Zamaradi amewaza nini kumhoji Gigy Money?

Zamaradi amewaza nini kumhoji Gigy Money?

Zamaradi awajibu nyie instagram

from @zamaradimketema - Ukiwa ni mtu wa social medias ndio utagundua jamii yetu ina matatizo MAKUBWA kiasi gani, kizazi cha sasa ni cha hatari, kuna aina ya watu ambao huwezi kufikiria kama wapo, watu wanaoonekana kama wamepinda kupitiliza, wasiojali chochote tena kwenye maisha yao na wanaoweza kufanya jambo na wakakuachia maswali mengi mno, ni kama wamejitoa sadaka na kuamua bila kuogopa lolote kuuza UTU wao, na kwa bahati mbaya wako kwenye SOCIAL MEDIAS na wana uhuru mkubwa wa kuonesha chochote wanachotaka kuonesha, Huenda kuwalaumu pekee haisaidii, hebu tuangalie NINI CHANZO!!? Sababu UPOROMOKAJI WA MAADILI ni kitu kinachoongezeka kwa kasi ya ajabu, kinachosikitisha zaidi wengi ni vijana WADOGO MNO kiumri ambao kimaadili yetu huenda walitakiwa wawe chini ya uangalizi wa wazazi'

Imeshatokea nawafanyia interview watu wa aina hiyo wanaoonekana ni wa AJABU kwenye jamii, na zaidi hata kwenye kipindi kuna muda ninaowaruhusu kuonesha uajabu wao, lengo likiwa JAMII IJUE KUNA HAYA YANAENDELEA, TUSILALE!! Na kubwa kuliko yote KUNA HISTORIA ZAO NINAZOZIONESHA ambazo kwa namna moja ama nyingine zinasaidia kuonesha TATIZO LILIPOANZIA'

cha kusikitisha NILICHOGUNDUA kwa asilimia kubwa CHANZO NI KIMOJA, wengi ni watoto waliozaliwa na watu walioamua kwa makusudi kabisa KUKWEPA MAJUKUMU YAO KAMA WAZAZI, HISTORIA NYINGI ZINAFANANA, MAMA anapobeba mzigo wa majukumu hadi ya kihali peke yake kuna hatari ya mengi kutokea, hasa kama MAMA anapokuwa hana kazi yoyote,

Natamani sana KUIOMBA SERIKALI kuangalia swala na sheria mpya ama KUKAZIA ZILIZOPO kuhusiana na MALEZI YA WATOTO na hasa MAJUKUMU YA WAZAZI HASA MABABA WANAOZALISHA na KUAMUA KWA MAKUSUDI KUTOKUWEPO KWENYE MAISHA YA WATOTO WAO, kwa kuendelea kuyadharau haya tunayoyaona madogo, kuna hatari ya kushangaa zaidi mbeleni'

hatukwepi tatizo kwa kukwepa KUJUA, naamini mtoto alielewa na wazazi wanaojali hata anapoharibikiwa ni ngumu kufika kwenye level ya namna hii!
KWANINI TUACHE HILI LIENDELEE!!? wakati nafasi ya kurekebisha tunayo!!? Na serikali kupitia wizara husika inawezaje kusaidia kwenye hili!!? Nini kifanyike ili kila MZAZI ATAMBUE NA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE!!!? Sababu kwa bahati mbaya matatizo yote YANAANZIA HAPO'

HEBU TUZUNGUMZE!!
 
zamaradimketema-1470822268426.jpg


Instagram post jana kabla ya kipindi from @zamaradimketema - Katika miaka 19 aliyoishi Duniani hakumbuki idadi ya wanaume ambao ameshalala nao

Akiwa amezaliwa katika Familia ya Watoto wanne ambao kila mtu ana Baba yake, kwa upande wake HAKUWAHI KUMJUA BABA YAKE

Mama yake alimzaa pembeni ya mlango wa choo, na ni mtu aliekuwa akiwa anaamini hapendwi na Mama yake mzazi kutokana na sababu tofauti kabla hajagundua ukweli

