Zama za Haji Manara zipo ukingoni na asipokuwa makini zitalazimishwa kutamatika

Zama za Haji Manara zipo ukingoni na asipokuwa makini zitalazimishwa kutamatika

Wakati mwingine ujuaji usio na kiasi huweza kumsababishia mhusika matatizo yasiyo ya lazima mbele ya safari ambayo pengine angefika salama.

Haji Manara kwa mfano. Bwana yule hujifanya anayo mengi ayatambuayo. Na kutokuwa kwake makini na ayasemayo, hatimaye yanaelekea kumfitinisha hata na waliopo kwenye mfumo ( serikalini).

Kwa msiofahamu, mapema jana, bwana Haji kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, alidai haoni mantiki ya timu za Taifa kuchangiwa na Wananchi ilhali gharama zote zihusuzo ushiriki wake kwenye mashindano mbalimbali yaliyo chini ya chama cha soka barani Afrika, hugharamikiwa na wao (CAF).

Huenda bwana Haji alikuwa sawa kutoa malalamishi yale, pengine. Lakini unajiuliza, je, bwana yule hakugundua halibio lile lingewaathiri hata maswahibaye walio ndani ya mpango ule wa upigaji!? Kwamba, Haji hatambui tawi pekee (Serikali) linalomfanya aweze japo kubaki akining'inia asidondoke ndilo hilo ameanza kulitusi eti linamuumiza?

Hakika, naanza kuuona mwisho wa zama za Haji! Na akiendelea kufanya mchezo, hata hizo zama zilizopo ukingoni-zitawahishwa na ujuaji wake usio na kiasi.

Acha muda/mda uwe Mwalimu.
Tanzania ni nchi ya ajabu sana.
Uhalifu unalindwa kwa gharama yeyote ile
 
Ana hoja asikilizwe,,,ni aibu kubwa kwa timu ya taifa kupitisha bakuli kwa wanainchi..


Serikali imejaza watu wengi kwenye msafara wa timu ya taifa ambao hawana faida zozote,,
Halafu mnawabebesha wanainchi mzigo wa gharama.
Sijawahi kuona dunia kote kwenye msafara wa timu imejaza wanasiasa na wacheza comedy balada ya kujaza football veterans.

Manara ana hoja asipuuzwe .
Ni aibu kubwa! Team ya Taifa ichangiwe kwa lipi? mbona zile 10m kwa kila Goli zingewekwa vizuri wasingehangaika kuchangia? huu ni uhuni tu uliovuka mipaka. Haji ana hoja
 
Nakuheshimu sana Mjoli wa Bwana ila hapa umeenda kwenye Personal attack na hakuna hoja iliyojibiwa. Mjibuni, kama mama aliwapa Milioni 500 baada ya kufuzu na kule CAF anatoa Milioni 10 kwa goli, kwanini serikali isibebe huu mzigo. Ikishindwa serikali, kwanini TFF wasiubebe huu mzigo? Pesa wanazokusanya TFF zinaenda wapi?
1. Mauzo ya Jez.
2. Simba na Yanga kutumia uwanja wa Mkapa.
3. NBC wadhamini wa ligi.
4. Azam TV.

Wao ndo wagawa tenda nani aoneshe na nani atangaze ligi kuu ya Tanzania.
 
Tatizo la haji anazeeka vibaya kwanza kwa umri wake anatakiwa busara zake ziongee zaidi kuliko sifa zake zakijinga, haji anadharau, anakiburi na jeuri, hana nidhamu....ndio maana simba walimtimua na ndio maana kila mwanamke anaemuoa anamkimbia....haji anashida
Kihuni hoja ya Hajj siyo kumshambulia tu bila majibu.
 
Ni aibu kubwa! Team ya Taifa ichangiwe kwa lipi? mbona zile 10m kwa kila Goli zingewekwa vizuri wasingehangaika kuchangia? huu ni uhuni tu uliovuka mipaka. Haji ana hoja
Kabisa mkuu .
Hii aibu kubwa kwa taifa.
 
Uzuri wa Haji ulopokaji wake huwa wa uongo na ukweli. Yeye haangalii hizo impact zake. Nyie walaji wa matamshi yake ndio mjipime.

Ila ni ushamba kupitisha bakuli kuzisaidia timu ambazo mamlaka husika zinabajet zake. Kama hatuna hela sio lazima tushiriki mashindano yote.

Mbona serikali haichangishi kununua mabasi ya mwendokasi yawe mengi tuache kubanana kama mbuzi tunaopelekwa mnadani.

Majanga tuombe msaada, michezo, bajet kuu nako bakuli.

Hatuwezi kuendesha masuala yetu kwa kuchangishana kwa raia na makampuni yanyolipa kodi.
 
Back
Top Bottom