Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Kabla sijajibu naomba urejeree kwanza vifungu vifuatavyo...​


Yn 4:24​

"Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."

Mwanzo 2:7

"BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. "

"And the LORD God formed man of the dust of the ground, and breathed into his nostrils the breath of life; and man became a living soul."


Ayubu 14:22

Lakini mwili ulio juu yake una maumivu,
Na nafsi yake ndani huomboleza.
Jibu Sasa....
 
LIni Roho wa Mungu alianza kukaa ndani ya watu?
Unataka kumaanisha alianza kukaa kipindi cha agano jipya?

Lini Kanisa lilianza kuwa hekalu?
Unataka kuniambia Kipindi cha Paulo?
Jibu ni kwamba yote yalikuwepo tangu zmani na yalifahamika...

Na ndo maana paulo anavyoongea kwenye 1 wakorintho 6:19..

Hasemi kwamba "nawaambieni kwamba....."
Ila anatumia neno "Au Hamjui kuwa....." ikiwa inamaanisha kuwa ni jambo lililokuwa Tangu zamani...

So tangu zmaani kulikuwa na roho mtakatifu,Tangu zamani Hekalu lilihesabiwa kuwa mwili ,tangu zamani Vyote vilikuwepo japo vilikuwa kwa namna nyingine..

Mhubiri 1:9​

"Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua."
Jamaa analeta propaganda maana hapa tunazungumzia hekalu lililofanyika kwa mikono na kanisa lililofanyika kwa mikono na zaka inayo tolewa kwenye makanisa yaliyo fanyika kwa mikono na ile iliyo tolewa kwa hekalu lililo fanyika kwa mikono ....hayo mambo ya hekalu la roho na kanisa la roho ni vitu vingine vilivyo nje ya mada ....jamaa ana taka kuleta ubishi husio na akili.
 
Habari. Assume wewe ni mfugaji wa Kiebrania. Umepewa urithi wa ng'ombe 100 na baba yako. Ndani ya mwaka wakazaliwa ngombe 20. Ukawa na ng'ombe 120. Wakati wa kutoa zaka unefika.

Je utatoa ng'ombe wawili kama asilimia kumi ya ng'ombe ishirini walioongezeka au utatoa ng'ombe 12 kama asimilia kumi ya ng'ombe 120 ulionao? Vipi mwaka huo upate majanga na kubakiwa na ng'ombe 80. Utatoa zaka kiasi gani?
Kwanza hili neno zaka la kiiburenia au kiswahili?tuanzia hapa kwanza
 
Na hawa je?
2023_11_22_22.39.37_edit.jpg
 
Hakuna watumishi wa Mungu hapo wachungaji wote ni wezi kwa niaba ya hawa hapa chini
2023_11_22_22.39.37_edit.jpg
 
naamini hii kodi tunayoilipa serikali na PAYE ndio zaka zenyewe.

Maana hii kodi na PAYE serikali si ndio inazitumia kupeleka huduma kila mahala, kununua madawa hospitalini, nk.

Zaka ni mfumo uliokuwepo zama za kale kabla ya hizi serikali.... ndiyo ilikuwa kama kodi zama hizo.

Ni mtazamo wangu.
 
Habari. Assume wewe ni mfugaji wa Kiebrania. Umepewa urithi wa ng'ombe 100 na baba yako. Ndani ya mwaka wakazaliwa ngombe 20. Ukawa na ng'ombe 120. Wakati wa kutoa zaka unefika.

Je utatoa ng'ombe wawili kama asilimia kumi ya ng'ombe ishirini walioongezeka au utatoa ng'ombe 12 kama asimilia kumi ya ng'ombe 120 ulionao? Vipi mwaka huo upate majanga na kubakiwa na ng'ombe 80. Utatoa zaka kiasi gani?
Achaneni na huyo ujinga. Unatoaje 10% kanisani wakati una ndugu kibao maskini.
 
Back
Top Bottom