Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Hakuna aijuaye siku hiyo ila Mungu Baba tu nukta.Tuambie sasa alichomaanisha Yesu na tuonyeshe kwa andiko Yesu alipokiri anaijua siku ya kiama.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna aijuaye siku hiyo ila Mungu Baba tu nukta.Tuambie sasa alichomaanisha Yesu na tuonyeshe kwa andiko Yesu alipokiri anaijua siku ya kiama.
Tunaiba sanaHiyo haipo bwana! Ukienda kichwa kichwa tunafunga biashara. Tena mimi nimeenda mbali zaidi kama nina rejesho natoa kabisa hilo rejesho kwenye faida inayobaki ndiyo nakokotoa 10% yake!
Bhasi nafikiri una vingi zaidi vya kujifunza...Kanisa ndiyo hekalu
Wewe umetoa maana ya hekalu 'kidini' na kwa tafsiri ya sheria za dini ya Kiyahudi ...........hayo ni kwa mujibu wa mapokeo ya kidini kabla ya Kristo na ndivyo ilivyokuwa zamani hizo.Bhasi nafikiri una vingi zaidi vya kujifunza...
Ntakufafanulia kwa leo Kwa Faida Yako na wanaosoma wengine kwa sababu kama Nitakuacha ukiwa na Mindset hii na mimi nilijua Ukweli nitahukumiwa (Kama kuna hukumu) ksa hilo..
Sasa karibu kufatilia kwa uelewa zaidi
Hekalu na Kanisa ni vitu Viwili tofauti kimuundo kimaana na kimchoro..
Kuna vitu vitatu watu hushindwa kuvitofautisha Hekalu,Sinagogi na Kanisa...
Ntaanza na HEKALU
Hekalu kwenye biblia huitwa בית המקדש (beit hamiqdash)
Yaani Nyumba Takatifu kwa tafsiri ya neno kwa neno ila tafsiri ya Moja kwa moja ndo mnaita Hekalu..
Sasa mzee unajua lilitokea wapi Mpaka kuitwa hivyo?
Maneno mengi ya Kiswahili yamekopwa Kutoka katika Lugha ya kiarabu kwahiyo neno Hekalu limetokana na neno la kiarabu "haykalun" (هيكل)...
Ambalo humaanisha "Nyumba Ya Mungu"
Japo hata kiaramaic pia hikal" (ܥܘܩܐ) ambalo nalo humaanisha "Nyumba Ya Mungu"
Fun enough ni kwamba Waarabu walikopa Neno hilo kutika katika lugha ya kiaramu na sisi tumekopa kutoka katika kiarabu...
Mpaka sasa Yamekuwepo Mahekalu mawili tu katika Historia..
Hekalu la kwanza ni lile alilojenga Mfalme suleiman...
Unaweza ukasoma 1 Wafalme 6 mpaka 1 Wafalme 9. (1 Wafalme 6-9)
Hekalu lilijengwa na Mfalme Sulemani, mwana wa Mfalme Daudi, katika karne ya 10 KK. Sulemani alianza kujenga hekalu mwaka wa 480 KK, na likakamilika miaka saba baadaye, mwaka wa 473 KK.
Kama unakumbuka Vizuri Nebukandreza II Mfalme wa Babel ndo alilivunja Hekalu hilo na kuivamia Israeli..
(Unaweza ukasoma tena 2 Wafalme 25:8-17)
Na Hekalu la pili lilijengwa tena na Zerubabeli baada ya Waisrael Kurudi tena Kutoka uhamishoni
(Ukisoma kwenye Daniel 9 anatabiri yote hayo na anataja miaka kabisa ya kufanyika yote)
Hata hivyo mwaka 70 Baada ya Kuzaliwa Yesu Lilibomolewa tena na Warumi...
Na halikujengwa tena..
HEKALU HUWA NI MOJA DUNIA NZIMA Au kwa lugha nyepesi lilikuwa moja tu,(Ndiyo ibada za upatanisho,Kafara,Na maondoleo ya madhambi hufanyika..
Ni Sehemu ambapo Kuna Chumba maalumu Kinaitwa PATAKATIFU PA LATAKATIFU..
na Hiyo sio sehemu ya kufanya Ibada mara kwa mara japo makuhani na Watu waliowatakatifu hufanya kazi humo...
Ni tofauti Na sinagogi wala kanisa ambalo sinagogi huwa ni mengine pengine hata kila baada ya Nyumba kumi utakuta sinagogi...
Sinagogi huwa mengi na huwa ni sehemu ya kusali,Kuimba zaburi wakati Hekalu sio..
