Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Kwa kifupi 10% ni kwa kila ulichopata! Umepewa ng'ombe 100 unapaswa kutoa 10% kwa mara ya kwanza.
Baada ya hapo unaanza kutoa 10% ya Faida.
Sasa ukikutana na Wachungaji waliojaa tamaa ya hela,watakwambia ni 10% ya (Mtaji +Faida) kila mwezi! Ukifilisika wanakutimua Kanisani.
Wakitaka kukubana vizuri wanakupa Fomu ya kujaza! Unatakiwa kujaza vyanzo vyako vya mapato yote, kazi, biashara, zawadi, nk harafu wanakukadiria kiwango cha kutoa kila Mwezi.
Sasa kwa mfanya biashara wanakukadiria (Mtaji + Faida)! Sasa bila kujali kuwa biashara yako inaweza kukwama na usipate Faida, hilo hawaangalii.
Usipotoa unaitwa Mwizi, ukikwama zaidi wanakwambia umekufa kizaka!
Shughuli ukisema unajifufua, sikiliza mtiti wake!!
 
Zaka ya asilimia 10 unatoa kote kwenye faida na kwenye utajiri lkn kwa kwenye utajiri unatoa baada ya muda fulani, wa miaka 3, au 5 itategemea na upandaji thaman ya mali zako.
Niongezee kwenye zaka ya mali itakuwa unapigia hesabu kile kilichoongezeka mfano thaman ya mali zako now ni 1000 sp utatoa 100 utatoa zaka then baada ya miaka 5 inakuwa na thaman ya 1500 kinaongezeka 500 unatoa zaka kilichoongezela 50 hvyo hvyo

NB: Kwa karne hii yaipaswi kutolewa kanisani, ipeleke kwa wahitaji😁
 
Kwa kifupi 10% ni kwa kila ulichopata! Umepewa ng'ombe 100 unapaswa kutoa 10% kwa mara ya kwanza.
Baada ya hapo unaanza kutoa 10% ya Faida.
Sasa ukikutana na Wachungaji waliojaa tamaa ya hela,watakwambia ni 10% ya (Mtaji +Faida) kila mwezi! Ukifilisika wanakutimua Kanisani.
Wakitaka kukubana vizuri wanakupa Fomu ya kujaza! Unatakiwa kujaza vyanzo vyako vya mapato yote, kazi, biashara, zawadi, nk harafu wanakukadiria kiwango cha kutoa kila Mwezi.
Sasa kwa mfanya biashara wanakukadiria (Mtaji + Faida)! Sasa bila kujali kuwa biashara yako inaweza kukwama na usipate Faida, hilo hawaangalii.
Usipotoa unaitwa Mwizi, ukikwama zaidi wanakwambia umekufa kizaka!
Shughuli ukisema unajifufua, sikiliza mtiti wake!!
Wapo wale wengine pia ambao wanawabana wafanyakazi mpaka wanakondeana kwa mawazo,unakuta mshahara ni mil.2,umekopa unapata kigari chako na nyumba,makato kila mwezi unabakiwa na laki 3,anakwambia toa 10% ya basic salary yako,hapo ndio utakapoona kuwa kaumini kwako kumegeuka maumivu...
 
Habari. Assume wewe ni mfugaji wa Kiebrania. Umepewa urithi wa ng'ombe 100 na baba yako. Ndani ya mwaka wakazaliwa ngombe 20. Ukawa na ng'ombe 120. Wakati wa kutoa zaka unefika.

Je utatoa ng'ombe wawili kama asilimia kumi ya ng'ombe ishirini walioongezeka au utatoa ng'ombe 12 kama asimilia kumi ya ng'ombe 120 ulionao? Vipi mwaka huo upate majanga na kubakiwa na ng'ombe 80. Utatoa zaka kiasi gani?
Zaka ni sadaka ya hekalu ila wapumbavu mnapeleka makanisani hata kule Israel zamani zaka ilipelekwa hekaluni tu siyo kwenye masinagogi na hekalu lilikuwa moja tu hata ujenge mengine hayawezi kuwa hekalu ....tumieni akili acheni upumbavu makanisani
 
Zaka ya asilimia 10 unatoa kote kwenye faida na kwenye utajiri lkn kwa kwenye utajiri unatoa baada ya muda fulani, wa miaka 3, au 5 itategemea na upandaji thaman ya mali zako.

