miss pablo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2018
- 5,411
- 11,025
Sasa hv nauli balaa. Hakuna gari ya bei hiyo mkuu.. yaaan kisafiri sasa hv ujipangee.Tatizo ni hapo wanachukua 33k wakati gari ni ordinary wanatakiwa 17k. MBUZI WAKUBWA.
Kubadili namba kutoka private kwenda private inaruhusiwa kumbeAlinunua kwa dar lux akabadili namba ila ilikuwa 908 DNU
Kwa mganga, baada ya kusemwa halina huduma nzuri, nadhani wameenda kumshughulikia mleta mada.Hilo basi limeenda kufanya nini huko?
Anakaribia kufikisha lorry 250 kama sio 300 tanzania na zambiaMmiliki wake inaweza kuwa uchumi umeyumba
Nakumbuka enzi izo ilikua kila baada ya li saa inatuharibikia kufika mikumi likagoma na kuendelea na safari service toka morogoro mjini ndo kidogo ikasaidia tukafika dar saa 7 toka mbeya iyo ni 2006Hiyo kampuni hata kama hapo katikati ilikuwa inatoa huduma nzuri, niseme tu kwa sasa hiyo huduma wanayotoa sasa hivi ndio level zao. Kwa sie wahenga tuliosafiri mwanzoni mwa miaka ya 2000 tulikuwa tunaikwepa maana mnaweza kuishiwa mafuta njiani....enzi hizo kampuni ilikuwa inajulikana kama Kilimanjaro trucks au Sawaya
N.B. Kama taarifa ya kweli lakini maana kwa gari za Arusha kwa Kilimanjaro Express sio mbaya sana
Hata mimi nikienda Arusha huwa napanda haya mabus ya Esther,Extra luxury au Happy nation na silipagi zaidi ya 25k.Arusha panda
1. BM
2. Tilhisho
3. Marangu
Ukikosa hayo panda
4. Extra luxury
5. Esther
Ukikosa haya hairisha safari ndugu hao wakina Kilimanjaro sijui Dar express wamejichokea ni safari za kubahatisha.
BM ndo basi ya kupandaJuzi kati nikawa na kijisafari cha kuelekea mikoa ya huko kaskazini mwa Tanzania. Nikasema ngoja nipande Kilimanjaro express, duh kwa kweli nilijuta sana kupanda lile basi.
Cha kwanza tulidanganywa kuwa basi ni luxury hivyo tukakatishwa nauli kubwa ila kiuhalisia hakuna luxury bus pale, bus siti zake zimechakaa, ndani linatoa harufu kama ya uvundo flani hivi, hakuna cha AC wala TV ndani ya basi. Basi lilikuwa limejaza kiasi kwamba abiria wengine wakawa wamekaa pale mbele kwa dereva na tulikuwa tukifika karibu na mizani wanawashusha baadhi ya abiria wanawachukulia bodaboda then tunawakuta mbele ya safari tukishavuka mizani.
Wahudumu wa basi ni kama wamekata tamaa yaani hawana mwamko na kazi yao, wanaongea lugha mbaya kwa abiria, badala yake muda wote wa safari walikuwa wamekaa tu kule mbele wanapiga story pasipo kusikiliza abiria pia bus lilikua linavuja.
Kwa kweli Kilimanjaro express niliyoipanda miaka mitano huko nyuma ina tofauti kubwa sana na hii ya leo. Wakati narudi Dar nikasema ngoja nijaribu kupanda BM coach, kwa kweli nimeinjoy sana kusafiri na BM, huduma nzuri sana na wahudumu wao wakarimu mno.
Kilimanjaro express msipobadilika na kufanyia kazi hizi kero za wateja wenu basi naweza kusema huu ndiyo mwisho wa zama zenu.
View attachment 2285942View attachment 2285943
Kwanini wasi-kunyer mkuu na misosi wanakula??Kwani wanawake wanakunyer?
Nipo Tanga Joto SanaUna uhakika? Maana nimetoka Dar J3 na kuna baridi Dom tunalala na maduveti
Zisipokuwepo leo unaamini Oct zitakuwepo?Mkuu unataka AC kweli kipindi hiki😄😄
Mtoa hoja kwanza unazungumzia Kilimanjaro Bus ipi? Moja ya kampuni smbazo zinaongoza na ndio mfumo wake unaigwa na Kampuni zote za Ma Bus ni Kilimanjaro Truck. Huduma zake ni za Uhakika, Hawana historia ya kujaza abiria, kuacha Abiria wala kutoa huduma tofauti na abiria sliyoahidiwa.
Katika hoja yako unasema juu ya Uchakavu wa Ma bus huku ukiwa umeonesha Tiketi badala ya kutuonesha picha halisi ya Unachozungumzia. Sehemu ambayo umejichanganya zaidi ni kuanza kutaja kampuni ya gari ambayo imekutuma kuchafua Kilimanjaro Bus, Hizi propaganda zako haziwezi kuondoa imani ya Wateja wa hii kampuni. Tumekua tukipanda haya mabus sababu ya huduma nzuri na za uhakika, utu na ubinadamu wao pindi inapotokea Abiria umechelewa bus hawana longolongo wanakupakia kwenye bus jingine.
Nauli zao hazipandi na kushuka kama hizo za mabasi mengine za msimu. Hayo mabasi unayataja Unaweza jikuta kwenye bus kils mmoja kachajiwa nauli yake.
ACHA MANENO MENGI KILIMANJARO BUS ITABAKI KUWA BABA WA NJIA.View attachment 2287844
Sent from my SM-G980F using JamiiForums mobile app
Nimefika huku nasoma comments😀