Zama zetu kali. Unakijua hiko kidubwasha wewee!?

Tulipenda mpira wa visoda, mimi niliipenda sana brazil enzi hizo za kina rivaldo, dunga na 8, ronaldo na 9, na wengine. Kila kisoda kilipewa namba yake.

Pia tulibandika picha za jojo za wachezaji kwenye madaftari. Tulishindana kujaza wachezaji bora hasa wale wa brazil
 
Mimi siyo wa 95 ni wa 98
 

Hii mwakabunguja ni kwa watu wa Mbeya nafikiri.
 
Yani nikiwa na hiki naweza kimbia km 25 bila kuchoka
 
Hapo unatakiwa ukimbie kuzidi motokaa ili mambo yawe mswano.Utoto raha sana![emoji13][emoji13][emoji13]
Ukirudi jioni yanaonekana meno na macho tu...halafu kuna jiwe,dodoki la kisalufeti na maji ya baridi yamo kwenye karai sasa kama kwenu ndo makambako utafurahi suala la kuoga lilifanana na kuchoma sindano
 
Umenikumbusha njumu zangu za Romalio...ndo kilikuwa kiatu changu pendwa S/M Masebe
 
Hahaa umesahau kupiga baruti tulikua tunatumia spoko za baiskeli halafu kule kwenye tundu unajaza ule unga wa njiti ya kiberiti
Sisi tulitumia plugs zilizokufa na bolt. Tunaenda garage huko kusaka
 
Ukirudi jioni yanaonekana meno na macho tu...halafu kuna jiwe,dodoki la kisalufeti na maji ya baridi yamo kwenye karai sasa kama kwenu ndo makambako utafurahi suala la kuoga lilifanana na kuchoma sindano
Makambako kule Kitisi?😂😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…