Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,686
- 46,842
Alichokiandika Meneja Habari Wa Azam ZakazaKazi Baada Ya Yanga Kuishinda Simba…
SASA NI TANO KWA TANO
Agosti 9, 2023 Azam FC ilifungwa 2-0 na Yanga kwenye Ngao ya Jamii jijini Tanga,
Shabiki mmoja wa Simba aliyefahamika kama Kisugu, alitokwa povu jingi sana na kuonesha dharau kubwa kwa viongozi wa Azam FC na mpira wa miguu kwa ujumla.
Huu ulikuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Azam FC kupoteza dhidi ya Yanga, na wa nne kwa jumla ndani ya michezo mitano...katikati yake kulikuwa na sare moja, na mechi zingine ziizosabisha waamuzi kufungiwa, akiwemo Ahmed Arajiga.
Licha ya Azam kupoteza na waamuzi kufungiwa, lakini Yanga wenyewe walilalamika kwamba Azam FC inakamia.
Maana yake walipewa mechi zilizowafanya wakalale na viatu.
TURUDI KWA TIMU YAKE
Kipigo cha 2-0 cha leo ni cha TANO mfululizo kwa Simba, ndani yake kukiwa na kifurushi kikubwa cha 5-1.
Na katika mechi zote hizi tano, hakuna hata moja ambayo Yanga walilalamika kwamba wamekamiwa...zilikuwa nyepesi na za upande mmoja utadhani sio watani wa jadi.
Nadhani huu ni muda muafaka kwa Kisugu kutoka hadharani na kumueleza Mohamed Dewji, kama alivyomueleza Bakhresa, kwamba katika viongozi wa Simba, kuna mapandikizi ya Yanga.
Maana sijawahi kusikia hata mara moja timu yoyote kufungwa michezo mitano mfululizo na Yanga, zaidi ya Simba ya sasa.
Haya yote Kisugu anayaona lakini hasemi kitu...au Kisugu mwenyewe ndio Yanga?
HEBU TUKOKOTE KIDOGO
5 = vipigo mfululizo
5 = kipigo kikubwa ndani yake
5 X 5 = 25....mwaka wa uchaguzi
Kwa kifupi hii ina maanisha MITANO TENA kwa mama!