Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Zamani nilivyokuwa Mjinga!

nilikuwa naamini ukioga maji ya MOTO baada ya Ku'DU' huwezi kupata ukimwi
 
Neno kufunga shule lilinitatza saana!! Nakumbuka npo STD one 2po xul baraza mkuu akatangaza "shule itafungwa leo na afunguliwa 11/january". Baada y kuruhusiwa Nilibana sehemu kuona kufuli ya xul na nan itafunga
 
Nilikuwa na amin masomo ya 'sunday school ombeni nanyi mtapewa' basi kunasiku nilipoteza hela hom nikajifungia rum nkaweka kikopo kumwomba Mungu anirudishie aziweke humo bt kila nikifungua kikopo hola!
 
sitakaa nisahau enzi hizo utoto akili yote ilijaa mapicha/movie, kwenye pepa moja kulikua na maswali ya kuandika kinyume mf, nene-nyembamba, kuna swali tukaambiwa kinyume cha adui nikajibu stelingi.

Kuna dogo class kwenye hili swali la kinyume alijaza kama hivi:-

1. Njaa = anja
2. Kulia = aliku
3. ...

Alipata 0 kati ya ishirini, basi ticha akatusomea majibu yake darasa zima tulicheka!!
 
kipindi kile naanza primary school nilikuwa naona shule ni kama sehemu ya kupewa adhabu tu, basi nikawa naogopa sana na nikawa naomba nisishinde kuendelea na hatua nyingine, mawazo haya yalianza kupotea baada ya kufika darasa la sita
 
Mi nilipoambiwa kuwa mwanaume ndiye anaetoa mayai nilidhani staweza kuzaa maana niliona sina uwezo wa kutoa yai maana nilijua tunatoa mayai kama ya kuku

mmh we mjinga mpaka leo.,mwanaume hatoi mayai bali mwanamke ndo anayetoa mayai
 
Nilikuwa najua ukifa Tz unazaliwa Ulaya.,ndo mana watu wengi wakichukizwa walikuwa wanajiua.,
 
nakumbuka kila nikipewa dawa kumeza naibana chini ya ulimi na baadaye kuitema, kimbembe ni pale dawa inapokua chungu ka chloroquin
 
Dah!nakumbuka niliimwagia maji radio ya mdingi,aliponiuliza nikamjibu hawa watu hawajaoga muda mrefu!teh teh
 
mi nilikuwa napenda komborera ili kademu fulani nikagonge. Nilikuwa najinoma kweli. Hivi nao ulikuwa ujinga eti eeh?

Dah!umenikumbusha mbali kinoma,nilikua navibamiza kinoma,chezea kombolela wewe!
 
Mimi nilikuwa najiuliza umeme umekatika mbona magari taa zinawaka? ha ha ha

mi nilikuwa nikijiuliza zaidi mbona magari yanawaka taa na sioni waya zilizotoka kwenye nguzo na kuunganishwa kwenye hayo magari?
 
ha ha ha ha nilipokuwa mtoto kuna shangazi yangu alikuwa nesi huko kijijini sasa kaja kwenye hospt ya wilaya anaporudi kijijini kapewa mikondom kibao kafika nayo home nikaanza kuyalilia mapulizio wakaniambia yana dawa mpka yaoshwe nikaiba kama kumi hivi, si nikaenda mitaani kuwalingishia watoto wenzangu wacha tuyapulize duh tunasema haya ya kizungu hayapasuki watu wazima wache watuulize na kushangaa kila mtu na condoma mdomoni kufurahia nikapelekwa home, mama alinichapa nilikoma namshukuru mungu alinifichia siri kwa mdingi maana anganiua kipindi hicho. nilikuwa mjinga sana
 
nilikuwa nadhan watoto wa kizungu wanaakili sana, wanaongea kingereza wakiwa wadogo vile jamani!
 
Kuna dogo class kwenye hili swali la kinyume alijaza kama hivi:-

1. Njaa = anja
2. Kulia = aliku
3. ...


Alipata 0 kati ya ishirini, basi ticha akatusomea majibu yake darasa zima tulicheka!!

katika wajinga huyu ndo mjinga tena nambari wahedi!
 
Mimi nilidhani viatu ni rasmi kwa kanisani tu. Kumbe wazazi walikuwa wanabana matumizi
 
Nyie wote mlikua na akili, mimi sasa, kipindi tunacheza KUJIPIKILISHA, kipindi icho baba (acting) kaenda kuwinda ndege na manati akalenga njiwa si nikajidai kumnyonyoa Njiwa kama mama anavyonyonyoa kuku kwa maji ya moto?? Wallah ilibidi tumpepee ili apoe na kukauka ndo anyonyoke manyoya!!
 
Back
Top Bottom