Aliwahi kujitoa kimwili katika umri mdogo ili apate hela ya kuweza kumnusuru MAMA yake mzazi kulipa Deni la mkopo wa Benki

Ametaja MASTAR WA KITANZANIA ambao ameshawahi kushirikiana nao kingono

Lakini zaidi HATAMANI kumlea mtoto atakaempata katika malezi ambayo alilelewa na mama yake

Ni malezi ya aina gani!? Kuna siri Gani!? Anayoyafanya yametokana na nini!? Historia na alipotokea tukutane LEO saa TATU kamili USIKU kupitia CLOUDS TV ndani ya TAKE ONE the new chapter.. tunaona wengi na kuwahukumu kimatendo lakini kuna siri nyingi tusizozifahamu nyuma yao ambazo zinaweza kuwa zimechangia kwa namna moja ama nyingine

Anaitwa GIGY MONEY!! USIKOSE!!!
 
Hivi kwa nini baadhi ya waTanzania tumekuwa watu wa ajabu sana? kwa nini mnataka watu tuwe na fikra zinazofanana? Hata hao akina Gigy mnaowalaumu ni waTanzania kama mimi na wewe. wana haki ya kusikilizwa just like you and him or her or them. Tuache hizi tabia za kujiona kwamba kuna baadhi yetu ndo tuna maadili au ndo tumehodhi uelewa wa mambo Fulani. Kwanza Gigy na wenzake kama yeye wamekua na uthubutu. Kuna wengi wetu sisi ni wachafu kuliko maelezo. Lakini tunaishi maisha ya uongo uongo.

Unles waTanzania tupewe kitabu standard kinachoonyesha maadili ya mTanzania ni yapi. Hivi kweli Raia million 50 na ushee bado mnataka tuwe na fikra zinazofanana?

I really get disappointed na mawazo mfu kama haya. Anayofanya Gigy chumbani yanakuhusu nini wewe?

Get life! Mjini ni kutafuta siyo kutafutana.
Inaelekea haulewi maana ya vipindi PG,V,S,N,L na kadhalika kuna kipindi vya kuangalia na watoto lakini kwa uangalizi (Parental Guidance) , kuna kipindi vya kuangalia under 16 , kuna kipindi vya Sexy (S) , kuna kipindi vya NUDITY(KAMA CHA GIGY NA YULE SHOGA) , Kuna vipindi ni lugha chafu Language (L) .... Kama bado haujaelewa tofauti ya Hivyo vipindi na vionyeshwe muda gani utakuwa na tatizo
 
Kuna watu wanazaliwa ili malengo ya shetani yatimie! Huyo binti ni sawa na mwanangu wa kuzaa ila sasa ameishafanya mengi mabaya hapa duniani. Tumwombeeni

Yaani wewe Tutor B ni mtu wa ajabu sana...una uhakika gani dhambi anazofanya Gigy Money ni nyingi na kubwa zaidi ya za kwako?Yaani umejipa cheo cha Mungu cha kuweza kuhesabu dhambi za watu na uzito wake,mtu wa ajabu sana!

Yaani dhambi za Gigy Money hazifanyi wewe uwe holy,never..

Usione mwenzako ni mdhambi zaidi kwasababu tu wewe una-sin differently..uache this hypocrisy
 
Aiseee kuna mambo kuongea ni aibu,ye anaona sifa kabisa ni sawa na yuke picha zake zilisambaa halaf akaenda kuhojiwa hana hata aibu,halaf huyu gigy ana mpenzi nadhani wamefanana akili maana utamruhusuje aongee mambo yaliyopita si ni kuaibishana huko
 
Huyu mtangazaji wa Clouds TV, Sielewi hawa watu anaowahoji lengo lake ni nini, naona upumbavu anaoongea Gigy Money kwenye kipindi chake cha Take One, najiuliza kwanini anaruhusu ujinga huu. Nilidhani amejifunza na ile ishu ya yule shoga kumbe bure kabisa
Vpi huyo mdada aliuza SUPU YAKE HAPO KWA WAPROMOTE USHOGA?
 
