Faida ni kile Mungu alichokuwezesha kukipata baada ya wewe kuwekeza mtaji, hicho ndicho unachopaswa kukitolea zaka ya asilimia 10 au zaidi ukiamua hivyo.
Mwanzo 14:16
Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.
Mwanzo 14:20
Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Abraham alimpa kuhani Melikizedeki fungu la kumi la vitu vyote alivyovitwaa kutoka kwa wale wavamizi (asilimia kumi ya faida aliyopata).
Kumbukumbu la Torati 14:22
Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
Toa fungu la kumi la 'maongeo: yote ya mbegu zako......(faida inayotokana na mbegu zako kwenye shamba mwaka baada ya mwaka).
Kumbukumbu la Torati 14 28
Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;
Toa fungu la kumi la maongeo (mapato,maongezeko) yako ya mwaka huo ndani ya malango yakk.