Zamani nilikuwa nikihisi kuwapa vijana nyadhifa za juu kutasukuma maendeleo kwa kasi, kumbe nilijidanganya

Zamani nilikuwa nikihisi kuwapa vijana nyadhifa za juu kutasukuma maendeleo kwa kasi, kumbe nilijidanganya

Bahati mbaya vijana wanaopewa vyeo ni wale waliokulia maisha ya dhiki mno !
Hypothesis yako ni fyongo. Mbowe hakukulia maisha ya dhiki, lakini mbona hajaisaidia chadema kujenga angalau hata kaofisi kadogo ka makao makuu; angalau hata kuwa na kiwanja tu?
 
Enzi zile nilikua napenda nione vijana wanawekwa kwenye vyeo vya ukuu wa wilaya/mkoa ana hata uwaziri, nilikua nikiamini vijana watasaidia pakubwa kusukuma maendeleo haraka nikipenda wazee wapishe vijana kwenue hizo nafasi..
Dhambi ya kuiba kura haitawaacha salama.
 
Viongozi vijana hawajaanza awamu hii, Toka uhuru nchi yetu iliongozwa na vijana. Nyerere mwenyewe alikuwa kijana alikuwa Rais akiwa na miaka 30 na kitu, angalia akina Msekwa wakati huo. Akina Kikwete wote walikuwa vijana walipo shika nyazifa mbali mbali. Kikubwa tujiulize kuna tofauti ipi vijana wa zamani na sasa? Vijana wa sasa wanaonesha kushindwa kuliko vijana wa zamani.
 
Back
Top Bottom