndie bilionea tajiri kati ya maskini!!!
Huyo mungu waliyemuandika kwenye noti zao unamfahamu!? Vipi matendo yao yanasadifu kuamini katika Mungu?
Wao ndo watetezi wa mashoga na ushoga, je ndiyo maagizo ya Mungu waliyemuandika katika noti? Mungu wa kweli haandikwi kwenye noti ambayo ni mali ya shetani.
 
Back
Top Bottom