Sasa Kanisa limetokana na neno la kiyunani (Kigiriki) linalitwa ekklesia. Tafsiri ya moja kwa moja ni Mkutaniko na Tafsiri ya neno kwa neno "ek" ni kutoka na "kaleo" ni Kuitwa ...
Kwahyo unaweza kusema ni "Jamii ya walioitwa kutoka" au "Jamii ya walioitwa..."
Na hekalu huwa na Ramani maalum iliyokuwa Design na Mungu mwenyewe
HII NI RAMANI YA HEKALUI..
View attachment 2830131
Ni swali zuri. Naomba Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa.Habari. Assume wewe ni mfugaji wa Kiebrania. Umepewa urithi wa ng'ombe 100 na baba yako. Ndani ya mwaka wakazaliwa ngombe 20. Ukawa na ng'ombe 120. Wakati wa kutoa zaka unefika.
Je utatoa ng'ombe wawili kama asilimia kumi ya ng'ombe ishirini walioongezeka au utatoa ng'ombe 12 kama asimilia kumi ya ng'ombe 120 ulionao? Vipi mwaka huo upate majanga na kubakiwa na ng'ombe 80. Utatoa zaka kiasi gani?
Hapo mnaposema mapato yako kama faida kuna utata sana, unataka kusema faida ndiyo inayolindwa tu na siyo mtaji?....Ni swali zuri. Naomba Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa.
Kwanza ujue maana ya zaka Soma Malaki 3:10-12
1. Mungu anamkemea yeye alaye wala hataharibu mazao ya Ardhi yenu.
2. Wala mzazi wenu hautapukitisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba yenu asema Bwana wa Majeshi
Lengo la kukueleza hivi kwamba ukitoa zaka usahau habari ya majanga uliyoyataja hapo Kwenye post yako. Mungu atasimamia uchumi wako kikamilifu kabisa. So Hakuna hasara tena.
Lingine nikusaidie kuja. Ukiona Kwenye Bibilia Mungu amejifunua kama Bwana wa Majeshi uelewa hapo kuna vita ....Mean Mungu atapigana upande wako utakaa salama na uchumi wako utastawi sana.
SASA TURUDI KWENYE FUNGU LA KUMI NI NINI
AU 10% NI NINI
Fungu la kumi ni sehemu ya 10 ya mapato ya Mapato yako kama faida iliyopata
Unampa Mungu 10% yake. Na lazima iwe kamili.
Alisema mwana ajui ila baba .....mwana ni mwili baba ni nafsi ya mungu ...hivyo alivyo sema mwana ajui alimaanisha mwili ila nafsi yake inajua ...pia alipo sema mwana wa adamu atakufa na siku ya 3 hata fufuka alimaanisha mwili ndio ulio kufa na kufufuka siku ya tatu ila nafsi yake ni mungu haiwezi kufa hata sekunde moja ndiyo maana alipo kuwa msalabani anamwambia yule jamaa leo hii utakuwa,pamoja nami pema peponi.....hivyo wanafunzi wake walipo pewa lile jibu walidhani yesu kasema hajui hiyo siku .....ila kiakili alipo sema baba alimaanisha nafsi yake ...ndiyo maana kuna sehemu wanafunzi wake walimwambia tuonyeshe baba na sisi tutalidhika akawaambia nyinyi mpo nami siku zote msinijue anionaye mimi kamwona baba .Tuambie sasa alichomaanisha Yesu na tuonyeshe kwa andiko Yesu alipokiri anaijua siku ya kiama.
Mungu baba ndiyo nafsi ya kristoHakuna aijuaye siku hiyo ila Mungu Baba tu nukta.
Kuna kitu unachanganya...Alisema mwana ajui ila baba .....mwana ni mwili baba ni nafsi ya mungu ...hivyo alivyo sema mwana ajui alimaanisha mwili ila nafsi yake inajua ...pia alipo sema mwana wa adamu atakufa na siku ya 3 hata fufuka alimaanisha mwili ndio ulio kufa na kufufuka siku ya tatu ila nasfi yake ni mungu aiwezi kufa hata sekunde moja ndiyo maana alipo kuwa msalabani anamwambia yule jamaa leo hii utakuwa,pamoja nami pema peponi.....hivyo wanafunzi wake walipo pewa lile jibu walidhani yesu kasema hajui hiyo siku .....ila kiakili alipo sema baba alimaanisha nafsi yake ...ndiyo maana kuna sehemu wanafunzi wake walimwambia tuonyeshe baba na sisi tutalidhika akawaambia nyinyi mpo nami siku zote msinijue anionaye mimi kamwona baba .
