Zaka au sadaka ni hiari, kuwapigia simu waumini kuwakumbusha ni kuwalazimisha

Zaka au sadaka ni hiari, kuwapigia simu waumini kuwakumbusha ni kuwalazimisha

Agizo la Mungu ni "TOENI MALI ZENU MUWAPE MASIKINI" kanisa hupokea kwa niaba ya masikini (wahitaji) kwahiyo ni sahihi zaidi kupeleka zaka yako kwa wahitaji moja kwa moja maana viongozi wa siku hizi wamekuwa na tamaa kupita kiasi, wanakula pesa za wahitaji hadharanj!
Wewe huwezi kujua wahitaji zaidi ila kanisa linajua. Pia acha kuwasema kwa ubaya watumishi wa Mungu.
 
Wewe huwezi kujua wahitaji zaidi ila kanisa linajua. Pia acha kuwasema kwa ubaya watumishi wa Mungu.
Nisiwajue wahitaji ambao naishi nao mtaani!? Kanisa liwafahamu ila mimi nisiwafahamu!? Hauwezi kuwa serious.
Alafu siyo kwamba nawasema watumishi ila nasema ukweli: watumishi wengi wa siku hizi hasa wa makanisa ya kilokole wanasukumwa na ubinafsi na tamaa ya mali. Angalia namna wanavyotambiana kwa fahari za dunia (majumba, magari n.k) na wakati huo ujue hawana biashara nje ya utumishi wao kwa kanisa so hayo ni matumizi mabaya ya mapato ya kanisa ambayo yangeweza kuwanufaisha wahitaji wengi huko mitaani.
 
Hao wa mtaani ni wahitaji kuliko wagonjwa wa kansa wanaohitaji huduma ya mionzi ambayo hospitali za kanisa zinatoa? Unadhani ni nani anayetoa pesa za kugharamia matibabu yao zaidi ya nyinyi waumini.

We endelea kuwasema vibaya watumishi, utaharibikiwa.
 
Hiari ya kilazima, maana sio hiari ya hiari.

Mnasimamishwa kwny benchi wote, kisha wanasimama wa benchi linalofuata kwnda kutoa sadaka. Kwa hali hii huwezi unajisikia vyema usinyanyuke kwnda kutoa wakt wenzio wote benchi zima wamesimamishwa.

Sasa hapo sadaka sio moja tu, mnaweza kwenda zaidi ya mara 4. Kuna kanisa moja hamtoi kwny kikao, mbarusha pale mbele madhabahuni lila mtu anaangalia nani amerusha nini.

Utasikia njooni mtoe sadaka za ulinzi, kwamba kadri unavyotoa nyingi ndio unapata ulinzi mkubwa, halafu wakt wa kuondoka yy mchungaji anaondoka na msururu wa bodyguards.

Sadaka ni matokeo ya fungu la kumi kwa kile Mungu alichokubarikia.
Hama kanisa kama hukubaluani na taratibu zao au kaanzishe lako utakaloendesha kwa hayo mawazo yako yawe sawa au sio.sawa wapishe wenyewe wenye kanisa lao usiwabungudhi kwa lolote iwe kunungunika au chochote .Hama.Uache kelele zako kwenye makanisa ya watu
 
hakuna anaekulazimisha utoe zaka! ni upumbavu wako tu kudhani kukumbushwa zaka haustahili, tunakumbushwa mengi sio zaka tu! una roho ya kichawi ndio maana haupendi maombi ,na nyie ndio mkipata shida muda wote unamtaka mchungaji, mbwa koko wewe silimu uwe muislam labda kule hawatoi zaka shetani wewe!
 
Zaka na Sadaka(dhabihu) ni ibada Kwa YESU na siyo hiyari.
Kutorejesha ni kuiba.

Malaki 3:8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.

Malaki 3:9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
 
Zaka ni fungu la kumi la mapato yako.
Sadaka ni fungu la kumi la mapato yako.
Jumla 20/100

Zaka ni 1/10.
Sadaka 1/10.
Jumla 2/10.

Zaka ni 10/100.
Sadaka ni 10/100.
Jumla 20/100.

