Kwenye desturi za kale za Kiyahudi kazi za hekaluni zilifanywa zaidi na kuhani mkuu ambaye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja kwa mwaka.
Ila baada kifo cha Kristo kilichozaa agano jipya na kanisa, wale wote waliomkiri Kristo wanaweza kupaingia patakatifu pa patakatifu.
Tupe andiko kwamba Zaka iliacha kuwepo lini?....
Rabbon Mfalme Sulemani
Ndugu
Proved usibishane na watu wasioamini uwepo wa Roho MTAKATIFU,
Aliye na Roho mtakatifu anajulishwa yote,
Sadaka na ZAKA haijawahi kukatazwa, zaidi sana sadaka na ZAKA imeongezeka Kutoka 10 % Hadi 100% wakati mwingine, itategemea Roho mtakatifu amekusemeshaje Kwa habari ya Kutoa.
Tumeona zakayo aliposamehewa dhambi na YESU, ametoa nusu ya Mali zake zote na alikuwa tajiri, mfano mtu mwenye utajiri wa BL 100 atoe 50%zaka, huoni hiyo ni kubwa sana zaidi ya ZAKA ya kawaida?
Mama mjane akatoa senti chache alizokuanazo ambapo alotoa Kila kitu alochokuwa nacho 100%.
Hanania na Saphira, waliuza shamba na wakaadhimia kwenda Kutoa pesa yote ya kuuza shamba miguuni pa mitume Kwa ajili ya INJILI.
In short, ukiongozwa na Roho mtakatifu, huwezi kuuliza mara mbili kuhusu Kutoa Kwa ajili ya INJILI.
Yeyote anayekwambia Usitoe ZAKA na sadaka kwamba ni AGANO jipya ni Roho ya mpinga kristo inawaongoza hao.
INJILI itahubiriwa vipi watu tusipotoa sadaka na ZAKA? Watumishi watakula nini nk nk!!
Mungu akubariki.