Alisema mwana ajui ila baba .....mwana ni mwili baba ni nafsi ya mungu ...hivyo alivyo sema mwana ajui alimaanisha mwili ila nafsi yake inajua ...pia alipo sema mwana wa adamu atakufa na siku ya 3 hata fufuka alimaanisha mwili ndio ulio kufa na kufufuka siku ya tatu ila nasfi yake ni mungu aiwezi kufa hata sekunde moja ndiyo maana alipo kuwa msalabani anamwambia yule jamaa leo hii utakuwa,pamoja nami pema peponi.....hivyo wanafunzi wake walipo pewa lile jibu walidhani yesu kasema hajui hiyo siku .....ila kiakili alipo sema baba alimaanisha nafsi yake ...ndiyo maana kuna sehemu wanafunzi wake walimwambia tuonyeshe baba na sisi tutalidhika akawaambia nyinyi mpo nami siku zote msinijue anionaye mimi kamwona baba
Ni somo pana sana hili ila nitakuja kuliweka hapa tubadilishane uelewaKuna kitu unachanganya...
Niambie tofauti ya roho na nafsi ?......na 'kazi' za kila kimoja ni ipi ?
Neno roho kwa kiswahili linatumika vibaya maana wakati mwingine linatumika kama nafsi ....ila kiufasaha neno roho ni spirit ndiyo energy kisayansi...Kuna kitu unachanganya...
Niambie tofauti ya roho na nafsi ?......na 'kazi' za kila kimoja ni ipi ?
Jamani 😂Kwenye hizi mambo ya imani kumejaa utapeli mtupu, mtu anachukua mkopo benki baba yake wa kiroho anamwambia toa fungu la kumi kwa ajili ya ulinzi wa huo mkopo🦍
LIni Roho wa Mungu alianza kukaa ndani ya watu?Wewe umetoa maana ya hekalu 'kidini' na kwa tafsiri ya sheria za dini ya Kiyahudi ...........hayo ni kwa mujibu wa mapokeo ya kidini kabla ya Kristo na ndivyo ilivyokuwa zamani hizo.
Wewe umezungumzia hekalu kwa mfano wa jengo kubwa....hiyo ni kwa mujibu tafsiri za kidini,l.
Kwa agano jipya baada ya kufa na kufufuka kwa Kristo ambapo kulianzisha Kanisa, Mungu haishi ndani ya hayo majengo makubwa kama zamani tena, hata kwenye roho na mioyo ya watu Roho Mtakatifu anaishi humo.
Kwa Sasa 'Hekalu' sio jengo kubwa tu la nje, hata mwili wako ni hekalu la Mungu.
Tunaposema tunapeleka zaka hekaluni, hata tukipeleka kwenye madhabahu huko kanisani tunapokutana kuabudu ni sahihi kabisa maana Mungu pia yupo humo.
Hata mwili wako pia ni hekalu la Mungu.
1Wakorintho 6:19
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Soma neno la Mungu kwa tafsiri ya rohoni ili uyaelewe maandiko na sio kwa tafsiri ya sheria za mapokeo ya kidini.
TAngu juzi umeamka vizuri sana unajibu vitu kwa elimu nimependa sana..Neno roho kwa kiswahili linatumika vibaya maana wakati mwingine linatumika kama nafsi ....ila kiufasaha neno roho ni spirit ndiyo energy kisayansi...
kila kitu ni roho ndiyo maana ufalme wa mungu alisema ni ufalme wa roho ...nafsi ndiyo uzima wa kujitambua
Kama ndio hivyo mbona unatuambia hekalu ni jengo ?LIni Roho wa Mungu alianza kukaa ndani ya watu?
Unataka kumaanisha alianza kukaa kipindi cha agano jipya?
Lini Kanisa lilianza kuwa hekalu?
Unataka kuniambia Kipindi cha Paulo?
Jibu ni kwamba yote yalikuwepo tangu zmani na yalifahamika...
Na ndo maana paulo anavyoongea kwenye 1 wakorintho 6:19..
Hasemi kwamba "nawaambieni kwamba....."
Ila anatumia neno "Au Hamjui kuwa....." ikiwa inamaanisha kuwa ni jambo lililokuwa Tangu zamani...
So tangu zmaani kulikuwa na roho mtakatifu,Tangu zamani Hekalu lilihesabiwa kuwa mwili ,tangu zamani Vyote vilikuwepo japo vilikuwa kwa namna nyingine..
Mhubiri 1:9
"Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua."
Kuna kitu unachanganya...
Niambie tofauti ya roho na nafsi ?......na 'kazi' za kila kimoja ni ipi ?
Hekalu ni jengo na pia ni mwili ....yote yaliyoandikwa kweny biblia ni kivuliKama ndio hivyo mbona unatuambia hekalu ni jengo ?