jamani ndugu zangu kumbukeni nanyi pia mnaocomment humu ni wazazi,walezi na kuna wengine mmekataa mimba nyngi sana!
Tuombeeni Mungu tu jamani yasitukute ktk vizazi vyetu!
Maneno mnayotoa ni Makali mnoo as if sie ni malaika
yule binti tayari yuko psychologically affected kumbuka,amekataliwa na baba,amezaliwa mazingira ya hovyo,mama mwenyewe aliyemlea wa hovyo,amekulia malezi ya kuanza mapenz miaka13 aiseeehh!!
Jamani haya mambo yapo sana kwenye jamii zetu tena gigy amewakilisha wasichana wengi mno nyuma yake.

Kingine hao we so called celebrities wa bongo wote ni km kina gigy tu ukiskiliza story zao za kitambo utakimbia
Kuanzia kina Klynn mnaowaona masupa lady mpk kina shilole na faiza wote wako under the same roof!Sema wao kipindi hicho hakukua na digital tu
Cha msingi shukuru sana Mungu wako umelelewa vyema na ukasikilza Yale uliyoambiwa mpk Leo uko hapo.
Gigy ana inferiority complex that's her problem!na akifika anapopataka atatulia!
Dada yangu kipenzi umeandika kwa hisia kali malezi waqt mwingi yanachangia s
asa kama mzazi ndio role model wake anamuelezea jinsi alivyo unategemea bint atakuwaje? mpaka apatikane mtu makhsusi wa kumshika mkono.
Pia umechambua vizuri kuhusu hawa celebrities wetu ni kama wanafuata mikumbo kujitambua ni zero ila kwa umri na ulimbukeni wao wanaona ndio mfumo mzuri wa maisha.
 
jamani ndugu zangu kumbukeni nanyi pia mnaocomment humu ni wazazi,walezi na kuna wengine mmekataa mimba nyngi sana!
Tuombeeni Mungu tu jamani yasitukute ktk vizazi vyetu!
Maneno mnayotoa ni Makali mnoo as if sie ni malaika
yule binti tayari yuko psychologically affected kumbuka,amekataliwa na baba,amezaliwa mazingira ya hovyo,mama mwenyewe aliyemlea wa hovyo,amekulia malezi ya kuanza mapenz miaka13 aiseeehh!!
Jamani haya mambo yapo sana kwenye jamii zetu tena gigy amewakilisha wasichana wengi mno nyuma yake.

Kingine hao we so called celebrities wa bongo wote ni km kina gigy tu ukiskiliza story zao za kitambo utakimbia
Kuanzia kina Klynn mnaowaona masupa lady mpk kina shilole na faiza wote wako under the same roof!Sema wao kipindi hicho hakukua na digital tu
Cha msingi shukuru sana Mungu wako umelelewa vyema na ukasikilza Yale uliyoambiwa mpk Leo uko hapo.
Gigy ana inferiority complex that's her problem!na akifika anapopataka atatulia!


Kweli hamjuo Klynn kwa kweli bora usingemiweka humo, yeye kuolewa na mzee haimaanoshi kakulia kama hao wengine...amekulia kitofauti sanaaaa hata kusoma, hata huyo gigi hamfikii 0.0005%
 
Mimi alinikera pale anasema hakumbuki idadi ya wanaume aliolala nao mana kuna wengi walikuwa wanafika dau la hata milioni mbili.

Kilichonikera hapo bila kujali ni kweli au sio kweli watu walimtangazia dau la hilo pesa ni mafundisho ambayo mabinti wanayapata kutokana na kauli hiyo, wanafikiri kumbe kujiuza kunalipa mana kuna wakati mtu atafika dau la milioni mbili.

Nawashauri watangazaji wahoji wasanii ambao wanajitambua na mfano wa kuigwa, au wale ambao vichwa ni vibovu wapewe semina kabla ya mahojio au kipindi kifanyiwe editting pumba ziondolewe
 
Back
Top Bottom