Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Habari zenu wandugu?? Leo embu tukumbushane mambo ya zamani ambayo ulikua unatumia akili za kitoto ktk kufikiri. Basi bhana mimi zamani nilivyokua mjinga nlikua najua ukizima RADIO kama ilikua ni taarifa ya habari au matangazo ya vifo, ukija kuwasha baadae kitaendelea kilichokua kinatangazwa kabla hujaizima radio. Nlikua mjinga eh? Embu na wewe tupe kaujinga kako kazamani...

Mimi nilivyokuwa mdogo niliaminishwa kuwa wanaokula filigisi ni wakubwa peke yao tena wanaume, watoto wakila watakufa,mwanangu wa kike alikula mwaka juzi hadi leo hajafa.
 
Mi nilikuwa naambiwa mtoto akiwa mchanga yale maneno anayoongea Akiwa anajifunza kuongea(yale uasioeleweka)ni kiingereza.yani nilipoenda shule nilitangaza kwa wenzangu mtoto wetu anaongea kiingereza.basi muda wa kutoka shuleni nikawakusanya kwenda nao home wakajionee wenyewe.
 
Mimi kwa kweli kipindi nikiwa mdogo nikipelekwa sinema nilikuwa najua wanacheza sinema wamo humo nyuma ya pazia. Basi Amitabh Bachan akipigwa risasi nilikuwa nalia!!
 
Kingine kipindi kile RTD mtangazaji akiweka mziki anamwambia fundi mitambo. Basi mimi nilidhani wanamuziki wote wamo humo ndani wanabadilishana tu muda wa kupiga mziki.
 
Nilikuwa mjinga mana wale wadada waliokuwa wanajiachia na vichupi vyao hata sikuwa na tym nao.....yan niliishi na vigoli wala moyo haukushtuka naishi na vitamu.....balaaaa nilijuaga mvua ikinyesha na jua linawaka et simba anazaa....nkajua albino hawafi....nkajuaga et Jamiiforum nikama fb wacha nipewe zachembe...
 
hahahahahahahahaaaa...!
umenikumbusha shuleni.
nilikua mdogo kuliko wote darasani ila nilikua mtundu sana. akili pia hazikua haba saaaana.
siku moja niko dawati la nyuma kabisa mwalim wa kiswaz anaendelea kufundisha me na mwanangu GP (RIP) tUnapiga
story. mara tcha akanistukiza....."tasi...mapenzi ni nini?" sasa mie kwa kukumbuka maneno ya mtaani mara mapenzi kidonda, mara mapenzi kikohozi, mara mapenzi nika uginjwa hayafichiki.....nikajibu "mapenzi ni kizunguzungu"
darsa looote kicheko......maskini mwalimu machungwa wala hakunichapa nae akashangaatu.
Mkuu tasia1 ni wwe yule wa mtendeni ps au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom