Umeongea point sana Mkuu, wengi wanakimbilia Kusema wamekusomesha, wamekulea n.k kama lugha ya kutetea uzembe walioufanya kwa kuendekeza starehe na maisha ya kutaka sifa.
Kulea, kulisha, kusomesha n.k. Ni majukumu ya msingi na ya lazima kwa mzazi kwa uzao wake, haiwezekani mimi leo nibweteke nisijiwekeze kwa maisha yangu ya baadaye ili nije kuwa mzigo kwa watoto wangu eti nilitumia muda wangu kuwalea na kuwasomesha.
Ndiyo maana umasikini hauishi kwenye familia nyingi unakuta kijana ameanza kazi badala aanze kujiwekeza kwa maendeleo yake binafsi unakuta kuna lundo la ndugu na mzigo wa wazazi waliouchezea ujana wao wanataka wagawane kamshahara hako kiduchu kwa mtu anayeanza maisha.
Kijana pambana kujijenga na punguza starehe zisizo na msingi ili usiwe mzigo kwa uzao wako na kuwaongezea majukumu ambayo ulitakiwa uyafanye ukiwa na nguvu badala yake uje kuwatishia watoto kuwa utawapa laana kwa ulofa wako.