Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Zamani nilivyokuwa Mjinga!

me nazani now ndo mjinga kuliko zamani, me nilikua natisha enzi za utoto
 
Habari zenu wandugu?? Leo embu tukumbushane mambo ya zamani ambayo ulikua unatumia akili za kitoto ktk kufikiri. Basi bhana mimi zamani nilivyokua mjinga nlikua najua ukizima RADIO kama ilikua ni taarifa ya habari au matangazo ya vifo, ukija kuwasha baadae kitaendelea kilichokua kinatangazwa kabla hujaizima radio. Nlikua mjinga eh? Embu na wewe tupe kaujinga kako kazamani...
ule ulikua utoto na si ujinga.ila ulichoandika hapa ndo ujinga.,teh teh tehee!
 
Mie zamani nilipokuwa katoto nilikuwa nikisikia kuwa yule binti ni bikira nilidhani yule binti huwa na kabirika kazuri ka kuwanawisha watu wanapotaka kula ugali. Sasa naelewa kidogo ingawa hadi sasa sijaona hizo bikira, jee wewe?
 
Ule mchezo wa kukaa barabarani then kila gari linalopita mnashindana kwa kusema hili langu nyie hamjaupitia? Mimi nilikuwa naibuka kidedea kila siku! Amakweli utoto mzigo!

Mwisho Wa huu mchezo nilijikuta nimechagua magari yenye plate number SU na mwenzangu akachagua SM. baadae nikajikuta SM zilikua nyingi kwa wakati ule basi nikawa bored saaana!
 
Mi nilifuata upinde wa mvua(rainbow) na wenzangu tukitaka kujua umetua wapi, ukiwa mbali unaona umeishia sehemu fulani,lakini ukuifika wapi. Tuligonga km kadhaa mazee,tulipochoka tukarudi home.
 
mii nilikua nikipita pale posta si kuna makatuni wamevalishwa suti wanapouza nguo kule basi nilikua nawashangaa halafu nawamkia
 
Mwisho Wa huu mchezo nilijikuta nimechagua magari yenye plate number SU na mwenzangu akachagua SM. baadae nikajikuta SM zilikua nyingi kwa wakati ule basi nikawa bored saaana!

Mm nilikuwa nachagua magari yote yenye matairi meusi! So nikajikuta magari karibu yote ni yangu.
 
Back
Top Bottom