Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Huko wizi mtupu, mimi naijuwa zakat ya Kiislam tu, kama una swali lolote kuhusu hiyo niulize.
 
Ndyo kuna ubaya kwa sababu huduma za hekalu hazipo tena sasa unampa nani?
Sauli kuna kisa alishika vazi la samweli likapasuka katikati akaambiwa ufalme wako umepasuliwa kwa maana umekataliwa ...wapumbavu wa makanisani wa leo wanabisha kuwa hekalu alipo tena mungu kalikataa katika kanuni aliyo sema yesu kuwa ...mara ngapi nimekukusanya kama vifaranga lakini umekataa basi nyumba yako umeachiwa ukiwa .....pia wasome uzinduzi wa hekalu mungu alisema nini juu ya Israel kuhusu hekalu kuwa kama wana wa Israel watamuasi yeye basi atalipiga hilo hekalu hata watu wa mataifa watashangaa kakisema hawa walimfanya nini mungu wao ....kitendo cha yesu kukuta wahuni hekaluni ndiyo ushuhuda kuwa hekalu lilikataliwa kwa kupasuka kwa pazia vipande viwili.
 
Sisi wakristo tuna Kanisa sio Sinagogi hivyo kupeleka zaka kanisani ni sahihi kabisa.
Somo tena nilicho andika ujaelewa wakati ule wa hekalu kulikuwa na nyumba za ibada nyingine nyingi tu zote azikuitwa hekalu kwa sababu hekalu ni moja tu milele ....sasa nilisema kwanini watu awakupeleka zaka kwenye nymba za ibada za sinagogi ambazo ndiyo sawa na makanisa ya sasa? Sababu ni kuwa zaka ni sadaka ya hekalu tu ambalo sanduku la agano la musa lilikuwa hapo.
 
Uwa kuna mafundisho kwamba zaka inatakiwa itolewe kwa usahihi yaani bila kuongeza au kupunguza, hivyo ibaki moja ya kumi ya faida. Sasa bila kutoa PAYE, NSSF na gharama nyingine zilizopelekea kupata huo mshahara kama usafiri wa kwenda kazini, chakula n.k. hicho kiasi sahihi cha kupunguzwa moja ya kumi yake kama zaka utakipataje?
Yani Mungu kwanza....mshahara ukiingia tu kabla ya kuanza kutumia au kulipa madenii tenga zaka asilimia 10 ya icho kilichoingia kwenye account then ndo uanze ku
 
Somo tena nilicho andika ujaelewa wakati ule wa hekalu kulikuwa na nyumba za ibada nyingine nyingi tu zote azikuitwa hekalu kwa sababu hekalu ni moja tu milele ....sasa nilisema kwanini watu awakupeleka zaka kwenye nymba za ibada za sinagogi ambazo ndiyo sawa na makanisa ya sasa? Sababu ni kuwa zaka ni sadaka ya hekalu tu ambalo sanduku la agano la musa lilikuwa hapo.
Hizo zilikuwa ni desturi za dini ya Kiyahudi kulingana na torati Ila kwa agano jipya hatuishi tena chini ya hizo sheria za Kiyahudi huku kwenye agano jipya tunaishi kwa 'imani'........

ndio maana kwenye kanisa lolote mradi Mungu amekuelekeza usali hapo ni sahihi kabisa kutoa Zaka hapo.
 
Acha kunitukana, jadili kistaarabu.

Sababu ya Daudi kutoruhusiwa kumjengea Mungu hekalu inajulikana wazi ndio maana baadae Sulemani alilijenga, hivyo yeyote angeweza tu kujenga hata wewe.

Hekalu na Sinagogi hakuna tofauti yeyote, ila Sinagogi kubwa ndio huitwa hekalu kwa desturi za Kiyahudi.

Hekalu ni mahali pa ibada katika dini ya Kiyahudi, wakati sinagogi ni jengo la ibada na kusanyiko la Kiyahudi lililotumika kwa sala na kufundisha Torati. Hekalu kuu lililokuwepo lilikuwa Hekalu la Yerusalemu lililoharibiwa, na sinagogi ni vituo vya ibada vya jamii za Kiyahudi duniani kote.

Hata Kanisa ni hekalu pia
Hiyo sababu nyinyi mnapo jenga makanisa ninani aliwaambia mjenge ....hekalu siyo kitu cha mchezo mchezo ndiyo maana daudi na utakatifu wake wote alikataliwa
 
Kwa kanuni za Muumba kuna matunda ya malimbuko yaani (wazaliwa wa kwanza) na fungu la kumi katika faida uliopata,so hapo utatoa wawili baada ya kupata 20 kama faida.

Ila kikanuni kila mtaji unatakiwa kuutolea fungu la kumi kabla hujaanza biashara au uzalishaji ili kumtanguliza Muumba katika jambo unalofanya so kama umepewa ng’ombe 100 basi 10 ni fungu la Muumba wako.
 
Hizo zilikuwa ni desturi za dini ya Kiyahudi kulingana na torati Ila kwa agano jipya hatuishi tena chini ya hizo sheria za Kiyahudi huku kwenye agano jipya tunaishia kwa 'imani'........

ndio maana kwenye kanisa lolote mradi Mungu amekuelekeza usali hapo ni sahihi kabisa kutoa Zaka hapo.
Kanisa la ukristo wa kweli siyo jengo bali ni mwili wa mtu binafsi tumia akili
 
Muumba hali zile fedha au mali unazotoa kama zaka (matunda) bali ule moyo wako unavyohiari kutoa ni harufu ya manukato kwake na ndo anavyotaka. Ila zile fedha zinatumika kukuza utukufu wake kupitia watumishi wake na kujenga majengo ya ibada.
 
