Nina mambo kadha wa kadha nataka niongee leo. Kwanza samahani mno kwa ndugu zangu walokole wenzangu kwa maneno na maswali makali ninayokwenda kuuliza humu!
Hivi kwa dunia ya sasa mtoto wako kufaulu darasa la saba ni jambo la kumshukuru Mungu mpaka kwenda kanisani KUTOA USHUHUDA?
Ndugu zangu kuna vitu naona kama havi make sense hivi.
Anyway twende kwenye ZAKA.
ZAKA ni sheria ya agano la kale, ambalo YESU alilitimiliza na kutuweka katika neema na si chini ya sheria tena.
Sasa kwa nini Wachungaji wa kileo wanalazimisha watu watoe zaka na kufikia mpak hatua ya kuwapigia simu kuwakumbusha?
Mtume Paulo anasema, "kama umeacha agano la kale liache lote(acha sheria zake zote), na kama unalifuata basi fuata na sheria zake zote".
Sasa kwa nini ndugu zangu WALOKOLE mnachagua chagua? Mpo agano jipya la imani ila kwa nini mnazing'ang'ania baadhi ya sheria ili ziwanufaishe?
Ni bora muweke wazi tu kuwa ZAKA ni hiyari na siyo lazima, kuliko kuwalazimisha watu mpaka kupigiana simu kukumbushana.
Mwisho, naamini Mungu anatoa utajiri na haangalii unamcha au humchi, akiamua yeye anakupa tu. Ila hii haimaanishi tusimche yeye.
Kuna watu wana miaka na miaka wanamuomba Mungu utajiri ila Mungu anasema NO.
Wakipata sana basi ni laki laki za kula tu ili wasife.
Mungu anaangalia zaidi moyo wako, anajua utakuwaje akikupa utajiri.
Zaidi hongereni ndugu zangu mliopata bahati ya kuteuliwa na Mungu mwenyewe muwe matajiri(wa halali lakini siongelei wale wenye ndumba) ili muwatunze wengine.
Asubuhi njema!
Ila msisahau maswali yangu nasubiri majibu hapa.i
Kwa Kifupi naona wewe ndiye una shida...
Kama mimi nimeamua kutoa Sehemu ya Kumi ya mali zangu na kupeleka kanisani na hiyo hela ikatumika kunua vyakula na kulipa mishahara watumishi na kujenga miundo mbinu mizuri ya kiibada wewe kinachokuuma ni nini?
Hata kama ni agano la kale wewe unasumbuka na nini?
Mbona kuna watu wengi wanakesha bar kila siku na kununua pombe za gharama na Nyama na kununua Makahaba na ulafi uliopindukia wanatumia fedha nyingi tena mara nyingine hata mshahara wote?? Hao hauwaoni kuwa wa na shida? Ila unaumia roho kwa Mimi kutoa 10% ya mapato yangu kupeleka kanisani? Unasisitiza kwamba ni Agano la kale..
Kuna vitu vingi sana vya aibu na kutapanya fedha vinafanywa na watu lakini hamuoni, ila mnasumbuka na Sadaka...
Pilipili usiyoila yakuwashia nini??
Lipa zaka acha kujitetea, asiyelipa zaka anamwibia Mungu kwa hiyo siyo hiari ni lazima kulipa zaka "Malaki 3:7-10"