kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Wachambuzi wetu ni low profile, tuwasaidie kuwaandalia ajenda. Mayelle aliletwa Yanga na viongozi wa Yanga, kabla ya kuletwa Yanga alikuwa hatambuliki na wachambuzi wetu. Mayelle alikuwa na kipaji kilichonolewa na Nabi sawa na Fei Toto na wachezaji wengine pale Yanga ambao kabla ya kuja Yanga na kukutana na Nabi walikuwa na vipaji ambavyo havikuendelezwa.
Wachambuzi wetu wanajenga hoja kwamba Mayelle hakutakiwa kuondoka Yanga milele, Yanga bila Mayelle imekwisha na pengo la Mayelle haliwezi kuzibwa na waliopo sasa na waliosajiliwa. Kuwaza kwa namna hii kunaturudisha nyuma; yaani ligi yetu na mpira wetu unazidi kukua lakini waandishi na wachambuzi wa mpira ama wako vilevile au wanarudi nyuma.
Mayelle ni mchezaji bora kabisa kutokea tangu tanzania hii kuumbwa; na ubora wake ukom pale alipoweza kuwa mfungaji bora wa mashindano ya CAF rekodi ambayo haijafikiwa na mchezaji yeyoyote yule Tanzania. Hata hivyo unapomsifu mkiambiaji lazima umsifu zaidi yule anaemkimbiza. Mayelle alikuja Yanga akitokea ligi ya DR Congo lakini hakuwika kama alivyowika Yanga, hii inaonyesha kuwa sifa ya kwanza lazima iende kwa Eng. Hersi na uongozi wake, GSM, benchi la ufundi, wachezaji wezake na mashabiki wa yanga waliokuwa wako nyuma yake.
Kama Eng. Hersi na wenzake, bench la ufundi, wachezaji na mashabiki bado wako yanga, nina imani kuwa pengo la mayelle litazibwa na hata mayelle anaweza kuomba kurudi tena yanga bila kupata nafasi kwakuwa nafasi imejaa.
Wakati ligi yetu inaongezeka thamani hata wachambuzi wetu wasibaki palepale na vilevile.