Hiyo sababu nyinyi mnapo jenga makanisa ninani aliwaambia mjenge ....hekalu siyo kitu cha mchezo mchezo ndiyo maana daudi na utakatifu wake wote alikataliwa
Kwa agano jipya hekalu sio jengo tu hata mwili wako ni hekalu la Mungu.

1Wakorintho 6:19
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

Kusema hekalu ni jengo la kipekee ni kufuata desturi/sheria za kale za Kiyahudi Ila kwa agano jipya hatuishi tena chini ya hizo sheria.
 
Acha kunitukana, jadili kistaarabu.

Sababu ya Daudi kutoruhusiwa kumjengea Mungu hekalu inajulikana wazi ndio maana baadae Sulemani alilijenga, hivyo yeyote angeweza tu kujenga hata wewe.

Hekalu na Sinagogi hakuna tofauti yeyote, ila Sinagogi kubwa ndio huitwa hekalu kwa desturi za Kiyahudi.

Hekalu ni mahali pa ibada katika dini ya Kiyahudi, wakati sinagogi ni jengo la ibada na kusanyiko la Kiyahudi lililotumika kwa sala na kufundisha Torati. Hekalu kuu lililokuwepo lilikuwa Hekalu la Yerusalemu lililoharibiwa, na sinagogi ni vituo vya ibada vya jamii za Kiyahudi duniani kote.

Hata Kanisa ni hekalu pia
Wewe hauna akili kabisa ....sasa kama mtakatifu daudi alizuiwa na mungu kujenga hekalu wewe unafananisha hekalu ma sinagogi ...wakristo wengi mnaukataa huu ukweli kwa sababu ya uchu wa pesa ...hata ujenge jengo kubwa na zuri kuliko lile hekalu... ilo jengo aliwezi kuwa hekalu ......hekalu ni moja tu narudia tena hekalu ni moja tu .sheria,za hekalu zipo tena zilitolewa na mungu mwenyewe walawi ndiyo wasimamizi wa hekalu toka kabla alijajengwa hadi lilipo jengwa je ilo kanisa walawi ndiyo wasimamizi ? Sipendi kubishana na wapumbavu ...
 
Yes,wanatunza wasiojuweza
Ht kkkt niliyopo mie pia wanafanya hivyo
Na Kuna mchungaji anawatembelea
Hata Roman ipo kwenye parokia yangu, hawatangazi lakini kwa sisi wengine tunaoenda kanisani kila siku, i know more than one person anayesaidiwa na pesa za zaka. Wengine wanalipiwa ada, wengine bill za hospitali na vyakula. Ila wanapeleka huko misaada na kifupi we are not supposed to know wanafanyia nini zaka zetu. Sisi tumemtolea Bwana, sio Padre wala mchungaji.
 
Hata jengo tunalokutanika kufanya ibada kuliita kanisa sio kosa wala dhambi.
Siyo kosa kuliita kanisa au sinagogi ila ni kosa kuliita hekalu wacha ubishi ...hekalu lilikuwa na sheria zake na kabila moja tu ndiyo lilipewa ruhusa kulisimamia .
 
Hata hayo ya walokole pia yametofautiana
Kuna yenye mifumo ,km Yale makubwa yenye matawi mpk mikoa,Wana utaratibu pia!

Ila haya ya mtu mmoja mmoja ndo hivyo!
Lkn pia mi nimeenda baadhi ya makanisa,nyie acheni tu sadaka unakuta ht elf 20 haifiki!

Hayo mnayoona watu wanakula na yana watu wengi wenye uwezo,watoaji ni machache sn ukilinganisha na ya kawaida
Siku hizi watoaji wa zaka wengi kanisani hawaendi. Hao wachungaji unaowaona wana makanisa sadaka hata 20k haifiki, wengi wanapanua huduma yao kwenda mahospitalini, shuleni na sehemu mbalimbali kwenye jamii kutatua shida za watu. Afterwards hao watu, Mungu huwa anawasaidia kwa kiwango kikubwa, ndo mwanzo wa kuanza kutuma zaka kwa wachungaji ili waombewe. Hizi scenario nishaziona sana mjini yaani.
 
In maana mpaka karne hii hekalu ni moja tu ?

Kwani ibada za hekaluni na kwenye sinagogi zina tofauti gani ?
Kuhusu ibada ndiyo kulikuwa na utofauti hekalu lilikuwa na kabila moja tu lililo kuwa limepewa amri ya daima ya kulisimamia mtu asiye wa ilo kabila ilikuwa haramu kusimamia hekalu ....pia hekalu kulikuwa na sanduku la agano la mungu ...tena kuna maneno ya mungu aliyo yasema juu ya hekalu lake tofauti na masinagogi au nyumba nyingine yoyote ya ibada.
 
Wan
Wapo wale wengine pia ambao wanawabana wafanyakazi mpaka wanakondeana kwa mawazo,unakuta mshahara ni mil.2,umekopa unapata kigari chako na nyumba,makato kila mwezi unabakiwa na laki 3,anakwambia toa 10% ya basic salary yako,hapo ndio utakapoona kuwa kaumini kwako kumegeuka maumivu...
Wanakwambia Mungu kwanza!
 
Back
Top Bottom