Mfano umepata laki Moja, Zaka na Sadaka Jumla ni 20,000.

Wewe utabakiwa na 80,000 mkononi Kwa ajili ya matumizi yako binafsi yanayofaa.

Tubarikiwe Sana na YESU tunapoamua Kwa vitendo kurejesha Zaka na Sadaka Kwa uaminifu. Amina na Haleluya Sana.
 
Nina mambo kadha wa kadha nataka niongee leo. Kwanza samahani mno kwa ndugu zangu walokole wenzangu kwa maneno na maswali makali ninayokwenda kuuliza humu!

Hivi kwa dunia ya sasa mtoto wako kufaulu darasa la saba ni jambo la kumshukuru Mungu mpaka kwenda kanisani KUTOA USHUHUDA?

Ndugu zangu kuna vitu naona kama havi make sense hivi.

Anyway twende kwenye ZAKA.
ZAKA ni sheria ya agano la kale, ambalo YESU alilitimiliza na kutuweka katika neema na si chini ya sheria tena.

Sasa kwa nini Wachungaji wa kileo wanalazimisha watu watoe zaka na kufikia mpak hatua ya kuwapigia simu kuwakumbusha?

Mtume Paulo anasema, "kama umeacha agano la kale liache lote(acha sheria zake zote), na kama unalifuata basi fuata na sheria zake zote".

Sasa kwa nini ndugu zangu WALOKOLE mnachagua chagua? Mpo agano jipya la imani ila kwa nini mnazing'ang'ania baadhi ya sheria ili ziwanufaishe?

Ni bora muweke wazi tu kuwa ZAKA ni hiyari na siyo lazima, kuliko kuwalazimisha watu mpaka kupigiana simu kukumbushana.

Mwisho, naamini Mungu anatoa utajiri na haangalii unamcha au humchi, akiamua yeye anakupa tu. Ila hii haimaanishi tusimche yeye.

Kuna watu wana miaka na miaka wanamuomba Mungu utajiri ila Mungu anasema NO.

Wakipata sana basi ni laki laki za kula tu ili wasife.

Mungu anaangalia zaidi moyo wako, anajua utakuwaje akikupa utajiri.

Zaidi hongereni ndugu zangu mliopata bahati ya kuteuliwa na Mungu mwenyewe muwe matajiri(wa halali lakini siongelei wale wenye ndumba) ili muwatunze wengine.

Asubuhi njema!
Ila msisahau maswali yangu nasubiri majibu hapa.
Wachungaji wapige simu kuwakumbusha waumini kusali, kutubu na kuwapenda wengine na SIO kulipa zaka. Hilo sio jambo la kwanza kwenye Agano Jipya!
 
Zaka na Sadaka(dhabihu) ni ibada Kwa YESU na siyo hiyari.
Kutorejesha ni kuiba.

Malaki 3:8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.

Malaki 3:9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Zaka sio sadaka kwa Yesu! Kwanza “sadaka” siku hizi za Agano Jipya ni YESU KRISTO mwenyewe na vinginevyo vitolewavyo makanisani ni matoleo, michango, dhabihu,nk. Ila huwezi kuwaambia wachungaji kitu kuhusu zaka kwani ndipo moyo wao ulipo.
 
Hama kanisa kama hukubaluani na taratibu zao au kaanzishe lako utakaloendesha kwa hayo mawazo yako yawe sawa au sio.sawa wapishe wenyewe wenye kanisa lao usiwabungudhi kwa lolote iwe kunungunika au chochote .Hama.Uache kelele zako kwenye makanisa ya watu
Kama kuna sehem kwny bible imekosewa ni kutuita waumini kondoo. Maana hata kwny ukweli unaogopa kusema. Unadhani wewe Dada yehodia ingeitwa kitimoto usingehoji?

Makanisa yasijengwe kwa nia ya kukusanya hela. Huyo Yesu mwenyewe na mitiume wake walifanya kazi huku wanahubiri injili tofauti ya haya unayoita makanisa TRA B.

