Zamani ilikua hatuwezi kutengeneza hii....sasa sijui kama wakati huu wa viwanda tunaweza tengeneza hii kitu.

Zamani ilikua hatuwezi kutengeneza hii....sasa sijui kama wakati huu wa viwanda tunaweza tengeneza hii kitu.

Antennah

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2015
Posts
6,754
Reaction score
8,750
Hii tulikua tunaiita hvo hivo kama ilivoandikwa ""sport"". yani ni wanafunzi wachache sana walikua wanarudi nyumbani bila huo mfuko kuwa na mafuta ya maandazi na bagia.

Sisi wanaume ndo ilikua mtu anaona bora daftari ashike mkononi lkn humo ndani mpira lazma ukae.

Sasa kuna wale walokua wanajifanya wana matilio na mavitabu mengi ya darasa la tano la sita au la saba unakuta mpaka hcho kimfuko kinatamani kiseme kuwa kimetingwa ila ndo hvo.

SASA BHANA KUMBE VILIKUA VINATOKA CHINA HUKO VINAKUJA KWA MELI KABISA........
Screenshot_20180416-175354.jpg
 
Ni kweli siasa zimechachamaa lakini hii ni kuidhalilisha nchi yetu. Zile cherehani nne unafikiri zinashindwa kutengeneza hiyo kitu?
yani hyo huko china inatengenezwa na watoto wa std 4
 
Namuomba mkulu akazindue kiwanda cha mama kijijini,amefungua kiwanda cha pombe aina ya flasher,ni mixer komoni na ile nyingine inayopigwa vita aka chingili...ni nzuri sana kwakweli.
 
Daah! Umenikumbusha mbali,

Nakumbuka vilikuwa vinauzwa mia tano, ila nikawa naogopa kumwambia Bi mkubwa aninunulie na mimi nikatambe,

Kwa kuwa mwenyewe ninaubunifu nikanunua mfuko wa Nailoni ile migumu yenye mistari myekundu na myeupe, nikakata juu kuondoa ile sehemu ya kushikia kisha nikachukua sindano na uzi nikapiga Pindo,

Baada ya hapo nikafumua kiroba nikachukua zile kamba zake kisha nikasokota,

Nikapitisha kwenye lile pindo kisha nikatoboa kwa chini then nikafunga,kwa hiyo ikawa ukivuta zile kamba palle juu panafunga kama ile ya kichina

Sasa na mimi nikawa na Sport Made by mi mwenyewe kufika shule nikafunika vibaya sana, yaani shule nzima nikawa na Sport ya kipekee,

Mvua ikinyesha sasa, mi sina wasi wasi na madaftari kuloa napuyanga kama kawa, wao wenye Visport vyao vya kununua ikawa wanasubiri mvua ikatike,

Bi mkubwa mwenyewe alinipigia saluti,
Akaniambia tu, huo ukiisha ntakununulia Bag, mi sikuwa na mpango wa Bag, ukiisha natengeneza mwingine

Daah! Yaani nilikuwa mbunifu kweli kweli
 
Dah!umenikumbusha mbali mkuu,nilikuwa nacho kimfuko cha hivyo chekundu[emoji23]

Watoto wa geti kali utawajua tu. Yaani enzi hizo sie bazoka ikitemwa unaiokota unapangusa mchanga unaendeleza ku show game. Nyie tayari mlikua mnamiliki vitu vya anasa kiasi hicho?

Kwanza kijijini ndani ndani huko ukiokoteza mahindibaada ya watu kuvuna ndio unaenda kununua kandambili za bora, unazivaa jumapili tu, ukirudi unazisuuza unazisunda uvunguniiii zisije kuibiwa hapo ni hadi okesheni nyingine.
 
Back
Top Bottom