Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Ishi na ndugu zako vizuri lakini wema usizidi uwezo,acha kuwasiliana na ndugu Mara kwa Mara kila aishi maisha yake.

Ukipigiwa simu za kupigwa mizinga na wewe tangaza njaa ya kufa leo au kesho yaani waambie una madeni kila kona kuanzia Bank mpaka kwa watu binafsi.

Hakuna haja ya kugombana na ndugu zako yaani mkikutana mnapiga story fresh mkianacha kila mtu na maisha yake.
 
Mimi kama ndugu Mtanzania acha niwawakilishe ndugu wenzangu wote wa Tanzania hii tunaosemwa na watu wasio ndugu.
 
Tatizo la watu wanaosaidia wanataka gratification. Hapo ndipo mateso yenu yanapoanzia...

Ukimsaidia mtu huwekezi, ukimsaidia mtu ni Wema ambao kanuni yake ni kwenda zako.

Jitahidini kuishi kwa kanuni na mnapotaka kuzivunja kanuni hakikisheni mmezielewa kwanza.
Unaongea kitu usichokifahamu mkuu
 
Pesa ya kutoa kwa ndugu peleka benki. Ikifika mwisho wa mwaka jipongeze kwa kiwanja, kumalizia nyumba ama gari.
NB: Hakikisha 95% ya pesa yako unaila wewe na familia yako (Mwenza , watoto na wazazi) ibaki 5% ya ndugu humo iwepo Michango ya harusi na misiba. Utaenjoy maisha Sana. Hapa nimeagiza vitz Clavia ya wife kwa kubana Michango ya ndugu. Sijachanga mchango wa harusi wa ndugu wala rafiki takribani mwaka wa 6 huu kila nikiletewa kadi ya mchango narusha huo mchango kwenye akaunti yangu NMB
 
Daaaahh!! sasa sie masikini tukasaidiwe wapi kama mnatutenga namna hii!!?
Umaskini wa kujitakia. Nimezaliwa kwetu Maskini nimekuja town kwa kuunga, nimeendesha bodaboda, kukaanga chips huku nasoma QT Sasa Nina degree 2. Japo sijaacha biashara ya chips. Ndugu kama wote, nawatolea mbavuni
 
Nilichojifunza kwa Tanzania hii ukijifanya mwema unatoa misaada inajiingiza kwenye matatizo na chuki maana wengine unawasaidia kiroho Safi kumbe wanachukia, wengine wanaenda hata kukuloga ili uangamie, maana kutoa msaada wanaona unaringa,ni Bora wakukomeshe ili mkose wote wakucheke. Dunia hii Bora kuwa na roho mbaya, kwanza watu watakuogopa sana

Uko sahihi [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Mawazo ya kimaskini haya. Kama wafungwa wasio na ndugu wanazikwa, sembuse mimi ambaye sio mfungwa? BTW wewe ukishakufa hata yanayoendelea huyajui, why ukae unaworry eti nikifa nani atanizika!! Stupid

Absolutely you are right
 
Pesa ya kutoa kwa ndugu peleka benki. Ikifika mwisho wa mwaka jipongeze kwa kiwanja, kumalizia nyumba ama gari.
NB: Hakikisha 95% ya pesa yako unaila wewe na familia yako (Mwenza , watoto na wazazi) ibaki 5% ya ndugu humo iwepo Michango ya harusi na misiba. Utaenjoy maisha Sana. Hapa nimeagiza vitz Clavia ya wife kwa kubana Michango ya ndugu
Hakika mkuu
 
Usirudie kuwasaidia

Maana hutapungukiwa kitu
Kuendelea kuwasaidia kutajeenga jamii isiyojifunza
Kabisa mkuu mi mshua alikufa ndo nipo seven then nikamaliza shule nikafail kuingia sekondari nakumbuka kulikuwa na msiba wa bibi yangu mzaa baba sasa kwenye vikundi vyake wakawa wametoa rambi rambi kama milioni tatu huwezi amini nilipoomba kupelekwa shule baba yangu mkubwa alinambia siwezi kusoma mi mi muhuni nililia sana akatokea mdhamini rafiki yake na baba akanipeleka shule nilisoma kwa hasira nyingi na kufika chuo saivi wanabaki wanaona aibu tu na wote waliokuwa na pesa wamefirisika watoto wao hawaishi kunipiga vizinga kuna time mpaka nasema sijui nisiwasaidie ila naona wao hawana makosa
 
Wengi munaochukia ndugu inaonekana mumetokea familia za shida na mumekulia maisha ya njaa sana,..... Kiukweli kama baba yako mdogo, wajomba, shangazi, bibi babu wapo vizuri, wao na watoto wao..... Kuna shida gani, mi naona fahali tu kusaidia mtu yeyote aliye na shida duniani
Hayajakupata
 
Muda mwingine kutumia hekima kwenye changamoto hizi za kifamilia ni kujimaliza mwenyewe, unaonesha upendo kwa watu ambao wao hawana upendo na wewe. Wanakuchekea kinafiki ukiwapa msaada, wakitoka wanapanga mipango ya kukudhuru na kukuombea uharibikiwe.

Binadamu wana Roho mbaya sana, hata Yesu hakuwa na kosa lakini walimsulubu msalabani japo aliwapa chakula wakiwa hoi na njaa walivokula na kushiba wakaanza kumtesa. Wanaonesha kukupenda lakini mioyo yao imejawa chuki. Naandika haya nikiwa na Jazba siku kadhaa zilizopita ningekuwa niko karibu na viumbe hawa waliofanya niandike hapa basi leo maiti kadhaa zingekuwa mochwari au zishazikwa na mimi ningekuwa nyuma ya nondo.

Ndugu zangu kwa sasa ni ndugu wa damu tu wadogo zangu na mama zangu. Hawa wanaojiita ndugu za baba huu ushenzi wanaoniletea kwenye familia yangu na mimi binafsi pamoja na kujishusha sana kwao Imefika mahali imetosha, naona ni kama nakumbatia kundi la wachawi huku nikijifanya nawapenda. Huku wao wakiwa na mipango yao binafsi.

Nimesaidia sana kifedha na kila aina ya msaada lakini hawa watu nia yao sio njema Lakini majibu niliyowapa nadhani washanifahamu kwamba mimi sasa ni mtu wa namna gani, siwezi kukumbatia nyoka tena.

Nilipofikia ukinipiga kofi, nakurushia bomu huu upuuzi wa kumuachia Mungu aamue sina tena. Tutajibu dhambi zetu tukiwa kwenye kiti cha enzi.
Ukitaka kuwajua ubaya wao vizuri ngoja siku uchache ndio utajua misaada yako haikuwa na maana kwao...
 
Nilichojifunza kwa Tanzania hii ukijifanya mwema unatoa misaada inajiingiza kwenye matatizo na chuki maana wengine unawasaidia kiroho Safi kumbe wanachukia, wengine wanaenda hata kukuloga ili uangamie, maana kutoa msaada wanaona unaringa,ni Bora wakukomeshe ili mkose wote wakucheke. Dunia hii Bora kuwa na roho mbaya, kwanza watu watakuogopa sana
Sahihi
 
Back
Top Bottom