Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Mtaji siyo mapato?..
Ukipewa magari kumi utasubiri yazalishe mengine ndiyo utoe ili uyaite mtaji na mengine faida au utatoa 01 kama sehemu ya kumi?.
Ukipewa ng'ombe 100 utasubiri wazae au uuze mbolea ndiyo utoe faida au?..
 
Biblia kwenye zaka imetamka na ipo mifano kadhaa imeelekeza kutumika kichwa au kutokukariri labda ni kupindisha maelekezo.
Sasa mkuu ni hivi,
Zaka tutatoa kwenye net faida, sio faida ghafi, na Mbinguni tutaenda tutakaa seat za mbele kabisa
 
Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23 Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. 24 Na njia
 
Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako; ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata
 
Kuna mbegu inapandwa ukishavuna ndio zaka itolewe,lazima Kuna process ya uzalishaji,mfano mtu akikupa mtaji 1000000,hutakiwi kuitolea zaka ila unaweza kuitolea sadaka ya shukrani,
Ukikopa million kumi unaweza kuitolea shukrani lakini siyo zaka,zaka utatoa baada ya kuzalisha hyo Hela na kupata faida,
Ulipata urithi wako milioni 150 unaweza kutoa shukrani million 20 lakini siyo zaka,hakuna double payment,
Wengine akikopea benk m 10 anatoa zaka lakini Kila mwezi mshahara ulikuwa unatolewa zaka
 
Kuna mbegu inapandwa ukishavuna ndio zaka itolewe,lazima Kuna process ya uzalishaji,mfano mtu akikupa mtaji 1000000,hutakiwi kuitolea zaka ila unaweza kuitolea sadaka ya shukrani,
Ukikopa million kumi unaweza kuitolea shukrani lakini siyo zaka,zaka utatoa baada ya kuzalisha hyo Hela na kupata faida,
Ulipata urithi wako milioni 150 unaweza kutoa shukrani million 20 lakini siyo zaka,hakuna double payment,
Wengine akikopea benk m 10 anatoa zaka lakini Kila mwezi mshahara ulikuwa unatolewa zaka
Chochote unachojaliwa sehemu Moja kati ya kumi si mali yako hata ukijaliwa saa 24 Kwa siku elewa saa 2 na dakika _ siyo yako
 
Habari. Assume wewe ni mfugaji wa Kiebrania. Umepewa urithi wa ng'ombe 100 na baba yako. Ndani ya mwaka wakazaliwa ngombe 20. Ukawa na ng'ombe 120. Wakati wa kutoa zaka unefika.

Je utatoa ng'ombe wawili kama asilimia kumi ya ng'ombe ishirini walioongezeka au utatoa ng'ombe 12 kama asimilia kumi ya ng'ombe 120 ulionao? Vipi mwaka huo upate majanga na kubakiwa na ng'ombe 80. Utatoa zaka kiasi gani?
Hakuna Kitu kinaitwa zKa kwa sasa hivi
 
Zaka ya asilimia 10 unatoa kote kwenye faida na kwenye utajiri lkn kwa kwenye utajiri unatoa baada ya muda fulani, wa miaka 3, au 5 itategemea na upandaji thaman ya mali zako.
Niongezee kwenye zaka ya mali itakuwa unapigia hesabu kile kilichoongezeka mfano thaman ya mali zako now ni 1000 sp utatoa 100 utatoa zaka then baada ya miaka 5 inakuwa na thaman ya 1500 kinaongezeka 500 unatoa zaka kilichoongezela 50 hvyo hvyo


NB: Kwa karne hii yaipaswi kutolewa kanisani, ipeleke kwa wahitaji😁
Safi sana ⚘️⚘️⚘️🌺🌺🌺🌺
 
Zaka ni sadaka ya hekalu ila wapumbavu mnapeleka makanisani hata kule Israel zamani zaka ilipelekwa hekaluni tu siyo kwenye masinagogi na hekalu lilikuwa moja tu hata ujenge mengine hayawezi kuwa hekalu ....tumieni akili acheni upumbavu makanisani
Kuna Muda unaongea point sana..
Kama hapa umenifurahisha kusema ukweli!
 
Back
Top Bottom