Bro uko sahihi kabisa, yaani tangu yule Mama aliyekuwa Mkurugenzi afariki huduma za KLM Express zimedorora hata Bus unaloambiwa ni luxury halina hadhi kabisa, mimi mwenyewe yalinikuta kama wewe nilitoka Dar - Arusha kwa kweli niliona huduma ziko tofauti na KLM Express niliyokuwa nasafiri nayo miaka ya nyuma, na tulikariri hakuna zaidi ya KLM Express, lakini hivi karibuni totally mambo yamebadilika Mabasi yamechoka mno, ilibidi wakati narejea Dar nisafiri na EXTRA luxury coach at list lilikuwa linakidhi. Uongozi wa KLM Express ufanyie kazi malalamiko ya wateja na waboreshe huduma zao kama mwanzo naamini watarudi kwani sasa hivi biashara ni ubunifu na ushindani.