Sio kwa povu hili! We jamaa mbona hii issue umeikomalia sana?! Ni WAPI Zamaradi amesema hii filamu ametengeneza yeye kwa Sh. 200M? Binafsi, nimemsikiliza Zamaradi hapa:-
Na ukimsikiliza kuanzia Dakika 1:10, Zamaradi amesema wazi kwamba HII NI FILAMU YA NJE ambayo IMESHIRIKISHA waigizaji kutoka Tanzania!! Sasa ikiwa mtu ameshasema ni Filamu ya Nje, how come tena aseme ni ya kwake?! Na amewataja hadi Directors na ma-producer wa filamu husika, huku yeye akijitaja kama MHUSIKA MKUU kwa Tanzania!
Kuanzia Dakika ya 07:53, kuna Mwandishi amemuuliza anamaanisha nini anaposema yeye ndie MUHUSIKA MKUU! Na akahoji ikiwa alimaanisha ni kazi yake mwenyewe,aliinua, au nini alimaanisha nini hasa!!! Ukisikiliza jibu la Zamaradi kwenye hilo swali, ameanza kwa kusema: "Kama nilivyosema, Producer kabisa wa hii filamu yupo Australia, ambae anafahamika kwa jina la John Kay. Huyu ndie Producer na ndie amecheza pia...." Kisha akaendelea: "
Lakini kwa hapa Tanzania, mimi ndie Mhusika Mkuu katika maana ya kuisimamia kimauzo, ki-promosheni na kwenye kila kitu. Kwahiyo hata kwa Distributors wote, au mtu yeyote ambae anataka chochote na hii filamu, Mwongeaji mkubwa ni mimi. Kwahiyo (mimi) ni kama sehemu ya hiyo filamu, katika namna kubwa, kwa maana kwa hapa Tanzania ndo nimepewa jukumu hilo"
Haya ndugu yangu, kama unavyoona hiyo clip, hicho hiyo ilikuwa ndio Press Conference ya Zamaradi!!! Sasa wewe hilo unaloshupalia kwamba kasema filamu ni yake umelitoa kwenye press conference ipi? Hivi we jamaa mbona unapenda sana kuongea vitu in negative way?!
Halafu ndugu yangu unaonekana mweupe kwenye hii tasnia!! Filamu inaweza kuwa na Release Dates zaidi ya 10 kutegemeana na wapi inakuwa released! Kwahiyo, kama ilikuwa released mwaka 2017, ulitakiwa kufahamu ni wapi ilikuwa released na hiyo release date ya Zamaradi ulitakiwa kufahamu ni release kwa nchi gani!!!
Hayo mambo ya cover kuwepo akina Wema Sepetu ni commercial strategies tu! Kwavile filamu imehusisha waigizaji kutoka Australia, Tanzania na West Africa basi wala usishangae cover za West Africa zikang'arishwa na Waigizaji wa huko hata kama wamecheza sekunde moja!!!!
Yaani ulivyoongea kwa lugha kali na ya kuudhi kwa wale walioamini alichoongea Zamaradi, ajabu inaonekana hayo maneno ya hovyo yanakuhusu wewe mwenyewe!!!!