Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habari. Assume wewe ni mfugaji wa Kiebrania. Umepewa urithi wa ng'ombe 100 na baba yako. Ndani ya mwaka wakazaliwa ngombe 20. Ukawa na ng'ombe 120. Wakati wa kutoa zaka unefika.

Je utatoa ng'ombe wawili kama asilimia kumi ya ng'ombe ishirini walioongezeka au utatoa ng'ombe 12 kama asimilia kumi ya ng'ombe 120 ulionao? Vipi mwaka huo upate majanga na kubakiwa na ng'ombe 80. Utatoa zaka kiasi gani?
 
Kwa mfanyakazi wa mshahara, unatoa 10% ya mshahara wako maana yale ni malipo ya kazi uliyofanya, ila biashara, faida ya mtaji wako ndo unatoa 10%

je mfanya kazi mwenye mshahara ya 1m kwa mwezi atatoa 100k au atasubir kwanza akate gharama zote alizoingia katika kufanya io kazi mfano nauli kwenda ofisini, chakula akiwa ofisin nk atoe asilimia 10 ya bakaa itayobaki? naomba unijibu mkuu
 
Kwa mshahara wa 1m after PAYE, utatoa 100K na alafu hela inayobakia, 900K ndo yako sasa inahusika na mambo mengine.
 
Mimi natoa kwenye faida mkuu..

MALAKI 3:8-10:-"Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? MMENIIBIA ZAKA NA DHABIHU. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. LETENI ZAKA KAMILIghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la."
 
Back
Top Bottom