Kama ni hivyo mbona sheria za zaka mnataka ? Au sheria mnazichambua nyinyi kua zipi mpo chini yake na zipi ampo chini yake ...uwezi kusema sheria za HEKALU NI HARAMU KWA SASA ILA SHERIA YA ZAKA YA HEKALU NI HALALI.
Zaka ni lazima kutoa kwa faida yako mwenyewe ili kuepuka laana.
Malaki 3:8
Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani?
Mmeniibia zaka na dhabihu.
Malaki 3:9
Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
Malaki 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Malaki 3:11
Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
Malaki 3:12
Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.
Asiyetoa zaka ni sawa na anayekula chakula chote bila kuhifadhi akiba (mbegu).
Kanisa la sasa lina mamlaka na ukuu kuliko hekalu la kale.