""Nimeongea na watendaji wa serikali yangu kuhusu baadhi ya wahubiri kucheza na imani za wakenya. Kuanzia sasa yule anataka kuuza maji asajiliwe na mamlaka ya maji, yule anataka kuuza mafuta asajiliwe na food and drugs authority, na yule anataka kuuza mbegu asajiliwe wizara ya kilimo. Watambulike kama wafanyabiashara, na serikali ijue wanauza ngapi kwa siku na walipe kodi. Huku kwa kanisa wabaki wanaohubiri neno la Mungu, sio wafanyabiashara. Hatuwezi kuruhusu imani za wakenya kuchezewa na wakora wachache, wanaotaka kujitajirisha kupitia shida za waumini wetu" William Samoei Ruto, Rais wa Kenya, 23/01/2022 Kiambu county."

Wakt unaniambia nihame kanisa, na wao kawaambie waanzishe kanisa sebuleni kwao kwa kukusanya sebuleni kwao.
Na ww kuwa mwenye akili, wapi imeandikwa Utaenda mbinguni kwa kutoa sadaka, au hutaenda mbinguni kwakua hutoi sadaka. Why sadaka imekuwa ndio naenda kanisani kwa wachungaji na mapdre badala ya neno la Mungu.
 
Wachungaji wapige simu kuwakumbusha waumini kusali, kutubu na kuwapenda wengine na SIO kulipa zaka. Hilo sio jambo la kwanza kwenye Agano Jipya!

Injili itapelekwa kwa maneno matupu?lazima wawezeshwe kifedha ili kuandaa mikutano ya kiiinjili,kujenga makanisa n.k
 
Zaka na Sadaka(dhabihu) ni ibada Kwa YESU na siyo hiyari.
Kutorejesha ni kuiba.

Malaki 3:8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.

Malaki 3:9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Hiyo malaki 3:9 hapo kwenye taifa ni taifa gani Hilo Mungu alikuwa anawaambia hivyo?? Maana alikuwa specific kabisa...... So why mtuhamishie Watanzania
 
Wachungaji wapige simu kuwakumbusha waumini kusali, kutubu na kuwapenda wengine na SIO kulipa zaka. Hilo sio jambo la kwanza kwenye Agano Jipya!
Njia sahihi ni kuwaombea wawe na roho ya ukarimu sababu Mungu humpenda yule atoaye kwa ukarimu pasipo kulazimishwa
Anyway sababu ya wengine kuwa wagumu kutoa sababu mojawapo ni kuwa hawaamini Mungu ndie kawapa kuwa ni nguvu na akili zao ndio zimewezesha hivyo
Wanaojua kuwa Mungu ndie kawapa hawana shida na hutoa sana tena kwa hiari bila kiburi wala majikwezo wala kelele
 
Huendi mbinguni kwakua unatoa sadaka, na wala hutozuiwa kuingia mbinguni kwakua hutoi sadaka. Katika zile amri kumi toa ama usitoe sadaka haipo katika hizo..

Makanisa hasa ya kilokole 70% ya muda wa ibada ni kuhubiri baraka utakazopata ukitoa sadaka. Na makanisa haya huwa wana sadaka sijui zaka zaidi ya ngapi kwny ibada moja.

Na siyo hayo makanisa tu, hata katoliki nao wanaelekea hukohuko. Kwny jumuia mnaletewa sijui padre hana godoro sijui hana kile, mumchangie.
Katoliki hawaelekei huko,wako huko tangu mwanzo. Hakuna kinachofanyika hawakuwahi kukifanya
 
Hata walokole wanstubu/kuungama kwa wachungaji. Baadae hutengwa(kuwekwa viti vya nyuma). Wakikamilisha vifungo wanaongozwa sala ya toba.
Mbona hata kuungama mwenyewe inaruhusiwa! Siyo lazima kuungama kwa mchungaji.
 
Kwa kuacha agano la kale maana yake tuibe ,tuzini na tuseme uongo au una maanisha nini
Hizo ni moral laws ndugu ambazo zipo pia kwenye agano jipya kwenye amri mpya ya UPENDO. Zipo sheria nyingi za agano la kale ambazo mfano za kutawaza au vyakula ambazo hazimo tena kwenye agano jipya
 
Back
Top Bottom