Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Nilivyokuwa mdogo nilisimuliwa kuwa gari aina ya range rover ikikimbia sana inapaa kama ndege

Kweli kaka tuliaminishwa kabisa kuwa eti hizo zimepigwa marufuku kabisa kupaki benki kwa sababu zinakimbia sana mpk zinapaa, i real love those days.
 

mkuu utakua unatokea pande za chadema a.k.a kilimanjaro.
 
mimi yaliletwa mafuta ya kupaka kopo jipya,nikawa nataka nilichezee lile kopo nilivyo maliza kuoga nikajipaka mafuta kopo lote.home walishangaa kinoma natoka na kopo wakaniuliza unapeleka wapi mafuta nikawaambia yameisha walivyo nitazama ninavyong'aa hawakuuliza tena walinicheka sana!
 
Nilipokuwa mdogo niliamini ukila chungwa na ukameza mbegu zake lazima zitaota tumboni,na we utakufa
 
Aaah!utotoni bwana kuoga ilikuwa issue,na mazingira ya nyumani mbeya basi unachua maji mengi unaingia bafuni,unanawa miigu na kujipaka maji uson na mikononi unachelea kama dk kumi hib huku unaua chezea maji,ukitoka unaingia ndan huku unatetameka kweli,cku moja mama aligundua hako kamchezo,fimbo nilizo chapwa nilijuta

Sent from my BlackBerry 9780{katefar}
 
tulikuwa na mchezo wa kulamba sukari kuna siku nliwategeshea mbokea ya s.a wacha wachubuke midomo nlichapwa sana pale songea angoni amsi
 
nlkua nadhan watoto wachanga wananunuliwa hosptal, mwanamke mja mzto et n kwamba amevmbiwa. Loh, ukila mbegu za ma2nda mti utaota kchwan. Hahah, n ujnga ujnga ujnga
Ilisaidia sana kuowahi kufanya mambo ya ngono mapema, kama ilivyo sasa watoto wanafahamu mimba.ns hsts ukisikia mtu anakuita mchumba wala mlikuwa hamfanyi chochote cha ngono, lakini miaka hii mtoto anazaa mtoto.
 
Mi nilikuwa nikimuona mtu alievaa miwani alafu anakipara basi najua ni daktari pia tajiri wakutupa
Hahahahahaahaaaaaaaaaaaa! Loh! Nami ningenyoa na kuvaa miwani ili niwe tajiri . umenifanya nicheke sana.
 
Mie wakati ndio naingia mjini..nilifikiri City Bus ni magari ya mtu mmoja bas nikawa najiuliza huyu citybus ni tajri kiasi gani maana magari yooote haya ni yake...
 
Nilipokuwa nikisikia radi najua Mungu anapanga mapipa ya mvua ili ije inyeshe
 
mimi nilikuwa nafikiri tanesko
**** mswichi mkubwa unabonyezwa na watu wanne,ambao hutumika
kukatia umeme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…