Daah! Umenikumbusha mbali,
Nakumbuka vilikuwa vinauzwa mia tano, ila nikawa naogopa kumwambia Bi mkubwa aninunulie na mimi nikatambe,
Kwa kuwa mwenyewe ninaubunifu nikanunua mfuko wa Nailoni ile migumu yenye mistari myekundu na myeupe, nikakata juu kuondoa ile sehemu ya kushikia kisha nikachukua sindano na uzi nikapiga Pindo,
Baada ya hapo nikafumua kiroba nikachukua zile kamba zake kisha nikasokota,
Nikapitisha kwenye lile pindo kisha nikatoboa kwa chini then nikafunga,kwa hiyo ikawa ukivuta zile kamba palle juu panafunga kama ile ya kichina
Sasa na mimi nikawa na Sport Made by mi mwenyewe kufika shule nikafunika vibaya sana, yaani shule nzima nikawa na Sport ya kipekee,
Mvua ikinyesha sasa, mi sina wasi wasi na madaftari kuloa napuyanga kama kawa, wao wenye Visport vyao vya kununua ikawa wanasubiri mvua ikatike,
Bi mkubwa mwenyewe alinipigia saluti,
Akaniambia tu, huo ukiisha ntakununulia Bag, mi sikuwa na mpango wa Bag, ukiisha natengeneza mwingine
Daah! Yaani nilikuwa mbunifu kweli kweli