NB: Kwa karne hii yaipaswi kutolewa kanisani, ipeleke kwa wahitaji😁
Kwenye hiyo sentensi ya mwisho yenye NB hawatakuelewa!😀😀
 
Kwa mfanyakazi wa mshahara, unatoa 10% ya mshahara wako maana yale ni malipo ya kazi uliyofanya, ila biashara, faida ya mtaji wako ndo unatoa 10%
Kwanini wachungaji na wasiajiriwe nao wakatoa fungu la 10?

je wao hawaruhisiwi kutoa fungu la 10 na kama wanatoa je wazipata wapi kama siyo kuchukua humohumo kwanwalizoleta waumini walio maskini wengi wao?
 
Habari. Assume wewe ni mfugaji wa Kiebrania. Umepewa urithi wa ng'ombe 100 na baba yako. Ndani ya mwaka wakazaliwa ngombe 20. Ukawa na ng'ombe 120. Wakati wa kutoa zaka unefika.

Je utatoa ng'ombe wawili kama asilimia kumi ya ng'ombe ishirini walioongezeka au utatoa ng'ombe 12 kama asimilia kumi ya ng'ombe 120 ulionao? Vipi mwaka huo upate majanga na kubakiwa na ng'ombe 80. Utatoa zaka kiasi gani?
Unatoka 20,faida ya kile kilichozaliwq/ongezeko!

Huwezi kutoa 120
 
Kwanini wachungaji na wasiajiriwe nao wakatoa fungu la 10?

je wao hawaruhisiwi kutoa fungu la 10 na kama wanatoa je wazipata wapi kama siyo kuchukua humohumo kwanwalizoleta waumini walio maskini wengi wao?
Hata wachungaji pia wanatoa 10%
Kutoka kwenye malipo Yao.
Hii ni Kwa wale walioko kwenye mifumo maalumu ya kanisa!
Nikisema mfumo,namaanisha wale walioajiriwa na wanalipwa,mfano makanisa ya ,kkkk, Anglikana,morovian,etc..Roman Sina uhakika km wanalipwa mishahara...
Haya ya kilokole yanegawanyika huko mambo ni mengi🙌

Km hatoi ss ni shida yake binafsi,ila anatakiwa kutoa pia
 
Mimi natoa kwenye faida mkuu..

MALAKI 3:8-10:-"Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? MMENIIBIA ZAKA NA DHABIHU. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. LETENI ZAKA KAMILIghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la."
Malaki ndiyo nani bwana?Babu wa babu yako anamjua malaki?

Huko nyuma kabla ya dini za kuja fungu la 10 WAAFRIKA tulikuwa tunampa nani?

Achana na kukalilishwa hadithi ktk biblia jakuna kitu hicho
 
Kwanini wachungaji na wasiajiriwe nao wakatoa fungu la 10?

je wao hawaruhisiwi kutoa fungu la 10 na kama wanatoa je wazipata wapi kama siyo kuchukua humohumo kwanwalizoleta waumini walio maskini wengi wao?
Wachungaji pia wanapaswa kutoa fungu la kumi kutokana na mshahara wanaoupata. Tatizo you don't know the things of God.
 
Malaki ndiyo nani bwana?Babu wa babu yako anamjua malaki?

Huko nyuma kabla ya dini za kuja fungu la 10 WAAFRIKA tulikuwa tunampa nani?

Achana na kukalilishwa hadithi ktk biblia jakuna kitu hicho
Malaki alikuwa nabii wa Mungu wa miungu yote duniani.
 
Back
Top Bottom