Zamani ilikua hatuwezi kutengeneza hii....sasa sijui kama wakati huu wa viwanda tunaweza tengeneza hii kitu.

Swahiba wewe najua mboga saba mtoto wa mjini haya mambo ya vibegi vya kichina ulikua unabadili unavyotaka mwenyewe.

Sie lazima uvizie suruali chakavu ukate miguu ndio ushone mfuko wa madaftari, kiwanda kingine cha kushona hicho...
Hapana mimi enzi zangu hivyo vibegi vya kichina vilikuwa havijazaliwa...
 
Sie ndio ilikua zetu mkubwa. Tena home wakikaa vibaya unawachenjua unapiga makopo kadhaa ya mahindi unachanganya na yako unaingia black market unauza unasunda mpunga kibindoni...I miss those days
Ila maisha ni safari ndefu sana mkuu yani mm maisha ya bata yalinishindaga utanikuta nachunga mbuzi za watu, naenda gombania ukoko wa ugali na viporo Kwa majirani wakati home mfanyakazi kashaanda chakula ila nikiziweka now day natamani bata sema ndo majukumu yashaniandama
 
bila shaka unatakiwa upatiwe milioni 100 [emoji23][emoji23]
 

Dah. Sisi hayo ndio yalikua maisha ya kawaida kabisa. Siku likipikwa beche hauchezi mbali. Lilikua linaitwa cheka na watoto. Kama kwenu kidogo mambo safi unalibahatisha krismas
 
[emoji23][emoji23][emoji23] watu mmetoka mbali kweli kweli. Mimi nakumbuka nilikua narafiki yangu anapita upande wa kushoto wa barabara mimi napita kulia tunaokota vifungashio vya biskuti tunakula zile chenga za biskuti zinazobaki
 
Hivi hii mipira ya kiume inatengenezwa hapa kwetu kweli ama tunaagiza kwa kontena? Nawaza tu just in case maana sikuwahi kuisoma made in wapi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…